Husninyo
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 23,851
- 9,472
All the Best Mkuu Ukifanikiwa, niambie na mimi nijaribu....
na wewe jamani?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
All the Best Mkuu Ukifanikiwa, niambie na mimi nijaribu....
Wanajamvi, utu uzima unazidi kuyoyoma, miaka 33 inakatika sina wa ubani mie. Huenda yumo humu jamvini aliye mpweke kama mie, binti maridhawa, mpenda maendeleo, asiyezidi miaka 30, elimu angalau asiwe chini ya kidato cha nne, anayejituma katika kufanya kazi mvivu simtaki akha! Kupima Virusi vya UKIMWI muhimu tena asiwe macho juu penzi tamu atapata.
Uliye tayari nitumie PM.
Nitapata kweli mie?
Nitapata kweli mie?
bubu ataka kusema, heshma umesheheni,
hakima wewe watema, bure hapa jamvini,
yafaa kwake wa ndima, judi daima makini,
mola akupe uzima, heri nyingi maishani
Huenda tayari anae ndo maana hajajiweka hapo
wapaswa kuvumilia, huku ukimwomba Mungu,
huna haja ya kulia, wewe tegemea mbingu,
kushoto ama kulia, kama u mwenye utungu,
mke aliye wa ndoa, aja mithili ya wingu
mie bado kumpata, japo miaka yaenda,
pia sinayo haraka, presha bado kupanda,
wajapo wengi wakaka, wenye kujua kupenda,
mmoja nitamtaka, kwake huyo nitaenda
Kumbe nawe u-mpweke, hilo katu sikujua
Labda umri uweke, wanajamvi wapate jua,
Bahati usiipige teke, akupendae wamjua?
ndoa haina bahati, yajengwa nao upendo,
muhimu kuwa thabiti, upate epa uvundo
hata pasipo na cheti, penzi huleta uhondo,
kwa umri niko fiti, hata kwa mwendo mdundo,
Je naweza kukupenda, penzilo nijikomiti,
Moyo usije kukonda, kama umri uko fiti,
Usinifanyie inda, Wa Ndima nijidhatiti?
kila la kheri wa ndima, mwandani mtie ndani,
ziwe kidogo gharama, za pete pia vidani,
pamoja mali kuchuma, ziwafae maishani,
tena muepuke ngoma, wana mpate sheheni
Nitapata kweli mie?
usisahau kupima na ujauzito,sio ukimwi peke yake.maana siku hizi kubambikiwa kwingiWanajamvi, utu uzima unazidi kuyoyoma, miaka 33 inakatika sina wa ubani mie. Huenda yumo humu jamvini aliye mpweke kama mie, binti maridhawa, mpenda maendeleo, asiyezidi miaka 30, elimu angalau asiwe chini ya kidato cha nne, anayejituma katika kufanya kazi mvivu simtaki akha! Kupima Virusi vya UKIMWI muhimu tena asiwe macho juu penzi tamu atapata.
Uliye tayari nitumie PM.
kupenda hilo waweza, kama waume wengine,
wewe walenga kupoza, wataka asali urine,
sitaki kukuchokoza, nia yako usikane,
ya kwako haitakoza, umelengesha mapene,
Judi mama wa hekima,bila hiana shauri,
Kijana mwama wandima,ahitaji si kidari,
atakwenda hata kupima,iwapo kipo kigori,
Heri mwana wewe heri,mpate aliye kimwana,
Sina mengi kwa hilo,mora akupe nguvu,
ushauri kwetu ulo,umpate wako ubavu,
hata kama nyalukolo,wala isiwe mabavu,
heri mwana wewe heri,mpate aliye kimwana,
Kupoza katu siwezi, nimejifunza kupenda,
Naweza kuwa mshenzi, nkiendekeza 'kudanda',
Kunichokoza mapenzi, hata mabegani panda
La 'Mapene' siliwezi, jando mi nilifundwa