Huenda Kanisa la Kiboko ya Wachawi likafunguliwa hivi karibuni; huduma kuendelea kama kawaida

Huenda Kanisa la Kiboko ya Wachawi likafunguliwa hivi karibuni; huduma kuendelea kama kawaida

Katika ile taarifa sikuona mahali lilipofungiwa bali lilifutiwa usajili
Lakini pia hakuna faini kwa aliyefutiwa usajili
 
Hii nchi ni ngumu sana aise
 
jamaa ni mkongoman..
enzi za jiwe, wange kuja kwanza uhamiaji, mara apewe kesi ya kutakatisha pesa haramu... hadi ange ondoka mwenyewe.
Sasa hivi wanalelewa kwa sababu ya serikali kuogopa kuharibu kura. Subiri kura zipite kwanza ndipo tutajua nini kinaendelea.
 
Katika ile taarifa sikuona mahali lilipofungiwa bali lilifutiwa usajili
Lakini pia hakuna faini kwa aliyefutiwa usajili
Ishushe hiyo taarifa hapa tuisome sote mkuu. Isije ikawa wewe una taarifa yako tofauti umejifungia nayo unaendelea kujipotosha bila kujua.
 
Mkuu unapaswa kutambua kuwa serikali haina dini. Serikali inaweka miongozo tu lakini haiwezi kuwazuia wananchi kufuata kile wanachokipenda. Haina mamlaka ya kufuta huduma ya kiroho bali kutoa miongozo tu na kuwaacha waumini waendelee na utaratibu wao wa maisha bila kuingiliwa na mtu yeyote.
Hapo ndipo mnapokosea kwa kuaminishwa uhuru wa dini na imani ni haki bila masharti. Kwani ukristo au uislaam haujulikani? Hao matapeli kabisa nchi gani yenye kujali watu wake itaruhusu wezi wahuni hao. Unafikiri hakuna sheria za kuwalinda watu na watu kama hao? Ndio maana tunahitaji itikadi ya kimapinduzi kuongoza nchi na sio uliberali wa magharibi unaolaghai waafrika eti utawala wa sheria badala ya utawala wa haki, au uhuru wa mahakama huku wanasheria wanauza haki.
 
Hapo ndipo mnapokosea kwa kuaminishwa uhuru wa dini na imani ni haki bila madharti. Kwani ukristo au uislaam haujulikani? Hao matapeli kabisa nchi gani yenye kujali watu wake itaruhusu wezi wahuni hao. Unafikiri hakuna sheria za kuwalinda watu na watu kama hao? Ndio maana tunahitaji itikadi ya kimapinduzi kuongoza nchi na sio uliberali wa magharibi unaolaghai waafrika eti utawala wa sheria badala ya utawala wa haki, au uhuru wa mahakama huku wanasheria wanauza haki.
Mkuu umeongea vizuri lakini ukumbuke kwamba serikali haiwezi kuzuia kile kitu kinachowapa raha wananchi hata kama kitu hicho ni cha kitapeli kiasi gani.

Wewe mwenyewe unaona jinsi waumini wanavyochachamaa kutska kanisa lao lifunguliwe. Utawazuiaje wananchi kama hawa wakuelewe bila kuvunja amani. Suluhisho sahihi ni kuwaacha tu waendelee na utaratibu wao wa ibada hata kama wewe unaona haufai.

Vinginevyo utawachukiza na kusababisha CCM kukosa kura wakati wakati wa upigaji kura. Umeona hiyo?
 
Wananchi mazuzu yana changa hayana tofauti na yale yanayo mchangia lissu anunue luxury car
 
Mkuu umeongea vizuri lakini ukumbuke kwamba serikali haiwezi kuzuia kile kitu kinachowapa raha wananchi hata kama kitu hicho ni cha kitapeli kiasi gani.

Wewe mwenyewe unaona jinsi waumini wanavyochachamaa kutska kanisa lao lifunguliwe. Utawazuiaje wananchi kama hawa wakuelewe bila kuvunja amani. Suluhisho sahihi ni kuwaacha tu waendelee na utaratibu wao wa ibada hata kama wewe unaona haufai.

Vinginevyo utawachukiza na kusababisha CCM kukosa kura wakati wakati wa upigaji kura. Umeona hiy
Tatizo linakuja sio kwa hao waomini ila hau wahuni wenye kuja na hayo makanisa kwa lengo la kujipatia kipato. Vijana wengi tena wasomi kutokana na ajira wanaanzisha shughuli za kulaghai wananchi kujipatia kipato. Bila kudhibiti hali itakua mbaya mbeleni.
 
Wananchi mazuzu yana changa hayana tofauti na yale yanayo mchangia lissu anunue luxury car
Mkuu kuwa na adabu kwa Lissu. Wewe umeridhika na haya maisha ya kishenzi tunayoishi hapa nchini? Unapaswa utambue kwamba Lissu ananunuliwa gari ili alitumie kwenye ukombozi wa umma, na wewe ukiwamo. Umeelewa?
 
Sababu ya kufunguliwa ni kwamba wanatoa rushwa kubwa. Kitu kinaonekama kabisa sio kanisa unawezaje kukiruhu kama kanisa. Lazima kutambua hii ni mission kama ile kueneza ushoga ambayo kutokana na kufadhiliwa nje wana fedha nyingi hadi kuweza kudumu hadi kugeuza vijana mamia mashoga. Hili la makanisa ni kuleta vurugu na kuwazubaisha raia kutumia akili na kufanya kazi ili wabakie masikini kwa faida ya mabeberu wenye kutaka kufaidi mali asili ya nchi zetu.
Haitotokea makanisa ya fungiwe Mazima kwa sababu yanawasaidia kupumbaza raia hawa viongozi wetu
 
Likifunguliwa matapeli watazidi kuongezeka wanaudhalilisha ukristo alafu Kwanza ni mkongo yule Bora wale kawe wanapigwa na Mbongo mwenzao uchumi unaimarika😆😆
 
Haitotokea makanisa ya fungiwe Mazima kwa sababu yanawasaidia kupumbaza raia hawa viongozi wetu
Kweli kabisa mkuu. Wakiyafungia watakuwa wanefanya kosa kubwa sana kwa kuwa yanawasaidia kuongeza idadi ya wajinga hapa nchini ili watawalike kwa urahisi.
 
Likifunguliwa matapeli watazidi kuongezeka wanaudhalilisha ukristo alafu Kwanza ni mkongo yule Bora wale kawe wanapigwa na Mbongo mwenzao uchumi unaimarika😆😆
Wa Kawe uchumi unabakia nyumbani lakini huyu Mkongo anachukua pesa zote mazima na kuzipeleka Kongo kujenga nchi yao. Kwanza halipi kodi yoyote serikalini. Inauma sana.
 
Huyo TAPELI asifunguliwe kabisa maana ni MWIZI...Kagame alifanya la maana kuwafukuza matapeli rwanda...Anachofanya ni maigizo ,waende mbele zaidi kwa kumfungia mwamposa ,kuhani mussa na matapeli wengine.
 
Hizo tozo anazotoza zimekomaliwa.Ni je watoaji huzifuata pale Lumumba au ni za kwao wenyewe? Je wamelalamika wapi kwamba tozo ni kubwa?Je anawalazimisha watoe? Je CCM kwa nini tulilalamikia tozo za simu, haikuzifuta na badala yake wanatutoza kwa nguvu na bado hawajafutiwa usajili?Why Double standard?
 
Back
Top Bottom