Unavoidable Servant
JF-Expert Member
- Oct 13, 2021
- 1,728
- 4,545
Yeye ni mamlaka ya rufaa, ambaye hajaridhika na maamuzi ya msajiri ndio anakata rufaa kwa waziri.Huyo waziri wa mambo ya ndani ameulizwa kuhusu hiyo issue
Amesema hakuna barua ya kufunga kanisa iliyofika ofisini kwake
Sasa hivi wanalelewa kwa sababu ya serikali kuogopa kuharibu kura. Subiri kura zipite kwanza ndipo tutajua nini kinaendelea.jamaa ni mkongoman..
enzi za jiwe, wange kuja kwanza uhamiaji, mara apewe kesi ya kutakatisha pesa haramu... hadi ange ondoka mwenyewe.
Ishushe hiyo taarifa hapa tuisome sote mkuu. Isije ikawa wewe una taarifa yako tofauti umejifungia nayo unaendelea kujipotosha bila kujua.Katika ile taarifa sikuona mahali lilipofungiwa bali lilifutiwa usajili
Lakini pia hakuna faini kwa aliyefutiwa usajili
Hapo ndipo mnapokosea kwa kuaminishwa uhuru wa dini na imani ni haki bila masharti. Kwani ukristo au uislaam haujulikani? Hao matapeli kabisa nchi gani yenye kujali watu wake itaruhusu wezi wahuni hao. Unafikiri hakuna sheria za kuwalinda watu na watu kama hao? Ndio maana tunahitaji itikadi ya kimapinduzi kuongoza nchi na sio uliberali wa magharibi unaolaghai waafrika eti utawala wa sheria badala ya utawala wa haki, au uhuru wa mahakama huku wanasheria wanauza haki.Mkuu unapaswa kutambua kuwa serikali haina dini. Serikali inaweka miongozo tu lakini haiwezi kuwazuia wananchi kufuata kile wanachokipenda. Haina mamlaka ya kufuta huduma ya kiroho bali kutoa miongozo tu na kuwaacha waumini waendelee na utaratibu wao wa maisha bila kuingiliwa na mtu yeyote.
Mkuu umeongea vizuri lakini ukumbuke kwamba serikali haiwezi kuzuia kile kitu kinachowapa raha wananchi hata kama kitu hicho ni cha kitapeli kiasi gani.Hapo ndipo mnapokosea kwa kuaminishwa uhuru wa dini na imani ni haki bila madharti. Kwani ukristo au uislaam haujulikani? Hao matapeli kabisa nchi gani yenye kujali watu wake itaruhusu wezi wahuni hao. Unafikiri hakuna sheria za kuwalinda watu na watu kama hao? Ndio maana tunahitaji itikadi ya kimapinduzi kuongoza nchi na sio uliberali wa magharibi unaolaghai waafrika eti utawala wa sheria badala ya utawala wa haki, au uhuru wa mahakama huku wanasheria wanauza haki.
Tatizo linakuja sio kwa hao waomini ila hau wahuni wenye kuja na hayo makanisa kwa lengo la kujipatia kipato. Vijana wengi tena wasomi kutokana na ajira wanaanzisha shughuli za kulaghai wananchi kujipatia kipato. Bila kudhibiti hali itakua mbaya mbeleni.Mkuu umeongea vizuri lakini ukumbuke kwamba serikali haiwezi kuzuia kile kitu kinachowapa raha wananchi hata kama kitu hicho ni cha kitapeli kiasi gani.
Wewe mwenyewe unaona jinsi waumini wanavyochachamaa kutska kanisa lao lifunguliwe. Utawazuiaje wananchi kama hawa wakuelewe bila kuvunja amani. Suluhisho sahihi ni kuwaacha tu waendelee na utaratibu wao wa ibada hata kama wewe unaona haufai.
Vinginevyo utawachukiza na kusababisha CCM kukosa kura wakati wakati wa upigaji kura. Umeona hiy
Mkuu kuwa na adabu kwa Lissu. Wewe umeridhika na haya maisha ya kishenzi tunayoishi hapa nchini? Unapaswa utambue kwamba Lissu ananunuliwa gari ili alitumie kwenye ukombozi wa umma, na wewe ukiwamo. Umeelewa?Wananchi mazuzu yana changa hayana tofauti na yale yanayo mchangia lissu anunue luxury car
Haitotokea makanisa ya fungiwe Mazima kwa sababu yanawasaidia kupumbaza raia hawa viongozi wetuSababu ya kufunguliwa ni kwamba wanatoa rushwa kubwa. Kitu kinaonekama kabisa sio kanisa unawezaje kukiruhu kama kanisa. Lazima kutambua hii ni mission kama ile kueneza ushoga ambayo kutokana na kufadhiliwa nje wana fedha nyingi hadi kuweza kudumu hadi kugeuza vijana mamia mashoga. Hili la makanisa ni kuleta vurugu na kuwazubaisha raia kutumia akili na kufanya kazi ili wabakie masikini kwa faida ya mabeberu wenye kutaka kufaidi mali asili ya nchi zetu.
Kweli kabisa mkuu. Wakiyafungia watakuwa wanefanya kosa kubwa sana kwa kuwa yanawasaidia kuongeza idadi ya wajinga hapa nchini ili watawalike kwa urahisi.Haitotokea makanisa ya fungiwe Mazima kwa sababu yanawasaidia kupumbaza raia hawa viongozi wetu
Wa Kawe uchumi unabakia nyumbani lakini huyu Mkongo anachukua pesa zote mazima na kuzipeleka Kongo kujenga nchi yao. Kwanza halipi kodi yoyote serikalini. Inauma sana.Likifunguliwa matapeli watazidi kuongezeka wanaudhalilisha ukristo alafu Kwanza ni mkongo yule Bora wale kawe wanapigwa na Mbongo mwenzao uchumi unaimarika😆😆
Kiboko anatoa huduma😀DC ni mkuu wa ulinzi na usalama wa eneo ambalo Kiboko anatoa huduma.