Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

hapo zenji ni sehemu za mjini na pwani kwenye hotel za watalii ndio wa bara utawakuta tofauti na hapo ni mbara mmoja kwa wazanzibar mia kwenye mtaa...
 
acha kuikashfu bangi tafadhali
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ila wanaubaguzi hawa watu usiombe wewe wa bara ukafanya kazi zenji yani hatar ndugu yangu alihama usiku wa manane kakimbia kazi mwenyewe
Sheikh Unfair usituseme vibaya hivyo, around the world kuna ubaguzi hata huko bara ubaguzi upo baina y kabila hili linajithamini lengine linadharauliwa, kweli sio kweli?
 
Kumbe umeajiriwa huna unalojua.

Siku moja miliki biashara au fungua kampuni ndio utajua ninayokwambia.

Halafu ukanda wa hoteli kote huko hauna connection na wanzanzibar kwa kiasi kikubwa.

Kama unataka kujua tabia za wazenji jichanganye kwenye Jamii zao.


Mimi nimewahi kuwa na mradi huko na sio kuajiriwa, sharti la kwanza mtu wa front lazima awe mzanZibar mwenzao. Kinyume na hapo hufui dafu.

Usijifanye umeishi Sana Zanzibar kushinda wengine.


Nimekaa sana Unguja mazizini.

Hotel zote za Upande wa Michamvini hakuna nisiyoijua. Ninaongea ninachokijua sio kusimuliwa.


Mtu kuhamishia familia Zanzibar ndio unakuja kutuambia wazanzibar hawana hizo tabia.
 
Sheikh Unfair usituseme vibaya hivyo, around the world kuna ubaguzi hata huko bara ubaguzi upo baina y kabila hili linajithamini lengine linadharauliwa, kweli sio kweli?
Bara hatuna Ubaguzi wa kijinga Kama Zanzibar.

Kule Pemba ukifungua Duka Kama ni mbara watu hawanunui vitu kwako.

Huku bara mtu unaweza kutoka songea ukaenda Mwanza na ukafanya biashara vizuri bila kunyoshewa vidole.

Kwanza mna wivu ile mbaya kwa wabara eti wanawamalizia fursa zenu wakati mmejaa uvivu. Mtoto wa kiume wa Zanzibar hawezi kuchimba choo au kuchimba mtaro wa maji machafu. Kazi zinafanywa na wabara ( mnaita wanyamwezi ) halafu mnaanza kulia lia.
 
Mmhhhhh.
Mradi na wewe umeandika!!!!

Zanzibar yenye mchanganyiko wa makabila kibaooo unasema hakuna warembo!!!?

Zanzibar ipi uloenda wewe? Au kwa vile wanavaa mavazi ya kuiljistiri ndio sababu?
Unguja Hakuna wanawake bana usilete ubishi wako. Hiyo Unguja kwa watoto visu haifikii hata Manyara.


Najua unabisha ila ukweli utakuwa unaujua.

Kama unabisha nenda pale Ofisi ya Boti za Azam au ZanFeries uone watoto wa kiunguja halafu linganisha na wa huku bara.
 
Kuna binadamu hapo juu anabisha utadhani ndiye mmiliki wa kisiwa cha unguja.

Kiukweli Unguja hakuna wasichana wazuri, maybe ukitaka wanawake wazuri utege kwenye vyuo, mathalani kule ZU tena unakuta siyo Mzanzibari ila katokea comoro kaja kusoma tu hapo, wengine ni mabinti zetu toka tabora hama Shinyanga hao ndiyo mashallah!.
 
Ukitaka kitunguu utatafuta sana sema naitaka tunguli
 
Duh nikisikia huko Zenji huwa nawaza kuwa ni sehemu ya kipekee sana.
Lafudhi kama hizo vyakula tofauti vyao, mavazi,
Kama hujui unaweza mtia dole kweli.
Vipi mkuu pisi zipo huko zinatafunika?
Watu wanaingia na pigo gani?
Si muchezo Babaake! [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Kwl MKUU,,unawajuwa vzr
 
Mmmhhhhh.

Ha ha haaaa. Ati nimeajiriwa.

Mie mazizini nimekaa tangu mwaka 1989 mpaka nimehama kwa kuolewa.

Kipindi hiko Mazizini wanakaa wazungu tu na watu wenye hela zao. Mawaziri n.k

Sasa wewe mkuu Kim Jong Jr umekaa mazizini kipindi kipi na kwa muda gani?

Mitaa kama kilimani na michenzani flats nyingi wamekodi watu wa bara na wageni wengineo kama wakenya nk.

Huko mazizini pamoja na mbweni yake na Chukwani ndio wameenea. Wanakaa sana kwenye zile nyumba zinojengwa zilokuwa hazijaisha. Huanza mmoja baada ya muda utaona wamejazana.

Na sehemu hizo wamefungua sana biashara za magenge, vimeza vya machinga, vinyozi, saloon za kike, bodaboda ndio wapo wengi.

Wengine wanalima sana hasa mbogamboga na kuuza jumla masokoni.


Nlivosema sehemu ninofanya kazi. Mimi nimewapokea sana watu kutoka bara na tunaishi nao vizuri tu. Ndio mmoja wao kuropoka kuwa kakuta hali tofauti na alivokua anaskia. (Kasumba) za vijiweni

Maeneo kama fuoni, bububu na mwera watu wa bara wengi pia wanakaa kwa sasabu ndio njia za kuendea mahotelini wanakofanyia kazi.

Ubaguzi ni tabia ya mtu. Kipindi hicho unasema wabara wanabaguliwa kwa sbb matukio mengi ya uhalifu plus uhuni ukiskia watendaji huwa wa upande huo. Ila sasa watu wamejichanganya sana Zanzibar mpaka hayo mambo yamezoeleka.
 
Hana kichaa. Kwa sababu kuna wanawake wazuri.

Half cast za kiarabu na kihindi na kikomoro.

Unguja nzima umetembea lini weye huachi kuzugaaaa. Mmmhhhhh.

Zanzibar kuna wanawake wazuri tena sana. Labda tu kwa sbb hawavai nusu uchii
Hahaha kwanza wewe ni mwanamke Mimi ni mwanaume. Unadhani nani ana haki ya kusema mwanamke ni mrembo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…