Huku kwenye maofisi ya Serikali huduma ni mbovu mno na watumishi wamerelax sana. Hivi shida ni nini?

Tunajua unachokusudia kusema lakini hakuna wakati wowote kulikuwa huduma nzuri huko maofisini.
Hivyo turidhike na hii hali sio...? TUMEPOTEA NDUGU ZANGU....
sema ukweli upunguze dhahama hata kwa ndugu zako.....nchi moja huduma tofauti daah ..
 
kazini sio sehemu ya excuses. kama huwezi kufanya kazi na una msongo wa mawazo omba leave uji-sort out. hizi sababu kuna siku nurse atamchomeka vibaya catherter mgonjwa anaekuhusu vibaya atatumia sababu hizi hizi unazotoa
Na ukiona yupo hivyo mtafute wa kukufanyia utakalo.Watumishi si sehemu ya kujitafutia umaarufu.Nenda kwingine.
 
Hicho unafikiri wala hakipo hivyo..siku ukija pokea huduma nje ya maeneo uliyoyazoea/kukulia kuna kitu utajifunza kitu na utafanya ulinganisho...TEMBEA NDUGU TEMBEA...tena kwa wewe mtoa huduma tembea maofini ya wenzenu wasiofanya kazi kama wamelazimishwa...Tembea hata hapa ndani ya nchi utajifunza kitu...
 
Dah mbuzi mee nimekuelewa japo hujapenda kushare expirience yako
 
Umemuongelea dada mmoja hivi mweupe kibonge yupo pale NIDA Iringa. Saa nane na nusu tu anaondoka ofisini.
 
Tusha ingia mfumoni tuvumilie hadi pakuche
Inasikitisha sana kwa vitu vingine havihitaji rasilimali fedha ila navyo bado tunashindwa kusimamia.......

Hivi ni kweli viongozi wa haya maofisi wanashindwa panga mpango kazi wa mzuri na kuusimamia vizuri kulingana na mazingira yao?

Ofisi inakosa ubunifu kabisaa wa kuhudumia wateja wao bila kutoka nje ya malengo ya kitaifa/kiwizara?

Hivi mnajua hata police ambapo wengi wetu tunapachukia panaweza toa huduma nzuri na ikawaridhisha wote washtaki na washtakiwa ...!!

Tuanapotea ndugu zangu..tunapotea...
Kuhudumia watu vibaya au visivyo au kupuuza hapamkomoi Rais au Bosi wako ila kunaumiza wananchi wasio na Hatia ..

Sasa hivi kuna baadhi ya maofisi ya serikali zile zinazohusisha malipo control number hawakupi ila wanaviduka vyao vya wakala wa pesa...uwarushie wao fedha na wao ndio wafanye malipo...nenda hospital ya Milembe Dodoma ukaone hicho kitu
 
anakukata na vat😂
 
Mimi mwaka Jana mwishoni nilienda ofisi ya NHIF pale Posta wale vijana walinipa huduma nzuri hadi nikashangaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…