Huenda yumo humu JF

Huenda yumo humu JF

Wanajamvi, utu uzima unazidi kuyoyoma, miaka 33 inakatika sina wa ubani mie. Huenda yumo humu jamvini aliye mpweke kama mie, binti maridhawa, mpenda maendeleo, asiyezidi miaka 30, elimu angalau asiwe chini ya kidato cha nne, anayejituma katika kufanya kazi mvivu simtaki akha! Kupima Virusi vya UKIMWI muhimu tena asiwe macho juu penzi tamu atapata.

Uliye tayari nitumie PM.

utakapompata na kafikia muafaka wa kufunga pingu za maisha, msisahau kutualika na sisi wanaJF tuje kuhudhuria.
 
Nitapata kweli mie?

wapaswa kuvumilia, huku ukimwomba Mungu,
huna haja ya kulia, wewe zitazame mbingu,
kushoto ama kulia, kama u mwenye utungu,
mke aliye wa ndoa, aja mithili ya wingu
 
bubu ataka kusema, heshma umesheheni,
hakima wewe watema, bure hapa jamvini,
yafaa kwake wa ndima, judi daima makini,
mola akupe uzima, heri nyingi maishani

Bado kidogo niruke, kwa furaha nliposoma,
Mapigo yanilipuke, moyo uende mrama,
Kumbe niache makeke, Judi makini daima

Mwenzenu namtafuta, binti mwerevu wa mana,
Penzi bora likiambata, maisha tukisaidiana,
Aliyempweke namwita, penzini kufungamana
 
Huenda tayari anae ndo maana hajajiweka hapo

mie bado kumpata, japo miaka yaenda,
pia sinayo haraka, presha bado kupanda,
wajapo wengi wakaka, wenye kujua kupenda,
mmoja nitamtaka, kwake huyo nitaenda
 
wapaswa kuvumilia, huku ukimwomba Mungu,
huna haja ya kulia, wewe tegemea mbingu,
kushoto ama kulia, kama u mwenye utungu,
mke aliye wa ndoa, aja mithili ya wingu

Hakika navumilia, mpaka nitapompata,
Kwa Mwenyezi naaminia, katu hawezi nitupa,
Ubavu kunipatia, na ndoa ikiambata,
Machangu siwezi rukia, nitaoza kama 'mbata'
 
mie bado kumpata, japo miaka yaenda,
pia sinayo haraka, presha bado kupanda,
wajapo wengi wakaka, wenye kujua kupenda,
mmoja nitamtaka, kwake huyo nitaenda

Kumbe nawe u-mpweke, hilo katu sikujua
Labda umri uweke, wanajamvi wapate jua,
Bahati usiipige teke, akupendae wamjua?
 
Kumbe nawe u-mpweke, hilo katu sikujua
Labda umri uweke, wanajamvi wapate jua,
Bahati usiipige teke, akupendae wamjua?

ndoa haina bahati, yajengwa nao upendo,
muhimu kuwa thabiti, upate epa uvundo
hata pasipo na cheti, penzi huleta uhondo,
kwa umri niko fiti, hata kwa mwendo mdundo,
 
ndoa haina bahati, yajengwa nao upendo,
muhimu kuwa thabiti, upate epa uvundo
hata pasipo na cheti, penzi huleta uhondo,
kwa umri niko fiti, hata kwa mwendo mdundo,

Je naweza kukupenda, penzilo nijikomiti,
Moyo usije kukonda, kama umri uko fiti,
Usinifanyie inda, Wa Ndima nijidhatiti?
 
Mmenikumbusha kipindi cha malenga wetu kilikuwaga rtd zamaaaani nikiwa mtoto , nyie mnapendezea chukuaneni
 
Je naweza kukupenda, penzilo nijikomiti,
Moyo usije kukonda, kama umri uko fiti,
Usinifanyie inda, Wa Ndima nijidhatiti?

kupenda hilo waweza, kama waume wengine,
wewe walenga kupoza, wataka asali urine,
sitaki kukuchokoza, nia yako usikane,
ya kwako haitakoza, umelengesha mapene,
 
kila la kheri wa ndima, mwandani mtie ndani,
ziwe kidogo gharama, za pete pia vidani,
pamoja mali kuchuma, ziwafae maishani,
tena muepuke ngoma, wana mpate sheheni

Judi mama wa hekima,bila hiana shauri,
Kijana mwama wandima,ahitaji si kidari,
atakwenda hata kupima,iwapo kipo kigori,
Heri mwana wewe heri,mpate aliye kimwana,

Sina mengi kwa hilo,mora akupe nguvu,
ushauri kwetu ulo,umpate wako ubavu,
hata kama nyalukolo,wala isiwe mabavu,
heri mwana wewe heri,mpate aliye kimwana,
 
Wanajamvi, utu uzima unazidi kuyoyoma, miaka 33 inakatika sina wa ubani mie. Huenda yumo humu jamvini aliye mpweke kama mie, binti maridhawa, mpenda maendeleo, asiyezidi miaka 30, elimu angalau asiwe chini ya kidato cha nne, anayejituma katika kufanya kazi mvivu simtaki akha! Kupima Virusi vya UKIMWI muhimu tena asiwe macho juu penzi tamu atapata.

Uliye tayari nitumie PM.
usisahau kupima na ujauzito,sio ukimwi peke yake.maana siku hizi kubambikiwa kwingi
 
kupenda hilo waweza, kama waume wengine,
wewe walenga kupoza, wataka asali urine,
sitaki kukuchokoza, nia yako usikane,
ya kwako haitakoza, umelengesha mapene,

Kupoza katu siwezi, nimejifunza kupenda,
Naweza kuwa mshenzi, nkiendekeza 'kudanda',
Kunichokoza mapenzi, hata mabegani panda
La 'Mapene' siliwezi, jando mi nilifundwa
 
usisahau kupima na ujauzito,sio ukimwi peke yake.maana siku hizi kubambikiwa kwingi

Nimeshindwa kukupa senksi, maana kitufe sioni,
Kwa ushauri nakupa maksi, kuchunguza kwa makini
Kweli kubambikwa nuksi, kisukari umebaini
 
Judi mama wa hekima,bila hiana shauri,
Kijana mwama wandima,ahitaji si kidari,
atakwenda hata kupima,iwapo kipo kigori,
Heri mwana wewe heri,mpate aliye kimwana,

Sina mengi kwa hilo,mora akupe nguvu,
ushauri kwetu ulo,umpate wako ubavu,
hata kama nyalukolo,wala isiwe mabavu,
heri mwana wewe heri,mpate aliye kimwana,

Nimekubali,
we mkali,
umeshuka mashairi,
utadhani huna akili,
pongezi wastahili, lol
 
Kupoza katu siwezi, nimejifunza kupenda,
Naweza kuwa mshenzi, nkiendekeza 'kudanda',
Kunichokoza mapenzi, hata mabegani panda
La 'Mapene' siliwezi, jando mi nilifundwa

mapenzi ya kujifunza, si matamu asilani,
ya asili hutaweza, nimekutia shakani,
usijeanza kuwaza, mfanye vipi mwandani,
hata ukinywa ya pweza, iko chini burudani,
 
Back
Top Bottom