Huenda Kanisa la Kiboko ya Wachawi likafunguliwa hivi karibuni; huduma kuendelea kama kawaida

Suguye akiwa kwenye mkutano wake Morogoro.
Anaendelea kuvuna maokoto kama kawaida yake aise. Alifungiwa kwa mbwembwe zote kisha akafunguliwa kimya kimya. Hii nchi ni ngumu sana.
 
Sababu ya kufunguliwa ni kwamba wanatoa rushwa kubwa. Kitu kinaonekama kabisa sio kanisa unawezaje kukiruhu kama kanisa. Lazima kutambua hii ni mission kama ile kueneza ushoga ambayo kutokana na kufadhiliwa nje wana fedha nyingi hadi kuweza kudumu hadi kugeuza vijana mamia mashoga. Hili la makanisa ni kuleta vurugu na kuwazubaisha raia kutumia akili na kufanya kazi ili wabakie masikini kwa faida ya mabeberu wenye kutaka kufaidi mali asili ya nchi zetu.
 
Mkuu unapaswa kutambua kuwa serikali haina dini. Serikali inaweka miongozo tu lakini haiwezi kuwazuia wananchi kufuata kile wanachokipenda. Haina mamlaka ya kufuta huduma ya kiroho bali kutoa miongozo tu na kuwaacha waumini waendelee na utaratibu wao wa maisha bila kuingiliwa na mtu yeyote.
 
CCM huwaza uchaguzi tu Wala hakuna kingine
 
Hii taarifa imenichukiza sana, huyo jamaa atimuliwe nchi hii anaaibisha Wakristo na Ukristo kwa ujumla kanisa itapendeza sana likachomwa na moto hao waumini wakatafute makanisa mengine wamuabudu Mungu mkuu alie juu.
 
Kazi yoyote ya chama cha siasa ni kushinda uchaguzi, si vinginevyo.
Sio kweli mzee Kama upo hivyo wewe ni kundi Moja na CCM ( mjinga) kiuongozi ukichaguliwa ukawafanyia vizuri waliokuchagua huhitaji chawa Wala mwijaku haya yote yanakuja baada ya kufeli kiuongozi.
 
Hii taarifa imenichukiza sana, huyo jamaa atimuliwe nchi hii anaaibisha Wakristo na Ukristo kwa ujumla kanisa itapendeza sana likachomwa na moto hao waumini wakatafute makanisa mengine wamuabudu Mungu mkuu alie juu.
Tatizo serikali ya CCM inapenda wananchi mbumbumbu kama hawa ili iendelee kuwakamua kama ng'ombe bila kuwapa malisho. Ndio maana serikali haiwezi kuthubutu kamwe kufuta huduma. Badala yake itawaacha waendelee kuibiwa sadaka na kutopea kwenye umasikini mamboleo ili watawalike kwa urahisi.
 
Sio kweli mzee Kama upo hivyo wewe ni kundi Moja na CCM ( mjinga) kiuongozi ukichaguliwa ukawafanyia vizuri waliokuchagua huhitaji chawa Wala mwijaku haya yote yanakuja baada ya kufeli kiuongozi.
Wewe unadhani chama na serikali wanalenga kuboresha maisha ya wananchi?
 
Itakuwa nchi ya hovyo haijawahi kutokea. Au kashapewa rushwa huyo?
 
Huyo waziri wa mambo ya ndani ameulizwa kuhusu hiyo issue
Amesema hakuna barua ya kufunga kanisa iliyofika ofisini kwake
Huyo Waziri ukimuangalia tu Kichwa chake kilivyo, Zungumza yake na Macho yake hadi alivyo alivyo tu yeye Mwenyewe unaona ana Akili sawa sawa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…