Huko Zimbabwe kuna kijana amegundua gari lisilotumia umeme, mafuta au nishati yoyote kutoka nje. Inawezekana vipi?

Nchi yangu inadharau sana wataalamu wake na kuamini kila kitu kizuri lazima kiletwe na ngozi nyeupe,vinginevyo hakifai
Mfano yule mzee wa kipare aliyeunda mtambo wake wa kuzalisha umeme usio wa maji,upepo,jua wala mafuta ,tanesco wamechangia kumpoteza kabisa huyu mpare wakati ambao angekua msaada mkubwa sana kwa taifa
 
Hana maisha marefu. Hakuna tofauti na wale wanaofanya ugunduzi wa engine za gari zinazotumia maji pekee bila nishati nyingine. Lazima wapotee
 
Kuna yule Dogo alokuja na Mfumo wa kupiga kura Kwa mtandao.


Sijui hata yuko wapi
 
Kweli kabisa Mzee hasikiki tena
 
Tatizo sio kuuza Magari, tatizo ni Teknolojia yake ambayo haipatikan popote pale Duniani na Wazungu mpaka sasa wameshindwa kupata jibu inakuaje , inakuaje MTU atengeneze energy from unknown source??.
Na bado hawajashangaa,burkina faso nae anaingia kwenye soko la magari ya umeme
Biashara ya magari africa sasa watuachie waafrika wenyewe
 
Hata yeye hajaumba wala kuiharibu Energy. Amebadilisha matumizi, sawa na sola. Mwanga wa JUA unazalisha umeme. Na yeye katumia iliyoko kwenye energy ya mawimbi ya redio kuendesha gari. Ujanja ni namna ya kuyabadili hiyo nguvu ndani ya mawimbi iweze kusukuma mitambo ikiwapo magari na hata baadae viwanda,. Je unajua giza ni mojawapo ya energy? Itafika muda vyombo vya utafiti vitatumia nguvu hiyo kupeleka wanaanga huko pamoja na utafiti anga za mbali. Hata hizo mawimbi ya radio yatafikisha wanadamu mbali maana YAPO KILA MAHALI.
 
Mkuu TESLA, Wachina na Ulaya ni kweli wameshtushwa Sana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…