Huenda utekelezaji wa mipango kamili ya uhani ilipangwa kufanyika kuanzia Oct.29.2025

Huenda utekelezaji wa mipango kamili ya uhani ilipangwa kufanyika kuanzia Oct.29.2025

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
51,453
Reaction score
41,274
Kama taifa tunafaa kuvipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kufanikiwa kudhibiti uhuni ule wa wahaini, ambao ulipangwa kwa ustadi mkubwa na vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi waliojificha ndani ya baadhi ya vyama vya siasa nchini.

Ni muhimu sana hatua kali za kisheria kuchukuliwa haraka tena bila huruma wala haya dhidi ya wale wote waliohusika na mipango hiyo haramu ya kuvuruga nchi, umoja, amani na mshikamano miongoni mwa waTanzania kwa maslahi binafsi ya familia zao na mabwenyenye waliowatuma. Hatua kali za kisheria na adhabu kali sana ichukuliwe dhidi yao ili hatimae iwe fundisho kwa vibaraka wengine na mamaluki wao waliopo ndani na nje ya nchi, wasithubutu kujaribu kupanga hiyo nonsense.

Vitendo vya kujaribu kuzuia na kuvuruga uchaguzi ni ushahidi tosha na wa wazi wa vitendo vya kuwatia hatiani wote wenye tuhuma za uhaini nchini.

Mahakama huru za Tanzania zinafaa kuchukua hatua haraka iwezekanavyo na kuwatia hatiani wahusika wote bila kubabaika na hatimae kufikia muafaka wa mapema dhidi ya hao wahuni waliopanga kuharibu Taifa letu, hatakama watasingizia kuskia njaa vizimbani.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom