Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Sauti ya umma imekita kambi huko Nairobi, Kenya! Hali imekuwa tete sana! Waandamanaji wamechoma moto ofisi ya gavana wa Nairobi na kuvamia bunge, bendera zote zimetelemshwa na mgahawa wa bunge umevunjwa, waandamanaji wameonekana wakila chakula na kutapanya kila kitu!
Jengo la Seneti limevunjwa na waandamanaji wameingia ndani ya bunge! Huku mamia wakilanda landa juu ya meza ya spika na kuharibu kila kitu! Yawezekana huu ukawa ndio ushindi wa kwanza wa waandamanaji kuwahi kufanyika Afrika Mashariki!
Utawala wa Ruto upo shakani na watabiri wa mambo ya siasa wanaona kuwa huu unaweza kuwa ndio mwisho wa utawala wa Ruto! Ajabu ni kuwa baadhi ya askari waliovalia mavazi ya jeshi wameonekana wakiwapatia maji ya kunywa baadhi ya waandamanaji jijini Nairobi na kuwapa nguvu ya kusonga mbele! Hii ni ajabu na hata walipoanza kuvunja mageti ya jengo la Seneti hakuna askari aliyejaribu kuwazuia!
Tuiogope sana dharau kwa tunaowaongoza. Kuna wakati binadamu huchoka pamoja na baadhi ya waandamanaji kupoteza maisha kwa kupigwa risasi na mabomu lakini bado raia wanasonga mbele.
PIA SOMA
- LIVE - Yanayojiri Maandamano Kenya: Waandamanaji wafika Bungeni, wawili wauawa kwa risasi