KERO Hujuma ya Huduma ya Maji Kinyerezi - Kifuru kutoka Dawasa Kinyerezi

KERO Hujuma ya Huduma ya Maji Kinyerezi - Kifuru kutoka Dawasa Kinyerezi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Salaam wakuu

Ni takribani mwezi na siku kadhaa tokea wakazi wa maneno ya Kinyerezi mpaka Kifuru na viunga vyake waone maji yakitoka katika mabomba yao ya maji ya Dawasa huku pakiwa hakuna taarifa yoyote kutoka Dawasa Kinyerezi ya kwanini huduma hiyo haipatikani

Tatizo la Maji maeneo haya limekuwa endelevu licha ya mabadiliko kadhaa ya mameneja pindi malalamiko yanapojitokeza ya ukosefu wa maji lakini haijasaidia kuondoa shida hii. Pamoja na changamoto hiyo lakini magari ya kuuza maji yamejaa na yakiuzwa bei haswa mathalani tank la 1000ltr linauzwa sh 15,000 na tena hawauzi tank moja ukihitaji wanataka uanzie 2000ltr ina maana sh 30,000. Kutokana na hali hii wananchi wengi hasa maeneo ya Kifuru kwa masista wanatumia maji ya kwenye mashimo ya choo ya wale wanaojenga nyumba ila hazijakamilika nayo kutokana na jua yamekauka hii imeleta adha kubwa sana na gharama kubwa ya maisha na kuzorotesha afya za watu kwa sababu ya kutumia maji yasiyo salama

Waliojaribu kumtafuta Meneja Dawasa Kinyerezi amekuwa akijibu yupo likizo bado hajarudi ofisini, mara ya mwisho akadai pampu iliharibika mpaka arudi ofisini ashughulikie. Sasa tunajiuliza mtu akiondoka ofisini hakaimishi kazi kwa mwingine, tutabaki bila huduma ya maji mpk lini kumsubiria?

Sisi tunaamini kuna hujuma zinafanyika pale Dawasa Kinyerezi huenda ni mradi wa watu wanaoshirikiana na wafanyakazi au ni wa wafanyakazi wenyewe wa kuuza maji kupitia magari kwa kutengeneza tatizo la ukosefu wa maji ambalo kiuhalisia halipo maana maeneo mengine kama Segerea na Kimanga maji yanaweza kutoka hata siku nne kwa wiki ila Kinyerezi hakuna maji hivyo tunaomba msaada ili kuwasaidia wakazi wa maeneo haya
 
Back
Top Bottom