Tetesi: Huenda Wakati wowote kuanzia Sasa Boniface Jaco, Yericko Nyerere na Emmanuel Ntobi wakavuliwa uongozi na kufukuzwa Uanachama

iyo rahisi kihivyo...kwa kosa lipi? kutoa maoni?
 
Vijana wa MBOWE DJ hao. Ije mvua lije jua hawawezi kufukuzwa.Labda waende tofauti na DJ AFM
 
Well said, waezingua sana na wanastahili kuomba msamaha na kuwajibika.
Watu wamefilisika, kuna waliofungwa kuna walioteswa na kuna walioawa na wengine wamepotea babu ya imani yao kwa Chadema
 
Bora Boni yai na Yeriko wanaweza kuomba msamaha na kusamehewa ila Ntobi, avuliwe uanachama mara moja,
 
Bado sana, ile katuni ya kipanya ya jamaa anasubiri kuzika haitofikia , wala CHADEMA haifi.
 
Kiukweli cdm wakatae kila aina ya uchawa la sivyo kitajifia
 
Hii kama ni Wenje asitafute mtu wa kufa naye , kutaja watu flani mbele ya lissu kwamba waeisha lamba , wenda ulikua ulaghai wa kitapeli ili lissu aingie mkenge, Wenje kama ndie awake ushahidi usio na shaka mezani ,ili tujue kama kweli alichokipresent kwa lissu kina ukweli, kumtajia mtu list kwamba uyu tiyari , yule tiyari hitoshi, Wenje kama ndie basi ni tapeli wa kisiasa
 
wafuasi wa Lissu mutafute chama cha kujiunga nacho, Hamuna uwezo wa kushinda uchaguzi
 
Namkubali Mbowe na ni mwanasiasa aliyechangia kwa kiasi kikubwa sana kuhuisha siasa za kizazi kipya cha siasa cha vijana kuanzia miaka ya mwanzoni mwa 2000.

Hawa akina Zitto,Lema,Mnyika,Mdee,Regia(RIP),Heche,Wenje,Kafulila,Sugu,Mkosamali etc watakuwa ni wanafiki sana wakikana kuvutiwa na Mbowe kabla hawajaingia kwenye siasa.Wengine (mfano Lema)ameiga hadi uongeaji wa Mbowe akiwa Jukwaani!

Lakini sivutiwi na namna ambayo Mbowe AMA anataka kuondoka kwenye nafasi ya uwenyekiti bila heshima inayoendana na legacy aliyoiweka kwenye siasa za upinzani kwa karibia miaka 30 sasa AU kuendelea kuwa mwenyekiti wa chama kilichomeguka kwa kiasi kikubwa kwa sababu ya uamuzi wake wa kugombea.Siamini kama Mbowe atagombea uenyekiti.Mbowe anajua umuhimu wa hilo kuliko sisi wengine.Alipaswa na najua anajua,kuachia nafasi hiyo bila kushindwa uchaguzi.Atoe baraka zake kwa wenye nia ya kugombea kujitokeza na kuchukua fomu na kuweka msimamo thabiti kuwa yeye sasa atakuwa tu ni mzee wa chama na mshauri wa karibu sana wa mwenyekiti mpya.

Hata akigombea na kushinda bado hiyo itaacha sintofahamu ndani ya chama na nje ya chama.Ndani ya chama ni kama hii misuguano inayoendelea.Itakuwa mikubwa zaidi baada ya uchaguzi regardless nani ameshinda ikiwa Mbowe pia atakuwa ni mgombea.Nje ya chama ni ileile hali ambayo wapinzani wao wataendeleza kuimba nyimbo zilezile za chama kukosa watu wenye uwezo ndomana mwenyekiti ni wa miaka zaidi ya 20.Nyimbo za chama cha demokrasia kukosa demokrasia ya kupokezana vijiti kwenye uongozi na pia nyimbo za ukanda.Nimeziita nyimbo kwa sababu zinajibiwa kwa hoja nzuri tu lakini kwa nini kila siku iwe kujibu kitu hichohicho tu?Ni fursa kwa mwenyekiti Mbowe kufuta na kuzizika hizi nyimbo kwa kutangaza kutogombea nafasi ya uwenyekiti.

Heshima kubwa kwake Freeman Aikael Mbowe kwa kukifanya chadema kuwa chama kikubwa cha upinzani na tishio kwa watawala.Ningefurahi zaidi heshima hiyo iendelee kudumu bila kuwekewa doa lolote.Binafsi kwangu Mbowe ndiye mwanasiasa bora wa upinzani nchini kuanzia mwaka 2000 hadi sasa.
 
Lissu sio makamu wa mwenyekiti alishajivua
 
Na iwe hivyo 🤣 🤣 🤣 🤣 Watimuliwe!!
 
Yeriko si ndiye Look-us Muwasha-mbwa wa Mwenyekiti? Au?
 
Kazi inaendelea huko CHADEMA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…