Haya maisha ukitafakari sana utagundua si chochote si lolote, ni masikitiko matupu na kujidanganya. La msingi ni kufanya kila liwezekanalo kuwatabasamisha watu wako wachache utakaoweza (maana wengi huwezi) na kisha kujiondokea zako kwenda kukutana na mwenyewe aliyekuumba.
Nafurahi kusikia kuwa huyu mheshimiwa kamwe hajawahi kuwa na maisha ya kujidai kwa wananchi wenzake wa Kilwa. Daima moyo wake na harakati zake zote zilikuwa kuwatetea na kuwainua wanaKilwa wenzake. Hata hapo, akiwa katika hali hiyo, yupo kwenye kikao na anatoa mchango wake kwa maendeleo ya Kilwa.
Angelikuwa mwepesi tu wa imani basi angekuwa ndani amejifungia. Mungu ambariki sana!