Huku akiwa ameshafungashiwa virago, Bodi ya Ligi Kuu yamfungia Gamondi michezo 3 na kumpiga faini

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Novemba 14, 2024 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatayo;

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Young Africans, Miguel Gamondi amefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh. 2,000,000 kwa kosa la kumsukuma na kumuangusha chini Kocha wa viungo wa Klabu ya Singida Black Stars, Sliman Marloene, baada ya mabishano yaliyotokea wakati timu hizo zikienda mapumziko katika mchezo wao kwenye uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Aidha, Klabu ya Singida Black Stars imetozwa faini ya Sh. 2,000,000 (milioni mbili) kwa kosa la kuingilia mazoezi ya klabu ya Young Africans siku moja kabla ya terehe ya mchezo

Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa New Amaan Complex huko Zanzibar, Yanga iliibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Singida Black Stars

Pia soma: Breaking News: - Rasmi: Yanga yavunja Mkataba na Gamondi
 
Wanafiki tuu hao bodi ya ligi.
Wangekuwa na weledi kwa tukio lile la Zanzibar huyo mhuni hakutakiwa kusimama tokea mchezo uliopita dhidi ya Tabora. Lakini Mungu alivyofundi, huo huo Mchezo ndio umepigilia msumari wa mkataba wake.
 
Wameona ameondoka ndio wanakuja tukio la muda sana wanafki tu
 
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Novemba 14, 2024 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya maamuzi yafuatayo;

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Young Africans, Miguel Gamondi amefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh. 2,000,000 kwa kosa la kumsukuma na kumuangusha chini Kocha wa viungo wa Klabu ya Singida Black Stars, Sliman Marloene, baada ya mabishano yaliyotokea wakati timu hizo zikienda mapumziko katika mchezo wao kwenye uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Aidha, Klabu ya Singida Black Stars imetozwa faini ya Sh. 2,000,000 (milioni mbili) kwa kosa la kuingilia mazoezi ya klabu ya Young Africans siku moja kabla ya terehe ya mchezo

Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa New Amaan Complex huko Zanzibar, Yanga iliibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Singida Black Stars

Pia soma: Breaking News: - Rasmi: Yanga yavunja Mkataba na Gamondi
Mwaka wa taabu

Back
Top Bottom