Huku barabarani truck za Scania zimekuwa adimu sana, ni mchina tu kila mahali

Huku barabarani truck za Scania zimekuwa adimu sana, ni mchina tu kila mahali

Scania moja tena used ina bei kubwa Sana sidhani kama kuna mfanyabiashara anaweza kununua Scania na akaacha mchina

Pia kwenye fuel consumption Kwa malori ya kichina ni rafiki Sana tofauti na scania
Gari za Mchina ni rahisi kukopa kupitia bank zetu ndio maana unaona zipo nyingi road ila Scania ni mwisho wa matatizo kwa sifa zote changamoto iliyopo zimeongezwa kodi mwaka huu kama mbinu ya kufifisha biashara ya Scania na watu wakimbilie Mchina naona wamefauru kwa kiwango fulani.
 
Mchina katutoa kimasomaso wamiliki wa coaster. Kupitia mikopo nmb nimenunua yutong 2
 
Hao mchina bei elekezi ni 136m, ukiwa na 25% of that price + gharama ya bima na GPS, benki wanakukopesha, same to yutong buses/zhongtong climber buses and the like. Hata scania inawezekana kwa mfumo huo ila matajiri wengi wanakwepa kwasababu ya gharama kubwa wakati wanajua horse moja ya scani unapata horse 2 za mchina....

Thanks to financial institutions.
 
Business dynamics ndo zina dictate soko.
Banks hazifinance kirahisi gari ya mzungu, daf Volvo Scania etc. Kwa sababu zikiwa mpya unit cost ni ghali, zikiwa mtumba zinakuwa sio reliable.
Gari za kichina zinakuja zero km, banks zinaona ni sahihi kuweka pesa huko
 
Hii boom ya magari ya Kichina sasa, itakuja kuleta burst huko mbele ya safari.
Banks wao wanajali faida zao tu, watu wanpodefault kwenye mikopo anayenufaika ni banks pekee.
Hiiikopo. Ya magari imesababisha watu wengi kufanya biashara moja kwa kutumia tools aina moja, na kugombea soko moja. Matokeo yake biashara inakuwa ngumu kwa kila mmoja
 
Sasa hapa si ndio tunapata ushindani mzee, hakuna pesa ya bure. Maeneo mengi hayajafikiwa na usafiri unaweza peleka huko gari au ongeza ubunifu ule mema, lakini pia soko bado ni kubwa sana abiria na mizigo kila siku inaongezeka as long as nchi imefunguka na watu wana import na export bidhaa/mizigo.
 
Business dynamics ndo zina dictate soko.
Banks hazifinance kirahisi gari ya mzungu, daf Volvo Scania etc. Kwa sababu zikiwa mpya unit cost ni ghali, zikiwa mtumba zinakuwa sio reliable.
Gari za kichina zinakuja zero km, banks zinaona ni sahihi kuweka pesa huko
Connection tu mkuu watu wanakopeshwa na gari za SA used hata hizi Land cruiser ila ni wachache wenye hiyo miguu..
 
Gari ya mzungu bei ya kununua ipo juu. Kwa Tanzania at least Scania hata transporter wanaingia kuchukua mpya. Volvo kuna kipindi mpaka dealer walifunga ofisi, saizi wamerudi tena na wana wateja wao. Mercedes Benz trucks kwa brand new wateja wake ni walewale kampuni kubwa.

Mchina kaweka unafuu wa kupata gari jwa cash na ukiwa na kianzio benki zinakupa mkopo.
 
Gari used za ulaya bado zinakuja kwa wingi kuna watu wabishi wanakomaa na Daf,Man,Renault,Benz,Iveco,Scania. Kuna transporter fleet zao ni Daf,Scania na Man Used na wanazileta tu.
Ukipiga hesabu za kibiashara kwa uhalisia wake vzr huwezi miliki fleets za Gari ya kichina .
Hii boom tunayoshuhidia ni sababu banks zina finance kirahisi na kufanya watu wengi kuwa attracted , na wengi wao hawana abcd za trucking bussines,
Mosi gari ya Kichina sio ya bei rahisi, , unaongelea dola 55000 horse tupu na hii ni very basic faw
pili haina maisha marefu, kupata km laki 3kwa gari ya Kichina ni majaaliwa ya Mola
Tatu sio comfortable na ni risk kwa afya ya dereva, kuendesha a fully loaded truck kwa km 500 sio rahisi na wengi wanaokaa wanaishia hospitali kutibu uti wa mgongo.
Ndo maana wengi wanaomiliki gari za Kichina inabidi wafanye kazi na vijana wadogo ambao hawajui madhara ya kiafya
 
Back
Top Bottom