Huenda Rais Samia anawaamini wasaidizi wake walioshiba wanapowasemea wenye njaa

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2020
Posts
279
Reaction score
480
Nachukua fulsa hii kumpongeza mama kwa kazi kubwa anazo zifanya kwa taifa hili tena ukizingatia amepokea kijiti kama mpira wa krosi ya kubabatizwa, lakini anajaribu kuutuliza mpira utulie hili aweze kuucheza.

Nikirudi katika mada

Hili lilionekana zaidi ile siku alipokuwa akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili BBC kuhusu tozo, na kama utaweza kuirudia hile video unaweza kuona mama alikuwa akijibu kitu ambacho amekifanyia kazi. Yaani mama alikuwa anaongea kwa uhakika na amejiridhisha vya kutosha kwani inawezekana aliwauliza labda mawazili wake wawili labda akiwemo wazili wa fedha pia.

Lakini kuna ukweli wa walivyo mdanganya mama, kwa mfano nauli ya kutoka Morogoro mpaka Dar iende irudi ni shilingi 16,000 zamani mtu akitaka kutuma 1,000,000 alitumia mtandao wowote kutuma lakini leo kwa kiasi hicho unakatwa takribani 40,000.
sasa 40,000 - 16,000 = 24,000 kama mtu anaokoa 24,000 si bora asafiri tu, sasa hawa ni wachumi gani wanamshauri mama. Kwanza tunajazana katika mabasi bila sababu pili maambukizi ya Korona yasiyo ya lazima unapata kusafiri.

Jana ghafla kwa mara ya kwanza katika serikali ya awamu ya 6 tumesikia kupitia kwa katibu wa wizara ya afya kuwa serikari inatoa wito katika matumizi ya nyumgu na dawa za kienyeji. Sisi wengine tumestuka kitu ambacho mwanzoni tuliwasikia mawaziri wanafki na mmoja alienda mbali zaidi na kusema lile jengo la nyungu pale Muhimbili libomolewe haraka kwani lina tutia aibu kama taifa. Na taarifa tulizozipata lilisha bomolewa sasa sijui litajengwa tena au.

Ushauri wangu kwa mama nadhani aingie jimboni mwake upya anze kujua ukweli kuliko kuwaamini Yesu aliowai kuwaita wanafkhi.
Na mimi kama mtoto wa mchugaji namsimamisha mama katika imani ya Mfalme Sulemani ambaye aliitafuta hikhima zaidi kuliko wapambe.
 
Changamoto ni hiyo hataki kutoka na kukutana na wananchi sio lazima asimame barabara, anaweza kwenda hospitalini au Sokoni mfano soko la ndugai akazungumza na wale watu wakampa taarifa za ukweli, atoke aende FIELD aache kukaa tu ndani haimsaidii

Waziri wa fedha alitakiwa ambadilishe tokea ule ubadhirifu wa mwezi wa 5 naona kaamua kuendelea nae, juzi kasema watu wahamie burundi kaamua kuendelea nae.

Ni mzito wa kufanya maamuzi Samia
 
Back
Top Bottom