Huduma ya 'salary slip' mtandaoni imeondolewa?

Huduma ya 'salary slip' mtandaoni imeondolewa?

Awamu hii ya mama mifumo inahujumiwa Sana, awe makini Sana...
 
Lawson mkataba ulikuwa umeisha ndo maana ulikuwa unasumbua sasa hivi haitumiki tena wana mfumo wa mpya unaitwa hcmis huu umetegenezwa na sie Tz wenyeLawson mkataba ulikuwa umeisha ndo maana ulikuwa unasumbua sasa hivi haitumiki tena wana mfumo wa mpya unaitwa hcmis huu umetegenezwa na sie Tz wenye
Mfumo huu wa Lawson, tuliaminishwa, utakuwa muarobaini wa madeni kwa watumishi, ilionesha, muda wa kustaafu, kupanda cheo, kama hujalipwa mshahara n. k. Kilichomnufaisha mtumishi ni kuingiza makato ya mikopo tu, mengine hovyo tu, bora ufutwe. Sasa huo mfumo wa hcmis una sifa zipi?
 
Mkitaja sijui salary slip sijui check number kuna wadau wanaona maruweru.
 
Hii issue naona inapuuzwa, labda mpaka iongelewa na mtu maarufu. Hakuna anaejali.

Labda Kigogo atusaidie.
 
Watumishi mna shida,kila siku Ni kulalamika tu
 
Wizara ya fedha, tunaomba maelezo nini kinaendelea kwenye hii system ya salary slip portal kwani haitoa salary slip za mwezi May mwaka huu wa 2021. Salary slip za miezi ya nyuma zinapatikana.

Imefika hatua watu tunaanza kujiuliza iwapo huu ni muendelezo wa kinachoonekana ni hujuma kwa system za serikali au ni tatizo tu la kiufundi?

Tunaomba majibu kwani watumishi wanazihitaji hizo salary slip za online kwa matumizi mbalimbali kama kuchukua mikopo, n.k.

Mama Samia, kama unapita humu na huna taarifa, basi hali ndio hio hivyo tunaomba uingilie kati.

Nawasilisha.
Pole kwa mkwamo Mkuu
 
Mfumo uliokuwa unatumika kutoa Salary Government Salaries Payment Platform (GSPP) haupo tena kuna mfumo mwingine ulioanzishwa ambao ni mpya I hope utaratibu wa kupata Salary slip kwa mfumo huo utatolewa.
 
Mfumo umerudi na Kuna mabadiliko ,tazama salary slip yako upande wa kushoto juu Kuna namba zimeandikwa pale Kama zimebadilika subiria mshahara mpya mwezi huu kwa maana nyingine unapanda daraja Kama zipo vile vile wewe chapa kazi utaonekana mwaka mwingine
 
Mfumo umerudi na Kuna mabadiliko ,tazama salary slip yako upande wa kushoto juu Kuna namba zimeandikwa pale Kama zimebadilika subiria mshahara mpya mwezi huu kwa maana nyingine unapanda daraja Kama zipo vile vile wewe chapa kazi utaonekana mwaka mwingine
Screenshot_2021-06-06-13-14-20-671_com.android.chrome.jpg



Haujarudi mzee baba.
 
Back
Top Bottom