Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Kha! Kwaheri.
 
Kwa hyo nyie huko ndo mpo sahihi si ndio
Katika kuhifadhi mila, desturi na tamaduni zetu. Ndio. Na ndio maana wewe kwa mujibu wa desturi zenu, mila na tamaduni zenu mnaona sio sawa.
 
Wacha nikusaidie

Maneno yenye asili ya kiarabu nimeweka RED

Maneno yenye asili ya English nimeweka BLUE

*Kuna vitu viwili unachanganya! Africa kama Africa ni jina la kupewa ni sawa na Victoria, hayo ni majina tu ya kupewa na watu waliokuja kama Explorer, lakini tunapoongelea lugha ni kitu ambacho kimetokana na mchanganyiko wa misamiati, hivi unafeli wapi? Weka kitu chochote kwa jina la kiswahili tuangalie na makabila ya kibantu wanakitambua kwa jina gani, ili tuone je jina la kitu hicho litashabihiana na lugha nyingi za kibantu au hazitoshabihiana basi. *


Hayo pekee ndio maneno yasiyo ya Kibantu kwenye hicho kikundi cha maneno, hayafiki hata 20 %

Muarabu asiejua kiswahili kabisa hawezi hata kuelewa chochote hapo, sa iweje mseme kiswahili ni kiarabu?
 
Sijui mwenzangu unaongea Kiswahili gani..au uko upande gani wa Afrika Mashariki

lakini ukweli ni huo, Mwarabu akiongea Kama unaongea Kiswahili ni rahisi kukamata baadhi ya maneno

Tafauta neno lolote halafu niandike, halafu lifanyie uchunguzi,utakuta maneno mengi ni ya Kiarabu..

Kama umeshindwa liweke hapa..Mimi naanza na maneno hata

Mubashara
Habari
Ridhaa
Shukurani.
 
Katika maneno yote ya kiswahili, maneno yaliyokopwa kutoka kiarabu hayafiki 10%
 
Ningefurahi kama Ningekua najadiliana na mzaliwa originally wa Zanzibar mwenye nchi, ninyi walowezi mna makandokando sana
Hahaha,kwani Mzanzibari original anaonekanaje?

Zanzibar ni Cosmopolitan state, Watu wamechngaanya damu na makabila ya Afrika na nje ya Afrika

Mimi naweza kuwa mweusi mwenye muonekano wa Mwafrika lakini mdogo wangu Baba mmoja mama mmoja akawa na muonekano wa Kiarabu

Nyinyi Watu wa bara hamjazoea haya,na ndio maana Wazanzibari wanakupasueni kichwa
 
Hahahaha ni sawa na kusema United States ni ya wazungu na weusi wakati ni ya redindians ndio wenye nchi

Muarabu, Muhindi, Mreno, Mzungu, Mjerumani wote wameikuta Zanzibar ipo na wenyeji, ninyi kwenu mlikotoka mnakujua
 
Hahahaha ni sawa na kusema United States ni ya wazungu na weusi wakati ni ya redindians ndio wenye nchi

Muarabu, Muhindi, Mreno, Mzungu, Mjerumani wote wameikuta Zanzibar ipo na wenyeji, ninyi kwenu mlikotoka mnakujua
Kweli, huo ndio mfano hasa wa Zanzibar,wenyeji wa kwanza Zanzibar walikuwa Wadigo, Wazaramo,Wazigua,Wasegeju..

Hao walizaana na Wahindi,Warabu,Wairani,Wachina,kizazi Chao ndio Wazanzibari wa sasa..

Zanzibar hakuna makabila,Kuna Wazanzibari

Makabila yamefutika zaidi ya miaka 500 iliyopita,ukisikia Mzanzibari anajinasibu kwa kabila Lake basi ujue mgeni huyo
 
Hakuna muafrica asie na kabila dunia hii, kabla haijaitwa zanzibar ilikua inaitwa unguja na nyingine pemba ikiwa na watumbatu na wahadimu ambao walikua na Mila zao na desturi kama waafrika wengine, kumezwa sana na utamaduni mpya kutoka nje na kumomonyoa asili yao hakuwafanyi kwamba ndio hawakuwa na asili.
 
1. Nahisi hujitambui.
2. Si kila mtu mwenye kuacess jamiiforums anatumia browser na ndio maana sisi tunaotumia App hatuna uwezo wa kuona rangi. Huniambii kitu kuhusu Kiarabu nakijua kukisoma na kukiandika pia. Muda mwingine huwa naepuka malumbano yasiyo na tija.
 
Hao Watumbatu na Wahadimu unawajua? Unaweza kuonesha walipo ndani ya Zanzibar kwasasa? Lakini mbona wadigo wapo na mpaka sehemu walipo inajulikana? Usilolijua uliza kwa wenyeji.
 
Sisi tunaongelea ndizi kumbe we unaongelea utumbo, mwalimu wako kipofu! Tatizo mnapenda kuamini sana kwa kitu ambacho ni cha kutengeneza. Hata mimi naweza kuandaa taarifa yangu na kuilisha kwenye wikipedia. Tatizo mnaamini sana Wikipedia bila kujua hata huyo alieandaa hiyo taarifa na kuiweka humo ni binaadamu kama wewe!
 

Amekikuta ndio, ndio akalazimisha Watanzania wote wajifunze kiswahili, by then Tanganyika walikuwa wanaongea lugha za makabila yao. Kama unesoma kwenye historia ya kugha kiswahili kimeanzia katika mwambao wa afrika mashariki
 
Ally wanaita arii

Ally ni jina la kiarabu kinalopatika kwenye Qur an, Jina la Swahaba Ally. Sisi hatuchanganyi ‘L’ na R mkuu hata kwa bahati mbaya. Hakuna mzanzibar hata mmoja Ally anatamka Ariii. Labda mzanzibara huyo.
 

kdg hali imebadilika mana mchanganyiko umekuwa mkubwa sana na hilo ndio lengo kupunguza au kuondoa kabisa maadil ya kizanzibar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…