Uchaguzi 2020 Huenda Askofu Gwajima akawa ni msaada mkubwa kwa nchi yetu

Uchaguzi 2020 Huenda Askofu Gwajima akawa ni msaada mkubwa kwa nchi yetu

Moto Ulao

Member
Joined
Jul 5, 2020
Posts
26
Reaction score
19
Tukiondoa itikadi za vyama na ushabiki usio na maana sana hasa kwa kipindi kama hiki cha uchaguzi, tujikite sasa kuangalia msaada wa mtu binafsi kwa jamii husika. Askofu Gwajima ambaye ni kiongozi wa kiroho upande wa Wakristo na mgombea ubunge Jimbo la Kawe kupitia CCM anaweza kuwa msaada mkubwa kwa jamii. Nitaweka baadhi ya shahidi amabzo kwangu naona ziko sahihi.

1. Askofu kuwa mbunge ni alama tosha kuwa kuna alama ya unyenyekevu inaongezeka bungeni, na huu ndio muda pia maimamu wetu kuamka na kuchukua nafasi bungeni. Hii itasaidia mambo yanayopitishwa na bunge kuwa na maslahi ya kiMungu ambapo Mungu ndio mmiliki wa watu

2. Muamko mkubwa kwenye kampeni za Gwajima ambapo jambo kubwa linaloongelewa na wananchi ni NJOO UTUSAIDIE ASKOFU linaonesha wazi uwezekano wa Askofu Gwajima kuwa msaada unakuja kwa kasi jimboni.

3. Sera za maendeleo zinazotolewa na Gwajima huenda zikaibadilisha Kawe kuwa mpya kama kauli mbiu ilivyo.

4. Exposer yake nje na ndani ya nchi sio ya kubezwa na mtu, ameonekana kuanza maongezi na viongozi wa serikali huku akianza mara moja utekelezaji wa ahadi hata kabla ya kuapishwa. Watu waliokuwa na migogoro ya ardhi kule Chasimba wameishapata jibu lao mapema.

5. Kama Askofu Gwajima atashinda ubunge. Huenda tukaanza kujilaumu kwanini hatukujua mapema tukamshtua agombee ile miaka 10 tuliyokuwa tunaongozwa na Halima Mdee ambaye amemaliza muda wake.

Imeandikwa na;
Mchambuzi Huru
 
Hata hii mtabisha naona. Ukiitwa upinzani sijui kitu gan huwa kinaingia kichwani aisee
 
Hakika nchi kama Tanzania ina muhitaji

Hii ni kweli kabisa kwa nchi kama Tanzania inamuhitaji mtu kama Gwajima.

Gwajima ni mtu mwenye uwezo wa kusimama mbele ya mtu yeyote na kueleza changamoto au kutoa hoja.

Gwajima hawezi akaona nchi ina matatizo akanyamaza bila kuliongelea hawezi akaona tatizo katika nchi aka lifumbia macho hivyo Tanzania tuna kila sababu ya kumkubali Gwajima kuwa kiongozi haswa kwa jimbo la Kawe.

Mwisho Tanzania tuache siasa za maisha binafsi tuangalie ukweli wa na ushujaa wa mtuu na power yake.
 
Back
Top Bottom