Huko Kitchen Party huwa mnafundishwa/wanafundishwa nini?

Huko Kitchen Party huwa mnafundishwa/wanafundishwa nini?

Calnde

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2008
Posts
1,373
Reaction score
278
Naomba kufahamu dada zetu huko kitchen party huwa mnafundishwa nini?

Maana nilisikia huwa mnafundishwa maadili. Namna ya kumtunza mumeo na watoto wako.

Mapishi ya vyakula vizuri kwa mumeo na watoto. Usafi. Namna ya kumridhisha mumeo kimapenzi

nk nk. . . Mbona bado matokeo hayaonekani baada ya hayo? Si nasikia huwa mnafundishwa jinsi ya

kuwadhibiti waume wasitoke nje? Mbona bado wanatoka? Mbona kupika kwa ninyi wakisasa

ambao ndo mnaenda sana huko bado issue? Mbona malezi ndo yanaporomoka? Maadili je? Mbona

wanaume wanalalamika hawafiki? Hivi huwa wanafundishwa nini? bado upo umuhimu??

Mhhhh!

Kitchen party ya siku moja hata shule inamihura kibao mpaka ufuzu.
 
kaka yangu usipate shida, tatizo ni kwamba haya yanafanywa kwa upande mmoja tu wa ke ilihali me tunaassume kuwa anajua majukum yake. kumbe ni makosa makubwa. mama peke yake hawez akafanya kila kitu bila kusaidiwa na baba na ndio maana kwangu kitchen paty naichukulia kama sherehe ya kupewa vyombo tu lakin siyo mafunzo
 
malezi yanaanzi mbali sana toka nyumbani ulikozaliwa na kulelewa. kama kwao mdada hajawah kumuona mama akiwa jikoni anapika au anambembeleza baba unategemea atakuja kuambiwa kama ngonjera aelewe?pale huwa hatuendi mna msufuria wala miko na moto ili apike wala hatuendi na watoto li akaone malezi haya alipaswa ajifunze kwao wakati anakua na mengine ajifunze mwenyewe kwenye maisha hata kw akusoma vitabu
 
ninyi wakaka je tabia zenu mnajifunzia wapi?
 
"Urembo unawazidi nguvu wasichana na mashairi hadimu zaidi ya birika uswahilini follow me"--Joh Makin

Tupigeni magoti tusali.
 
Kumbe hiyo ya siku moja contents zake zinakuwa nini sasa?

Sifagilii hayo makitchen wanayo fanyiwa but huwezi ukamlisha ng`ombe kwa siku moja utegemee ataongezeka ktk kilo zake za nyama.

Nakama gfsonwin alivyonena it has to be two way traffic
 
kaka yangu usipate shida, tatizo ni kwamba haya yanafanywa kwa upande mmoja tu wa ke ilihali me tunaassume kuwa anajua majukum yake. kumbe ni makosa makubwa. mama peke yake hawez akafanya kila kitu bila kusaidiwa na baba na ndio maana kwangu kitchen paty naichukulia kama sherehe ya kupewa vyombo tu lakin siyo mafunzo

Hivyo na mwanaume nae aende Kitchen Party siyo?
 
Ndiyo kusema huyu superstar wenu Ruru sijui Ulu , silikumbuki vizuri jina lake,
angekua amefundwa huko vichen pati , asingemfanya vile Kanumba ?
 
malezi yanaanzi mbali sana toka nyumbani ulikozaliwa na kulelewa. kama kwao mdada hajawah kumuona mama akiwa jikoni anapika au anambembeleza baba unategemea atakuja kuambiwa kama ngonjera aelewe?pale huwa hatuendi mna msufuria wala miko na moto ili apike wala hatuendi na watoto li akaone malezi haya alipaswa ajifunze kwao wakati anakua na mengine ajifunze mwenyewe kwenye maisha hata kw akusoma vitabu

Hapo sasa. Kama hayo yote hayafanyiki lipi huwa linafanyika?
 
Mie naona zogo tu hiyo Kitchen Party,huyo anae kufunda ameshaachwa mara kibao au wengine hata ndoa hawana sasa anamfundisha nini mwenzie? mafunzo yanaanzia nyumbani kuanzia usafi kumjali mtu na mengineyo,pale unachoambiwa unawachia wenyewe na kikubwa kuchukua vyombo vyako ulivyo wapa wenzio..si mind ukienda unyagoni mara 100 unaweza kuambulia japo matatu yakakusaidia.
 
8L3BKOwJSawd4AAAAASUVORK5CYII=
 
Kitchen party ni kama Women's Day, siku moja kati ya 365 inasaidia nini? Hakuna kitu.

Ni kuwaacha wajione wanapewa wanachotaka wakati kiukweli sidhani kama inasaidia chochote.

Labda ile kujikusanya na kufurahi pamoja.
 
kitchen pat ni sherehe ya kukusanya vyombo. nlickia wadada wa zaman walikuwa wanatawa kabla ya kuolewa. ktk kutawa hukaa kwa muda flan ndan bila kutoka hapo ndan ndo anapewa k-pat ya nguvu anafundwa anafundika. bt nw day wadada wanapga misele had cku yenyewe ya haruc unamkuta bdo yupo mtaan akitoka hpo ndo aenda kufunga ndoa. ndo mambo ya utandawaz yana faida na hasara pia. tushasahau km kuna kitu kutawa kwa bi haruc mtarajiwa cku hz!
 
Back
Top Bottom