Huenda Karia kaamua kuiabisha ligi yetu

Huenda Karia kaamua kuiabisha ligi yetu

uhurumoja

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2014
Posts
9,616
Reaction score
22,521
Ndugu zangu wanayanga na watz wengine wenye mapenzi mema na mpira wa nchi yetu

Wote Leo tumeshuhudia mechi ya nusu final Crdb ukienda live hewani kutokea pale Geneva ya afrika (Arusha)

Ndugu zangu ule uwanja ulikuwa ni tusi aibu na fedheha kwa soka la nchi yetu

Siwezi andika mengi lakini ule uwanja haufai hata kwa mashindano ya umisseta Wala umitashumita

Mda huu Zamaleki inacheza na Berkane katika uwanja halisi wa mpira na sio kile kituko Cha Karia na ndugu zake

Sio kwamba nchi yetu Haina uwanja mzuri (Mkapa,Azam,au ule wa pale Manyara (binafsi sio ule utaopigwa final ambao nao ni fedheha nyingine)lakini Karia aliamua nusu final ichezwe mwanza kwa Azam na coastal ambayo nayo ilikuwa mechi ya kituko na nyingine Arusha
KARIA JUA LEO UMEIDHARILISHA NCHI YETU.

Ngoja niendelee kuangalia Cafcc soka safi kwenye uwanja safi
 
Akubali kwa Sasa mechi zichezwe Mkapa hasa hizi ambazo uwezekano wa kufatiliwa na watu wa nje ni mkubwa au chamazi
Wanafanya hivo ku neutralize ground kusiwe na visingizio vya watu kubebwa mana unapoweka mechi uwanja wowote WA dar watu watasema tu azam,Simba na yanga zinabebwa mechi za nusu kila mwaka wao wanacheza nyumbani
 
Uwanja wa Taifa dunia nzima huwa ni neutral mkuu
Simba na Yanga Tanzania nzima ni home ground mi nasemea kwa taswira ya nchi hasa tunapoelekea hiyo Afcon 2027 hiki wqnachofanya ni Cha kipuuzi
 
Huwa mnalalamikia kila kitu ila hapo mlitaka afanyaje tena maana hizi mechi kuchezwa dar peke yake nayo ni aibu nyingine kwenye Taifa.
Mtoto hutambaa kwanza kabla hajatembea Kisha kukimbia
Ikiwa wanataka mechi zichezwe mikoani subra ivutwe kumbuka 2027 sio mbali
Arusha Dom kutakuwa na viwanja Bora mechi zichezwe wakati huo sio Sasa
Angalia hii final ya Cafcc utaona maana ya uwanja mzuri
 
Uwanja wa Taifa dunia nzima huwa ni neutral mkuu
Simba na Yanga Tanzania nzima ni home ground mi nasemea kwa taswira ya nchi hasa tunapoelekea hiyo Afcon 2027 hiki wqnachofanya ni Cha kipuuzi
Kwa jinsi ilivyo nchi yetu kwa soka taifa ni ya vigogo at least mikoani kidogo unaweza ukapata taswira tofauti.pia kucheza umashindano uwanja mmoja kila mwaka inaboa ndugu
 
Mkuu unaangalia mechi ya final cafcc mda huu!?Azam 3
 
Kwa jinsi ilivyo nchi yetu kwa soka taifa ni ya vigogo at least mikoani kidogo unaweza ukapata taswira tofauti.pia kucheza umashindano uwanja mmoja kila mwaka inaboa ndugu
Wembley Ina host Kila msimu FA na baiboi
Nadhani kinachoweza kuboa labda ni team kuwa zile zile ila uwanja kuboa hapana
Binafsi Sina tatizo na mechi kuwa nje ya dar(Mkapa au chamazi)ila viwanja hivi vikavu nyasi mpira unadunda sio sawa kwa mustakabali wa mpira mzuri
 
Mkuu usifosi 2 kuwa Moja wenzetu wametutangulia sisi bado tunatambaa muda ukifika tutasimama na kutembea pia
Sio kwamba wametangulia ni kwenye mashindano makubwa wanachagua uwanja mzuri kutumika na sisi tungeweza kucheza Mkapa kama Mkapa usingekuwepo tungekubali kuwa haupo basi ila upo utumike huo
 
Ndugu zangu wanayanga na watz wengine wenye mapenzi mema na mpira wa nchi yetu

Wote Leo tumeshuhudia mechi ya nusu final Crdb ukienda live hewani kutokea pale Geneva ya afrika (Arusha)

Ndugu zangu ule uwanja ulikuwa ni tusi aibu na fedheha kwa soka la nchi yetu

Siwezi andika mengi lakini ule uwanja haufai hata kwa mashindano ya umisseta Wala umitashumita

Mda huu Zamaleki inacheza na Berkane katika uwanja halisi wa mpira na sio kile kituko Cha Karia na ndugu zake

Sio kwamba nchi yetu Haina uwanja mzuri (Mkapa,Azam,au ule wa pale Manyara (binafsi sio ule utaopigwa final ambao nao ni fedheha nyingine)lakini Karia aliamua nusu final ichezwe mwanza kwa Azam na coastal ambayo nayo ilikuwa mechi ya kituko na nyingine Arusha
KARIA JUA LEO UMEIDHARILISHA NCHI YETU.

Ngoja niendelee kuangalia Cafcc soka safi kwenye uwanja safi
Karoia ni msomali hivyo hana cha kupoteza Kwa maslahi ya soka la Tanzania.
 
Mpaka ccm inyang'angwe viwanja vitabaki hivo hivo siku zote
Maccm ni majizi kweli eti kila kiwanja cha mpira ni mali ya ccm.

Wakati viwanja vote tulijitolea kujenga kipindi cha chama kimoja.

Hapa ilibidi viwanja vote virudishwe chini ya umiliki wa serikali.
 
Attachments

  • Screenshot_20240510-200253.png
    Screenshot_20240510-200253.png
    1.3 MB · Views: 4
Back
Top Bottom