Hujafa hujaumbika: Huyu ndio yule Sulemani Bungara (Bwege)

View attachment 2868973

Haya maisha ukitafakari sana utagundua si chochote si lolote, ni masikitiko matupu na kujidanganya. La msingi ni kufanya kila liwezekanalo kuwatabasamisha watu wako wachache utakaoweza (maana wengi huwezi) na kisha kujiondokea zako kwenda kukutana na mwenyewe aliyekuumba.

Nafurahi kusikia kuwa huyu mheshimiwa kamwe hajawahi kuwa na maisha ya kujidai kwa wananchi wenzake wa Kilwa. Daima moyo wake na harakati zake zote zilikuwa kuwatetea na kuwainua wanaKilwa wenzake. Hata hapo, akiwa katika hali hiyo, yupo kwenye kikao na anatoa mchango wake kwa maendeleo ya Kilwa.

Angelikuwa mwepesi tu wa imani basi angekuwa ndani amejifungia. Mungu ambariki sana!
Unajua ukiwa binadamu unatakiwa uwe tayari kwa lolote. Ukijua hili utaishi kwa amani. Sababu mleta mada unaweza ukafa kesho na ukamuacha Mh. Bwege na yeye 2025 akarudi Bungeni na akapelekwa nje na kupewa matibabu mazuri.
 
Huyu mzee kuna meme yake inatamba sanaa mpaka kenya wanaitumia kama sijakosea ni wa ACT wazalendo na alitoka madaraka ule uchaguzi wa kupita bila ya kupingwa.
Shukran sana kwa ufafanuzi kuna libwege hapo juu linaniambia nikamsearch youtube sasa si ningependa bila kuuliza humu
 
Yote ni bure katika maisha, maisha ya binadamu yamejaa huzuni kuliko furaha!!
Mimi nimeshiriki mazishi na mortuary nimeingia sana hata kuandaa maiti watu wa mtaani ...Acha tu maisha ni bure kabisa unaweza kuona binadamu sio kitu kabisa dk kadhaa tu basi hauna ujanja.

Maisha ni ubatili tuishi kwa kupendana , matabaka yapo ila unashangaa puuh! Umepata ajali na kuparalyze basi habari yako kwisha hauna ujanja tena.
 
Huyu ndiye aliyesema majimbo ya uchaguzi Zanzibar ni kama vijiji ukipuliza mluzi jimbo zima wanasikia.
Au nasema uongo ndugu zangu.
Yule ni Kessy wa Rukwa huko. Alikuwa haipendi Zanzibar yule! kuna siku alitolewa bungeni kwa ulinzi mkali baada ya kusema Zanzibar inahudumiwa kila kitu na Tanganyika na maneno mengine ya kuwaudhi.
 
View attachment 2868973

Haya maisha ukitafakari sana utagundua si chochote si lolote, ni masikitiko matupu na kujidanganya. La msingi ni kufanya kila liwezekanalo kuwatabasamisha watu wako wachache utakaoweza (maana wengi huwezi) na kisha kujiondokea zako kwenda kukutana na mwenyewe aliyekuumba.

Nafurahi kusikia kuwa huyu mheshimiwa kamwe hajawahi kuwa na maisha ya kujidai kwa wananchi wenzake wa Kilwa. Daima moyo wake na harakati zake zote zilikuwa kuwatetea na kuwainua wanaKilwa wenzake. Hata hapo, akiwa katika hali hiyo, yupo kwenye kikao na anatoa mchango wake kwa maendeleo ya Kilwa.

Angelikuwa mwepesi tu wa imani basi angekuwa ndani amejifungia. Mungu ambariki sana!
Mungu wangu🥺

Yesu amponye
 
Unajua ukiwa binadamu unatakiwa uwe tayari kwa lolote. Ukijua hili utaishi kwa amani. Sababu mleta mada unaweza ukafa kesho na ukamuacha Mh. Bwege na yeye 2025 akarudi Bungeni na akapelekwa nje na kupewa matibabu mazuri.
Kwa nini apelekwe nje ili apate matibabu mazuri? Mbona matibabu mazuri yapo hapa hapa Tanzania?
 
Unajua ukiwa binadamu unatakiwa uwe tayari kwa lolote. Ukijua hili utaishi kwa amani. Sababu mleta mada unaweza ukafa kesho na ukamuacha Mh. Bwege na yeye 2025 akarudi Bungeni na akapelekwa nje na kupewa matibabu mazuri.
Ni kweli kabisa, ila kama nimekosea kuleta hii mada basi niambie tu mkuu maana naona kama umekasirika hivi urafikiri labda nimemsema vibaya mheshimiwa!
 
Ukiwa na akili fupi na ndogo utajidai na kuringa sana hapa duniani lakini haya maisha si chochote wala lolote, / Tusali sana.
Kama maisha si chochote wala lolote si ufe uende huko kwenye maisha bora?

Kusali kunasaidia nini?

Huyo unayemsalia, Kwa nini akuweke kwenye dunia isiyo chochote na afanye maisha yawe si lolote?
 
Back
Top Bottom