Somalia na Ethropua hakuna rasilamali Zinazovuma hapa Afrika hivyo hawana cha kupoteza hivyo vijana wa kitanzania kuiga kijana msomali/muhabeshi ni kujipotezea muda.
Tanzania kuna migodi bubu mingi sana ya kujichimbia tu na kutoka maisha tena bika kodi.
Tanzania kuna maziwa makubwa 3 yanayotoa samaki muda wote ie Tanganyika Viktoria na Rukwa.
Tanzania ina mabonde oevu ya kulima mwaka mzima ambayo ni Rufiji,Kilombero, Ruaha/Usangu, Nyasa kagera, Kilimanjaro,Malagarasi nk
Tanzania kuna ardhi yenye rutuba isiohitaji mbolea mikoa ya Kagera,Kigoma,Songea,Mbeya,Tanga,Morogoro, Pwani, Lindi mtwara Njombe,Iringa Katavi ,Rukwa,Songwe, Kilimanjaro nk Jichagulie mkoa wa kwenda ukaanzishe kilimo.
Tanzania kuna mbuga za wanyama za kutosha.
Tanzania ina mipaka ya kutosha ya kukuwezesha kufanya biashara na nchi jirani.
Tanzania ina Amani tele na watu wakarimu wenye upendo kila mkoa.
Halafu umuige msomali kutapatapa kwenye maroli huku ukiacha rasilimali za kutosha kukufanya uwe tajiri .
Rejea shairi linaitwa Fikiri:
"Fikiri mimi jamani nakufa hapa kwa nini, chakula kingi nyumba, ..nyumbani ashiba..." .
Ulaya kuna rasolimsli gani za kumtajirisha mkimbizi kutoka Afrika, je waweza nitajia watu maarufu waliotajirika kwa kuwa wakimbizi huko ulaya .