Huku Kwetu Kuko hivi, Vipi Huko Kwenu?

Unashinda unalala na kuangalia tv, hela zije nyumbani kwako?
 
Naongelea matukio ya ujambazi
 
VP kuteka watu kwa wale waliopewa jina la ubatizo wasiojulikana?
 
hiyo ni kutokana na serikali imara ya ccm cha kufanya ni tarehe 28 kuichagua tena ili vilivyobaki viishe kabisa
 
kama kuna kitu kimeongzeka basi hako vilevile au hujaelewa swali?
 
Money is the source of all evils, when there is no money all the listed evils are not there or are greatly reduced. Hayo yote tunashuhudia kwisha au kupungua kwa sababu mzunguko wa fedha mitaani umepotea kwa sababu tunazoelewa sote. Mfano, jambazi haendi kuiba nyumba fulani kwa kubahatisha bali anakuwa ana hakika ya kupata chochote huku akijua anaweza kukamatwa kabla ya kutekeleza azma yake na nini kitampata akikamatwa. Mabasi na bodaboda wanapata ajali wakati wanafukuzana kuwahi abiria ambao sasa hawasafiri sana kwa sababu ya ukata. Rushwa mtu anatoa sehemu ya pesa zake kununua huduma ambayo hutolewa bure au kwa gharama ndogo ili akamilishe mambo yake mapema kabla pesa aliyonayo haijatumika yote kwa shughuli nyingine zinazoweza kujitokeza. Vyombo vya dola vinajigamba kuwa vimethibiti uhalifu au matukio mabaya kutokana na juhudi za watendaji wao, siyo kweli, ukweli ni kuwa watu hawana pesa ya kunyang'anyana. Aliyonayo anachunga kwa nguvu zote isichukuliwe na asiyenayo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…