Huenda Kanisa la Kiboko ya Wachawi likafunguliwa hivi karibuni; huduma kuendelea kama kawaida

Huenda Kanisa la Kiboko ya Wachawi likafunguliwa hivi karibuni; huduma kuendelea kama kawaida

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Unaweza kusema ni suala la muda tu kabla kanisa la Kiboko ya Wachawi kufunguliwa na kuendelea na huduma kama kawaida. Matumaini haya yanatokana na kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke, ndugu Sixtus Mapunda ambaye amewaambia waumini wasiwe na wasiwasi wowote kuhusu kufungiwa kanisa lao. "Tunafahamu waumini wanaosali katika kanisa hili ni wapigakura wetu, hivyo suala hili halihitaji nguvu bali subira, waumini wasiwe na wasiwasi, tutamalizana tu." Alisema.​
1722366127692.png

Waumini wa kanisa la Kiboko ya Wachawi wakiwa wameshikwa na butwaa baada ya kufika kanisani hapo na kukuta viti vyote vimeondolewa na hakuna huduma inayoendelea.
Sababu za kufunguliwa huduma zipo nyingi. Baadhi ya sababu hizo ni kama ifuatavyo:

Mosi, sio mara ya kwanza serikali kufungia huduma za kiroho na kisha kuzifungua baada ya kumalizana. Desemba, 2022 huko Kivule Matembele ya Pili, kanisa la Suguye liliwahi kufungiwa kwa mbwembwe kubwa kisha likafunguliwa kimyakimya na sasa huduma zinaunguruma kama kawaida.

Sababu za kufungiwa kanisa hilo hazitofautiani na hizi za Kiboko ya Wachawi. Yeye Suguye alikuwa anatoza Tsh 300,000 wakati huo, tofauti na Kiboko ya Wachawi anayetoza Tsh 500,000 wakati huu. Kwa hiyo, kuna imani kubwa ya Kiboko ya Wachawi naye kufunguliwa huduma baada ya kumalizana na serikali kama alivyosema DC Mapunda.

Pili, Kiboko ya Wachawi amepigwa faini kubwa ambayo anatakiwa kuilipa kabla huduma hazijarejeshwa. Haijawekwa wazi kiasi cha fedha kinachohitajika kulipwa lakini inasemekana serikali imemlima faini ya mamilioni ya fedha. Jana waumini wake walianza kuchangishana kiasi cha Tsh 5,000 kila mmoja kwa ajili ya kulipa faini hiyo.

Tatu, kama alivyosema DC, waumini wa kanisa hilo ni wapigakura wazuri, hvyo serikali isingetaka kuingia mgogoro wa wapigakura kipindi hiki tunachoelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kisha uchaguzi mkuu mwaka 2025. Kila mtu anafahamu kuwa kipindi hiki serikali inakuwa karibu na wananchi kwa sababu ya kuepuka kuharibu kura. Na waumini wenye uelewa kama hawa wa Kiboko ya Wachawi ni mtaji mkubwa wa kisiasa. Sio wa kuwabeza hata kidogo.

Nne, mojawapo ya masharti ya kufunguliwa ni kumuonya Kiboko ya Wachawi aache mahubiri ya ramli chonganisha na yenye kudhalilisha hadhi ya wanawake. Kwa mfano, kuna clip moja Kiboko ya Wachawi aliwahi kusikika akisema eti yeye akiona chupi ya waumini wake lazima aichungulie hataogopa kama waumini wengine wanavyoogopa. Hapa alikuwa akiwapiga vijembe manabii wengine kama vile Mzee wa Upako, Mwamposa, GeoDevie na wengine wanaoogopa kuchungulia chupi za waumini wao pale wanapokuwa wamekaa vibaya kanisani.

Kwa sababu hiyo, Kiboko ya Wachawi sharti afunguliwe huduma lakini atatakiwa kufuata masharti ya serikali. Na ili serikali ione kama kweli masharti yake yanatimizwa, sharti imfungulie halafu imfuatilie kama kweli anatimiza au la.
Tano, sote tunafahamu kuwa serikali haina dini na kwa maana hiyo haipaswi kuingilia mambo ya dini bali kutoa maonyo pale inapohitajika. Hivyo basi, serikali haiwezi na haijawahi kufungia huduma za kiroho kwani kufanya hivyo itakuwa imeingilia mambo ya imani.

Kwa sababu hizi na nyingine ambazo bado hazijawekwa wazi, ni dhahiri kuwa huduma ya Kiboko ya Wachawi ipo mbioni kufunguliwa siku yoyote kuanzia leo baada ya faini kulipwa. Na kwa sababu waumini wameishaanza mchakato wa kuchangishana, ni suala la muda tu kabla Kiboko ya Wachawi kuanza kuunguruma tena kama ilivyokuwa mwanzo.

Pia, Soma:

 
Sasa kwanini wasijikite katika kuwaelimisha "wapiga kura" wao juu ya makanisa ya namna hii kuliko kuwasumbua hawa "mitume na manabii"??
Serikali haina na haipaswi kuwa na dini mkuu.
 
Sasa kwanini wasijikite katika kuwaelimisha "wapiga kura" wao juu ya makanisa ya namna hii kuliko kuwasumbua hawa "mitume na manabii"??
Waumini wa aina hiyo sio wa kuelimisha bali unapaswa kuwaacha wafuate kila ambacho mioyo yao inapenda bila kuwabughudhi. Hapo watakuwa na furaha na kupiga kura kwa CCM bila shuruti.
 
Haijarishi, hiyo issue ni wizara ya mambo ya ndani na waziri wa Mambo ya ndani ndio mamlaka ya rufaa kama anaona msajili amemuonea.
Hata DC anayo haki ya kutetea kura za CCM Kwa niaba ya Rais. Kati ya waziri na Rais ni nani mwenye mamlaka makubwa ktk nchi?
 
Kwa mfano, kuna clip moja Kiboko ya Wachawi aliwahi kusikika akisema eti yeye akiona chupi ya waumini wake lazima aichungulie hataogopa kama waumini wengine
Nategemea kuanzisha kanisa litakaloitwa Sexless revival center ambalo waumini watapaswa kuingia kwenye ibada wakiwa wamevaa chupi tu.

Hii inatukumbusha kuwa tulizaliwa uchi na tutarudi kwake uchi, hivyo tuabudu uchi.
 
.
 

Attachments

  • FB_IMG_1722304254670.jpg
    FB_IMG_1722304254670.jpg
    96.8 KB · Views: 10
  • FB_IMG_1722304264184.jpg
    FB_IMG_1722304264184.jpg
    105 KB · Views: 12
Nategemea kuanzisha kanisa litakaloitwa Sexless revival center ambalo waumini watapaswa kuingia kwenye ibada wakiwa wamevaa chupi tu.

Hii inatukumbusha kuwa tulizaliwa uchi na tutarudi kwake uchi, hivyo tuabudu uchi.
Haina shida na utavuna waumini na fedha za kutosha. Cha muhimu tu uisapoti serikali na kununua watu wenye njaa ili kutoa ushuhuda feki madhabahuni na kwenye social media.
 
Back
Top Bottom