Huduma ya Train Dar - Arusha ni fedhea

Asante sana Kwa kuainisha bayana hii kero mamlaka zifanye kazi, vipi mipaka ya OSHA iko wapi , ni hatari sana
 
Hamna jambo likafanywa na CCM lisiambatane na aibu
 
Shida umeongelea sana kuhusu wazungu na sio watanzania wako!

Mkisha lipwa lipwa vihela vya kunywea maji na hawa jamaa huwa mnawanyenyekea sana na kutaka wawe first grade kila mahala.
Anyway weka point yako general vitu vikae sawa kwa ajili ya msafiri wa ndani na nje!

Pia kwa ajili ya kuvutia wasafiri wengi zaidi na ili mchi ipate mapato kuliko kukimbizana na vitu ambavyo sio sustainable.
 
Treni inafanya safari kati ya Dar Arusha, halafu unakerwa na matumizi ya kugha ya kiswahili kwenye matangazo! Ulitaka watangaze kwa lugha gani?

Kwani ikitokea umeenda kwenye nchi za hao watalii, na huko huwa wanatangaza kwa lugha gani? Mana maelezo yako karibia yote, yameegemea kwa hao watalii wako, as if ni watu special sana.

Kama unaona huduma ni mbovu, si uwashauri hao watalii wako wakodi magari maalum!
 
Stupid mind. Unajua northern cirtcuit ni kituo kikubwa cha safari za kitalii Kuanzia Arusha National Park, Tarangire National Park, Lake Manyara National, Mount Meru, Mount Kilimanjaro all the way to Serengeti na kwingineko, unajua ni idadi ya wageni wangapi wana access huduma zetu za usafiri ikijumuishwa tren?. Je unatambua Kanda ya kaskazini specifically Arusha ni ya ngapi kwa kutembelewa na kutazamwa kwenye mitandao ya usafiri ya kimataifa duniani? Kuna vitu havikupaswa kuwa kero zetu kabisa kwa sababu ni nonsense. Kwaiyo swala la kuwa na lugha 2 za kutolea maelezo kwa wasafiri ni muhimu kwakua usafiri huu ushakua international kwaiyo na wewe punguza UJINGA kidogo kwa kuelewa ilo.
 
Kwaiyo! Kwaiyo! .....kuelewa ilo! . .... kwakua! .....swala.! ....... usafiri huu ushakua...! Ona sasa! Hata kiswahili chenyewe tu, hujui! Halafu bado unataka matangazo kwa lugha za kigeni.

Jivunie lugha yako ya Taifa ewe punguani. Hiyo sababu yako ya kulazimisha matangazo kwa lugha ya kigeni, kubali tu haina mashiko.
 
Hasa kipande cha Arusha Moshi kina vumbi mno
 
Kwenye stesheni za hovyo nakuunga mkono Ila kwenye suala la lugha wasiojua kiswahili wajiongeze, mbona treni za ufaransa hawatangazi wala kuandika kiswahili?
 
Kaa kushoto na lugha zako hizo, aliyekwambia hii treni inapitia tarangire au lake manyara ni nani?
 
Mfano panda treni Ujerumani. Wanatoa matangazo kwa Kijerumani na baadaye Kiingereza, maana kuna watalii na wageni wengi. Hata ni kawaida kuona maelekezo kuhusu matumizi ya madirisha na bafu kwa lugha mbalimbali kama vile Kifaransa, kiitalia, kituruki,
 
jamani napenda kujua ratiba ya treni,kipindi cha sikukuu ilikuwa inatembea mara tatu wiki,je ni siku gani izo napenda kujua
 
Hapa Tanzania hakuna kitu ambacho serikali inaweza kuendesha kwa standard, kila kitu cha serikalini ni ovyo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…