Kuna huduma za chini chini kwa baadhi ya viongozi wa majeshi ukizitazama siyo afya kabisa kwa matumizi bora ya kodi!
Sasa hivi nchi inalalamika kuwa deni la taifa limefikia tirioni 96
Lakini kuna hizi mambo kwa baadhi tu ya watu lakini wengine wanalia na njaa
- Kuna haja gani wakuu wa majeshi wastaafu kulipwa 80% ya aliyepo madarakani wakati walitumikia nchi na kulipwa mafao yao yote kwa mkupuo?
- Kuna haja gani, au walitumia vigezo gani kwamba kila baada ya miaka minne magari ya wastaafu yanakuwa yamrchoka kwamba wanahitaji kupatiwa mapya 0KM Kila baada ya miaka 3 au 4? Wakati jamii haina ambulance
- Kuna sababu gani misiba yao na wastaafu inahudumiwa na serikali halafu misiba ya watumishi wengine wa umma tunahangaika kuchangishana walala hoi mtaani?
- Kuna haya mabasi mapya yamenunuliwa na kusambazwa nchi nzima kwa ajili ya kuwafuata watumishi wa majeshi majumbani na kuwarudisha; Je ni kweli nchi yetu inautajiri huu wa bajeti?
- Kuna mashangingi kama zawadi ya kuendea saloon kwa wake wa ....... Hili nalo linamaanisha nini katika matumizi!
Mbona hawa watu wana mishahara mikubwa tu hizi huduma nyingine VVIP kama ni mhimu kwanini isifanyike kwa watumishi wote wa uma?
Na hapo sijagusia malipo ya nafasi zingine kama
- Spika na spika wastaafu
- Majaji na wakuu wengine wa idara
- na idara zingine!
Kwamba kuwe na mabasi ya watumishi wa taasisi zingine pia!
Yaani mfano: kuwr pia na mabasi ya walimu mtaani, walimu wakifariki hata kama wamestaafu, ofisi ya mkurugenzi itoe gari na kulipia gharama kama huko majeshi wanavyotoa mabasi na helkopita!