Huko Afghanistan Taliban siku si nyingi watatawala Afghan yote, na kwa mara nyingine Marekani imefeli tena

Marekani akili Zake anazijua mwenyewe alikuja kuwatoa taliban madarakani, mwisho anaondoka huku akitaka serikali ya Afghanistan kujenga serikali na taliban, amepoteza pesa na maisha ya watu halafu anakimbia
 
Sisi tuliyajua hayo ila tulikuwa tunasubiri muda ufike.kama walivyokuwa wanawafadhili Mujahideen, mpaka Warusi wakaona isiwe shida wakaondoa majeshi.ikageuka Warusi na wa iran nao wakawa wanawafadhili wa Taliban mpaka Nato imeomba yaishe.

Ni swala la muda tu Taliban itachukua nchi nzima maana wamekuwa na kasi ya 5G.kila siku wanachukua maeneo,huku majeshi ya Afghanistan yakikimbia kuogopa kupambana na wa Taliban
 
ndo swali la kujiuliza, unavamiaje nchi na kuiacha katika hali mbaya kuliko ulivoivamia??
Taliban iko strong na stable kuliko hao waliowekwa na Marekani. Marekani ilikuwa inawalea wadhaifu ambao walipewa uongozi bila uzoefu wala hawana proper control. Taliban ni chama kilichoiongoza nchi miaka kibao kikiwa na jeshi na ukorofi wake huu, kukiondoa ukaweka watu wasio na maana ilimradi watakubali unachowaambia ndio kama hivi
 
Japo siipendi CHINA kwa baadhi ya mambo yao....

Ila......

Hawaingilii MATAIFA YA WATU....

Huu mwendelezo wa UKOLONI kupitia UBEPARI na kulazimishana watu waishi vile wapendavyo wengine ndio mwanzo wa YOTE HAYO.....

Hivi hao "Magaidi" Taliban ,hivi ni kwanini HAWAKWENDA kuwashambulia CHINA na KOREA KASKAZINI ?!!!!

Mchina anakataa kujishughulisha na ya watu kihovyohovyo ndio maana anazidi KUCHANUA.....

Nilitegemea uwepo wa US na NATO AFGHANISTAN kuwe kumewamaliza hao jamaa.....

Sasa 20+ years.....then mnaondoka....jamaa wako palepale tu......

Kweli MOVIES za HOLLYWOOD ni propaganda ya kutuonesha US ina maguvu zaidi ya UHALISIA WENYEWE.........

#ForNonAlignmentGovernments
 
Kama mwanzo Taleban walitawala pakawa na amani mpaka pale U.S alipokuja kuvuruga amani yao,acha watwae tena nchi yao watapata amani tu,watajuana wenyewe huko.
 
Huku dunia ya 3 tumeaminishwa kuwa Taliban ni kikundi cha magaidi, ila ukiwa Afghanistan wenye nchi yao wanaamini Taliban ni chama cha ukombozi, sasa kazi kwako uliyeko kwa Mtogole kwa Bi Nyau uamini unachoaminishwa na CCN na BBC ama uwaamini waAfghanistan wenyewe
 
kwa sasa hakuna nchi iayoweza kuvamia nchi nyigine na ukashinda, mwisho wa siku utaondoka kichwa chini tu
Wamesahau tu kuwa Somalia alishawakiza Marekani, wakaondoka uwanja wa vita wakiwa hawaamini macho yao hapo Somalia tu. Sema mabingwa wa Propaganda tu mengine uwanja wa vita ni wa kawaida sana tu. Hapo Syria Assad kawachemsha vichwa mpaka sasa na tekinolojia yao kubwa waliyonayo lkn wapi
 
Wanafadhilije? Kwanini wanaofadhiliwa wanakubali kufadhiliwa?

Hawana akili? Ni Majinga nchi nzima?
 
Kama mwanzo Taleban walitawala pakawa na amani mpaka pale U.S alipokuja kuvuruga amani yao,acha watwae tena nchi yao watapata amani tu,watajuana wenyewe huko.
sasa ndo ujiulize kama walikua na amani marekani alikua anafata nn
 
Hao Taliban wakishatwaa madaraka nao wajiandae kukumbwa na uasi kwani kwa style yao ya utawala wa mabavu sio wote watakubaliana nao.

Ili mradi tu Afghanistan haitakuwa na amani na kama watarudi kufadhili tena ugaidi hiyo itakuwa ni shubiri kwao.
hahahah.......................... wasome vizuri hao wafganistani uwaelewe. hao ni jamii ya watu wamaitwa wapashton
hao watu ni jamii ambayo mpaka marekani anavamia hawakuwa na ambukizi hata moja la ukimwi kwasababu waliridhia kutawaliwa kiislamu
hawa watu hawana technologia ya kumshinda muingereza, wala mrusi wala mmarekani laki hao wote yaliwakuta mazito, tena naona mzee baba kaiacha belgram base usiku bila hata kuaga
kiufupi hiyo ni jamii ya watu ilivamiwa na hayo mataifa kwasababu tuu hawakuwa wakitaka mfumo mwengine wa kiutawala zaidi ya utawala wa kiislamu lkn hakuna cha ugaidi wala mavi ya ugaidi na hakuna wa kuwafanya lolote as long as wanamuamini mungu na wanasimamia wanayoyaamini
 
kaka wasome hao wapashton uwaelewe kama unahisi ilikuwa rahisi hivyo muulize mrusi kabla ya mmarekani hao jamaa hawachoki bali utachoka wewe na kama ingekuwa rahisi marekani angeifanya hiyo ni alaska ya pili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…