Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Kiswahili kimeanzia Zanzibar,hata hichi ulichokiandika Kama sio Zanzibar usingeliandika

Nyerere alilazimisha Watanganyika lazima wajivunze Kiswahili baada ya kuipatia Tanganyika Uhuru

Zanzibar hakuna makabila, Wazanzibari halisi wamechanganyika damu na Warabu,Wahindi,Wasomali,Waafrika nk..

Lugha moja Tu Kiswahili..
Hahahaha eti kiswahili kimeanzia zanzibar na zanzibar Hakuna makabila sasa iweje zaidi ya 80% ya msamiati wa kiswahili unatoka kwenye makabila ya kibantu?

Nyerere ndio aliefundisha kiswahili? Wakati mjerumani alikuta tayari kiswahili kipo na akatafsiri Bible kutoka kijerumani kwenda kiswahili huko Bagamoyo na Bible hiyo kwa wakati huo huo ikawa inatumika kila pembe ya nchi?
 
Tafuta maana ya Swahili kwanza, Zanzibar hawaclaim kuwa ni wamiliki wa kiswahili bali ni lugha iliyokuwa ikitumika katika kufanya biashara maeneo ya mwambao na imechanganya misamiati kutoka katika lugha mbalimbali za kibantu na lugha za mataifa mengine pia, ikiwemo kireno, kifarsi, kihindi, kiarabu. Kama katika kusoma kwako uliwahi kukutana na kujadili mada za kiswahili ikiwemo:
1. Kiswahili ni Kibantu
2. Kiswahili ni Kiarabu
3. Kiswahili ni Pijini/Krioli zilizokomaa

Basi utakuwa umeelewa ninachomaanisha.
Kiswahili kipo toka miaka karne nyingi sana nyuma kimekua kikitumika Tanganyika nzima

Ila kimekua kikipanuka kimisamiati kila kilipokututana na lugha kutoka kwenye jamii mpya, wareno walivyokuja waliongeza msamiati, vile vile wahindi, waarabu, waingereza etc na ndio maana pia kwenye kiswahili kuna maneno beseni, penseli, televisheni, redio, suluhisho (solution), millioni, nambari, kilomita, propaganda, varanda, tochi etc

Nashangaa mbona kwa misamiati yote hii na mingine mingi kutoka English, kiswahili kisihusianishwe na kiingereza lakini kwa idadi almost the same ya msamiati kutoka kiarabu eti kiswahili ni kiarabu, Hakuna kitu kama hicho, kiswahili ni kibantu kitupu

Na Ukiwasikia washona wa Zimbabwe wakiongea kishona ndio utajua kiswahili ni kibantu kitupu sababu 40% ya kishona ni kiswahili

After all Kongo wamekua wakiongea kiswahili kwa miaka na mikaka hata kabla ya waarabu sababu kiswahili chao hata hakina Arabic borrowed words.
 
Wote ni wanaJF hakuna cha ziada lakini uongo au kupotosha hakusaidii, mimi ni mzaliwa wa huko na bahati nzuri naelewa jinsi ilivyokuwa/jina lilivyotokea, sasa huwa sikubali pale mtu anapotoa/kuongelea kitu isivyo sahihi.
Kuzaliwa huko hakukufanyi kila unachoongea kuhusu zanzibar kiwe ni kweli.
 
mzanzibar anayeponda muungano ni maamuma anayesubiria kuelekezwa na wachumia tumbo,hakuna mzanzibar timamu anaukataa muungano.

kwanza wao wanapata zaidi kuliko wabara amabo wanazushiwa kuwakandamiza.

zanzibari ina wajinga wawili watatu wanalilia ijitawale ili waishi kwa kutegemea ufadhiri wa nchi za kiarabu ziingie mifukoni kwao.ujinga kabisa.
Wasioutaka Muungano ni waarabu walowezi na wengine wa kuja, Sidhani kama hawa wa zanzibar halisi wanaotafuna mishahara na marupurupu ya kodi zetu za bara watataka kukata hiyo mirija

Zanzibar imekopa zaidi ya trillion 2 kwa kipindi cha miaka mitano iliopita kutoka kwa mgongo wa bara, zanzibar haina uwezo wa kukopesheka hata billion 300

Maana yake zanzibar wakimessup na hizo trillion 2 sisi ndio tunalipa deni lote hilo of course sisi ndio tunawalipia

Wanatumia umeme wetu wa bure kabisa gharama zao tunalipishwa sisi, huu Muungano unatutafuna sisi kuliko kawaida.
 
kuna mmama fulani wa kizanzibari alikuja home akawa anasema “bwana ...kafiliwa mwanae” nilistuka mpaka badae nilipoambiwa anamaanisha “bwana...kafiwa mwanae”
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] daah
 
Wazanzibari ni mchanganyiko wa Watu kutoka sehemu tafauti za Afrika nå Dunia..

Kila Kabila au kikundi fulani cha Watu kina historia yake ya vipi kimefika Zanzibar

Makabila ya kando kando ya Bahari ya Hindi ndio inasemekana kuwa ni watu wa mwanzo kuhamia Zanzibar

Wazaramo,Wadigo,Wasegeju haya ni makabila yaliyokuwa na utamaduni wa kuvua Kwa kuondoka sehemu zao za asili na kwenda sehemu nyengine na kupiga kambi(dago) kwa muda mrefu

Kabila la Kimanyema hawa waliletwa Kama Watumwa na Mwarabu

Kabila la kinyamwezi hawa walikuwa walinzi wa Sultani,kwahiyo hawa waliletwa nå Mwarabu..

Wahindi waliletwa na Sultan, Kama vibarua na ufundi mwengine,Kama Vile kujenga Nyumba,usaramala nk

Sultan aliletwa na Wazanzibari wa mwanzo waliohamia Katika visiwa hivi viwili ili aje awalinde na Mreno..

Wajemi(Wairani) Hawa walifika mwanzo Zanzibar kuliko Mwarabu,baada ya hawa kuondolewa na Mreno, ndio Wazanzibari wakamwita Mwarabu..

Zanzibar imeshawahi kuwa Empire kuna Empire nne Tu zinazojulikana duniania,Roman Empire,Othman Empire,Zanzibar Empire na British Empire

1964 Wakati Karume na Nyerere wanaiunganisha Zanzibar na Tanganyika kuwa Tanzania, Zanzibar ilikuwa na watu Laki tatu tu 300,000

Dini ndio kilikuwa kichochezi kikubwa Kwa Wazanzibari kumwita Mwarabu awalinde na Mreno

Dini ndio kichochezi kikubwa Kwa kupinduliwa Sultan 1964

Dini ndizo kichochezi kikubwa Kwa Zanzibar kulazimishwa kuungana na Tanganyika

Dini ndio kichochezi kikubwa Kwa Tanganyika kuing'ang'ania Zanzibar..

Dini ndio kichochezi kikubwa kuwekwa ndani na kusahauliwa kwa Masheikh wa Uamsho

Dini ndio itayokuwa kichocheo kikubwa kuvunjika kwa huu Mungano

Mark my word,save the day and today's date,one day you'll remember this..
Zanzibar empire..?,,kumbe mnaayenu ya siri
 
Ni kikundi cha Wazanzibari wanaoitwa CCM ndio wanaofagilia Mungano..

Kuna maslahi makubwa Sana Kwa hichi kikundi cha Wana CCM wa Zanzibar,Tanganyika imewafadhili sana hawa watu,..

Mzanzibari wa kweli hawezi kuufagilia Mungano,hakuna anaekubali nchi yake iwe Mkoa..

Mamlaka kamili ndio ndoto ya Mzanzibari
We unahisi sisi watanzania tunafaidika nini na muungano?
 
Kwa assumption zangu naona kama wadada na wanawake wengi wa kizanzibar wanajiheshimu na wana misimamo kuliko hawa wanawake wetu wa bara
Chuoni niliwahi kusoma na wadada kadhaa wa kizanzibar hata wanaume pia walikua very discipline. Muda wa msikitini utawakuta msikitini no matter what, wadada hao walikua very humble, hawapendi makuu, ikitokea ukamgusa tu hata kwa bahati mbaya jua ni ugomvi, and walikua very selected upande wa marafiki

Lifestyle yao ilinivutia sana. Sasa sijajua kama wote wapo hivyo au vipi, mwenye kuwafahamu anijuze.
 
wazanzibar ni wapole sana mpaka wamepitiliza ndio maana baadhi yao wakija bara hutapeliwa
 
Kiswahili kipo toka miaka karne nyingi sana nyuma kimekua kikitumika Tanganyika nzima

Ila kimekua kikipanuka kimisamiati kila kilipokututana na lugha kutoka kwenye jamii mpya, wareno walivyokuja waliongeza msamiati, vile vile wahindi, waarabu, waingereza etc na ndio maana pia kwenye kiswahili kuna maneno beseni, penseli, televisheni, redio, suluhisho (solution), millioni, nambari, kilomita, propaganda, varanda, tochi etc

Nashangaa mbona kwa misamiati yote hii na mingine mingi kutoka English, kiswahili kisihusianishwe na kiingereza lakini kwa idadi almost the same ya msamiati kutoka kiarabu eti kiswahili ni kiarabu, Hakuna kitu kama hicho, kiswahili ni kibantu kitupu

Na Ukiwasikia washona wa Zimbabwe wakiongea kishona ndio utajua kiswahili ni kibantu kitupu sababu 40% ya kishona ni kiswahili

After all Kongo wamekua wakiongea kiswahili kwa miaka na mikaka hata kabla ya waarabu sababu kiswahili chao hata hakina Arabic borrowed words.
Sawa mjuzi.
 
Ungemtumia DM kama ulitaka post yako isiingiliwe na yeyote zaidi ya uliemquote.
Sababu ya kuweka hapa, ni kutokana na hata yeye alichoongelea kipo hapa. Ila kusema niliyemquote ni kwasababu wewe hutoelewa zaidi ya niliyemquote.
 
Back
Top Bottom