Nimejaribu sana kutafakari huu ujinga utaisha lini, lakini sioni hata dalili yaani!!
Katika jamii yetu hasa afrika Tanzania hatupendi kabisa kukubali ukweli!
Inatakiwa tuanze kuwafundisha watoto shuleni ili watambue hill!
Kwasababu hata watoto wenyewe mwenzao akifaulu sana utasikia yule ALIDESA au yule Mjomba wake ni Mwalimu! Yaani ilimradi tu kujitetea!
KAMA HII HAITOSHI HATA KWENYE MISIBA UTASIKIA!
1. Mtu mashuhuri akifariki kijijini utasikia huyu lazima karogwa yule mzee flani pale mchawi kama ni nini
2. Mtu akifariki kijijini utasikia, nilijua tu maana Jana bundi na mbwa wamelia sana
3. Mama mjamzito afrika anaingia leba kujifungua na hofu ile ile ya mtaani kuwa tumbo lake linawindwa na wachawi.
4. Akifariki Mwanasiasa Hata kwa Corona, Hatusemi ni Korona ili tuelekeze nguvu kupambana na korona, lazima turembeshe na maneno mengine sijui inatusaidia nini kitaifa.
5. Akifariki kiongozi lazima tuwaze kuwa kalishwa sumu! Hatujui kabisa kuona kifo kama kipo.
Ni kibaka pekee ndiye anaetajwa kuwa kafa kwa ukibaka wake lakini wengine tunafumba fumba!
Siku moja nilikuwa namtania Mkuu wa usalama barabaranj nikamuuliza, Hivi kwanini Mnapotangaza ajali za magari ya jeshi na ya viongozi Hamsemi wazi kuwa CHANZO CHA AJALI ilikuwa mwendokasi, au Wrong side drive! ( Kwanini huwa mnasema gari lilimshinda nguvu?)
Lakini ajali za RAIA huwa mnasema ni mwendokasi? Pia nikamwambia hivi kwa nini huwa hamtaji UBOVU wa barabara kuwa ni sehemu ya chanzo ili mamlaka itatue?
Inakuwaje mtu ajikwae kisiki kilekile halafu usitaje kisiki kuwa ni sehemu ya tatizo? (Alinijibu Hayo ni mambo ya ndani sana).
Hivyo ujinga ni mwingi sana ndiyo maana hatufanikiwi!
Mambo ya UONGO UONGO na kufumba fumba hivi yanachangia hadi viongozi wetu wafanye mabaya bila hofu kwasababu wanahisi maisha yetu HAYAWAHUSU WAO!
Laiti Aliyekuwa mwenyekiti wa bunge la katiba angewaza kuwa kuna kifo angefanya vyema ili katiba mpya ifae kwa wote!
Laiti waliowahi kuwa marais wangewaza kuna kifo wangeruhusu katiba na maendeleo kwa usawa!
Lakini kwasababu za kijinga Viongozi hawajui wamebeba dhamana ya maisha ya watu, wanafanya wanayotaka wao na si wanayotaka watu!
Watu wanakwambia tunataka katiba mpya, kiongozi unasema siyo kipaumbele huu ni ubinafsi ambao Mungu hapendi!
Hivi hata ujasili wa viongozi kutamka mnampenda Mungu mnapata wapi kama binadamu wenzenu wanaoonekana kwa macho wakitaabika hamuwapendi?
Ujinga ni mwingi sana afrika

- Mwenzetu akifanikiwa kipesa (hatukubali moja kwa moja), Kauli zetu nyingi midomoni utasikia " Yule jamaa kama siyo Freemasonry basi kapata mganga mzuri,
- Mwenzetu akifanikiwa; tunasema yule jamaa anapiga sana kwenye kitengo chake kawa fisadi!
- Akifanikiwa , utasikia huyu atakuwa kauza shamba (Mali za urithi)
- Akifanikiwa mwanamke; utasikia huyu kapata danga lenye mihera analichuna!