Pia ni muhimu tukazingatia mazingira ya kazi ya hao watumishi yako vizuri? ikiwemo vitendea kazi, work load (nikimaanisha idadi ya watumishi kulinganisha na ukubwa wa kazi), motisha yakiwemo mishahara stahiki, posho, mafunzo nk. Kuna kipindi madaktari waligoma kutokana na mambo kama haya. Kama hatujawabana hawa viongozi na watawala watekeleze wajibu wao kwa wananchi badala ya kubaki kufanya ubadhirifu tutapiga makelele sana lakini hakuna kitakachoboreka kwenye huduma za wananchi zikiwemo huduma za afya.