Hujuma? Mwezi sasa wafanyakazi hawapewi mikopo yao kisa mfumo haufanyi kazi

jitombashisho

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2020
Posts
667
Reaction score
2,245
Ni takribani mwezi sasa wafanyakazi walioomba mkopo benki hawapewi pesa kwa kile kinachodaiwa ni mfumo wa mawasiliano kati ya benki na mwajiri kuwa na hitilafu.

Hoja hapa ni je, huo mfumo pia umechezewa ili kumchonganisha mama na wafanyakazi?

Na kwanini mamlaka inayohusika na mfumo huo haitoi taarifa kwa wadau?

Watu wanakopa kwa sababu maalumu hasa za kuwatibia wapendwa wao. Shime Serikali iingilie kati na kadhia hii iweze kutatuliwa.
 
Kama tatizo linajulikana POLE zao, hakuna benki itakubali kupoteza fedha huku ikitambua kuna shida katika mfumo wa marejesho.
Hakuna hujuma hapo. Hujuma itakuja bank inasema wameshatuma mkopo, wenye mkopo wasipokee ila wakute wamekatwa marejesho.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Ni takribani mwezi sasa wafanyakazi walioomba mkopo benki hawapewi pesa kwa kile kinachodaiwa ni mfumo wa mawasiliano kati ya benki na mwajiri kuwa na hitilafu.

Hoja hapa ni je, huo mfumo pia umechezewa ili kumchonganisha mama na wafanyakazi?

Na kwanini mamlaka inayohusika na mfumo huo haitoi taarifa kwa wadau?

Watu wanakopa kwa sababu maalumu hasa za kuwatibia wapendwa wao. Shime Serikali iingilie kati na kadhia hii iweze kutatuliwa.
Benki gani hiyo?Halafu hiyo post yako ni ya tarehe ngapi?Mbona imeandikwa 26 May 2021???????
 
Maelezo yako hayaeleweki lakini tayari umeshatoa lawama kwa Serikali ni Benki gani hiyo? Ili kama upo ufuatiliaji uanzie hapo
 
Back
Top Bottom