Ni ukweli usiopingika kwamba Watu maarufu hawa Mwanamuziki Nasib Abdul ( Diamond Platinum ) na Msanii wa Maigizo na Mlimbwende Wema Sepetu ( Sepenga ) ni Watu wenye ' Nyota ' kali sana za Kimafanikio katika maisha yao ya kila siku na ndiyo utaweza kuona kila siku wanasema / wananangwa na wengi lakini ndiyo wanazidi tu kutuacha Kimafanikio huku Sisi tukibaki tu majungu yetu na Wivu mioyoni mwetu.
Nadhani imefika muda sasa akina Diamond na Sepenga watugawie Sisi wengine sehemu tu ya ' Nyota ' zao za ' Jaha ' ili nasi basi tuweze ' Kutusua ' Kimaisha na tuwe na mafanikio badala ya Sisi kuwekeza tu katika kuwapiga wao majungu huku umasikini / ufukura ukitutawala hadi katika Kope za macho yetu.
Nawasilisha.