Huenda Ndugai alikuwa anajua tulichokuwa hatukijui, sasa tunakiona cha mtema kuni

Sasa mbona serikali haipunguzi matumizi yao kuendana na hali halisi? Wakati sisi tunaminyana kwenye tozo wao wanadai magari mapya ya kifahari na wengine ndio washajinunulia magari yenye kuweza kujenga hivyo vituo vya afya.
 
Huyo babu alikua sahihi.

Ila ndio hivyo tena pressure ya mamlaka ni kubwa kuliko haki kwa wananchi.

Ubaya zaidi ni pale mwenye mamlaka anapokua tofauti na yule mwenye nafasi hiyo ya kufanya maamuzi kuwanusuru wananchi.
 
Mkuu mbona kama ndugai alikuwa anataka tozo ziwepo au sijaelewa hapo?

Amesema tozo ziwepo ili tuijenge nchi yetu wenyewe sasa huyu alikuwa na huruma na sisi wananchi au ni vipi?

Me naona wale wale tu.
Mkuu izi vitu zina operate katika namna ambayo ni complicated kidogo... ukitaka kupata picha jiulize maswali kama haya, ni kwa nini serikali ndiyo inayotengeneza na kumiliki pesa ya nchi yake lakini wanataka izo pesa ziende kwa wananchi then wazichukue tena hata kwa dhuruma, utagundua kwamba maisha na uchumi wa taifa lolote linasimama kwa shuguli za uzalishaji(kilimo, ufugaji, viwanda na zingine nyingi) ambazo sisi walala hoi ni lazima tufanye.. ili tabaka tawala waishi kifalme.
Sasa izi issue za mikopo aliyoipigia kelele jamaa inafanya kazi katika mtindo kama huo, kinachorudishwa hapo ni asilimia fulani ya shughuli za uzalishaji na rasilimali za nchi ambazo kwa kiasi kikubwa tunakuwa kama tunawafanyia kazi hao mabwana wanaotukopesha,

Rejea maneno ya magu, mala nyingi alikuwa akisema hawa wakopeshaji wangekuwa na nia njema wangeacha kutukopesha au kusamehe madeni kabisa ili tunachokikusanya ndani ya nchi kifanye maendeleo... kwa sababu what happens, wanakupa mkopo then katika makusanyo yako ya mwezi ama mwaka(uzalishaji wako)... kuna asilimia ni moja kwa moja inalipa ayo madeni, japo kujinasua kwene hii mifumo ni ngumu... fatilia kuna documentary za watu wanaitwa economic hitmens zinaweza kukuongezea uelewa wa jinsi gani ivi vitu vinafanya kazi, inaumiza ila hatuna jinsi
 
Ndugai wewe ulikuwa muoga hata Jiwe ulimuunga mkono kiuoga tu!! sasa imekugharimu na huyu ni wewe usibishe!
 
Kuwa kiongozi mkuu wa muhimili mmoja mkubwa kati ya mitatu sio nafasi ndogo.
Ndugai wacha uongo!! hiyo ni kazi tena tamu sana km zilivyo kazi nyingine usitutishe hapa!! k vepi waiache wazi leo uone watu watakavyo changamkia! kma ni nafasi ndogo kwako siyo sisi!
 

Ndugai hakupinga tozo, yeye alikuwa mfuasi na muumini mzuri wa tozo. Yeye alichokipinga ni mikopo tu...
 
Angekuwa serious angeachia ubunge aingie upinzani apambane kweli kweli tofauti na hapo ni tapeli tupu
Nyerere alisema upinzani halisi utatoka ndani ya chama tawala chenyewe. Si lazima kujiunga na chama cha upinzani. Ona sasa ni miaka 30 tangu upinzani uruhusiwe nchini. Nini walichoweza kufanya kubadili sera za taifa? Lakini mwana CCM akiwa jasiri kweli na kusema hoja zake ndani ya chama atasikilizwa. Ilianza kuonekana hivyo chini ya Magufuli na kama angemaliza miaka 10 ya uongozi bila shaka kungeonekana mabadiliko.
 
Alikuwa zaidi ya shetani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…