Huku raia wakipigwa na Israel Mahmoud Abbas apiga picha na Blinken.Habari zilipovuja Blinken akakimbizwa mbio

Huku raia wakipigwa na Israel Mahmoud Abbas apiga picha na Blinken.Habari zilipovuja Blinken akakimbizwa mbio

Shambulio la Hamas la oktoba 7 ilikuwa ni sababu na kisingizio cha Israel kutekeleza ajenda zake za muda mrefu nazo ni kuifuta kabisa Palestina.
Ukweli huo unaonekana katika kuongezeka kwa mashambulizi ya jeshi la IDF na walowezi kwa kila raia wa Palestina maeneo aliko Mahmoud Abbas wa PLO.
Katika hali kama hizo viongozi wa Marekani wamekuwa wakipita huku na huko wakiwatuliza viongozi wa nchi za kiarabu na kuipa nafasi Israel kuendelea kupiga kila kitu kuanzia watu hadi mapipa ya maji.
Jana waziri wa nchi wa Marekani alikuwa na mazungumzo na viongozi wa baadhi ya nchi za kiarabu ambapo kwa mara nyengine na bila kumung''unya maneno aliweka wazi uungaji mkono wa taifa lake kwa Israel katika vita vilivyoanza kama kuwatafuta na kuwafuta Hamas.
Viongozi hao wa kiarabu kwa upande wao walitoa matamko ya kiakili japo hayana mashiko ya kivitendo.
Baada ya kuweka wazi kuunga mkono vita Blinken aliwataka viongozi hao kujadili nini kitakachofuata baada ya Hamas kushindwa na vita kuisha.Katika mapendekezo yake alisema anataka eneo hilo likabidhiwe vikosi vya kimataifa kama njia ya mpito kuelekea serikali ya Palestina.
Naibu waziri mkuu wa Jordan,ambako mkutano huo ulifanyika akamwambia hakuna haja ya kujadili suala la mbele wakati la muhimu kwanza ni kusitishwa kwa vita na kuokoa maisha ya watu.
Bila haya kiongozi huyo wa Marekani leo alikwenda maeneo ya Jeruisalem kwa kificho kukutana na Mahmoud ili kumshawishi kuunga mkono kupigwa kwa Hamas kutakapopelekea kukabidhiwa eneo la Gaza na serikali ya Palestina.
Pamoja na ushawishi wa kimadaraka,Blinken pia alimshawishi Mahmouud Abbas kwa pesa akimwambie zile pesa za kodi za wapalestina zilizozuiwa na Israel karibuni atapewa yeye katika serikali yake.
Habari za kikao cha Mahmoud Abbas na Blinken zilipovuja hali ilikuwa tete na haikuwezekana kukamilika kwa kikao hicho katika namna ya kufanya majumuisho mbele ya waandishi wa habari.
Kilichotokea ni kukimbizwa Blinken chini ya ulinzi mkali akiwa ndani ya vifaru na magari ya jeshi ili kumlinda na vurugu ambalo lingetokea na kuziba njia.Hata hivyo picha za mwanzo za mazungumzo hayo zilipatikana kuthibitisha kuwa kweli alifika ofisi za Mahmoud Abbas kwa kificho.

View attachment 2804896
na hao jamaa ni matajiri na watoto wao hawakai Gaza wala westbank. kama yule Ismail Haniye unaambiwa utajiri wake ni kama Bilioni za kitanzania 5.
 
Back
Top Bottom