Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Kuna waliokuja zanzibar kutoka tanganyika na mini dresses [emoji156], ila kwa sasa wanavaa baibui na hijaabu juu. Masha Allah
Zuchu katokea huko saivi anarudi huko kitovu wazi juzi nimemuona na miniskirt kabisa anawakosha roho.
 
Narudia tena weka maneno ya kiswahili, weka misamiati ya lugha nyingine za kibantu tuangalie mfanano ya lugha ya kiarabu tuone katika hayo maneno yatashabihiana na lugha zipi kati ya kibantu na kiarabu.
Sina huo muda sababu nimekuwekea link kutoka kwa wasomi wa lugha wamefanya tafiti zao, mwenzako kashazisoma jibu analo akusimulie
 
Sina huo muda sababu nimekuwekea link kutoka kwa wasomi wa lugha wamefanya tafiti zao, mwenzako kashazisoma jibu analo akusimulie
Hata usemeje, asilimia kubwa ya misamiati ya kwenye kiswahili inatokana na kiarabu na wala haiingiliani lugha za kibantu.
 
Hata usemeje, asilimia kubwa ya misamiati ya kwenye kiswahili inatokana na kiarabu na wala haiingiliani lugha za kibantu.
Kama ndio hivyo watanzania wote tungeelewa kiarabu kama Tunavyoelewa kiswahili
 
Kama ndio hivyo watanzania wote tungeelewa kiarabu kama Tunavyoelewa kiswahili
Achana na kuongelea Watanzania kwasababu, Watanganyika wote wana lugha zao za kiasili (mother tongue) na Kiswahili ni second selection. Tofauti na Wazanzibari. Ukubali ukatae ukweli ndio huu.
 
Kiswahili ni kibantu sababu moja kuu ni kwamba zaidi ya asilimia 90 ya msamiati wake ni kibantu

Baraza la Kiswahili Tanzania lenye mandatory na hii lugha na machapisho yote ya Utafiti kwa wasomi wa vyuo vikubwa duniani kama Oxford mpaka Mlimani wametoa conclusions kwamba kiswahili ni kibantu wewe ni nani unapinga?
Mimi ni Mswahili.. Kiswahili ni lugha niliyofundishwa na mama..'mother tongue'

Hawa wanaojiita Baraza kuu la Kiswahili si ndio hawa waliokiita KICHONGEO jina la KIFIRIO??🙂
 
Mgeni akifika Zanzibar, watu wa huku ukiwatizama wanazuga kama hawana tyme nae!

Lakini lazima huwa wanamfuatilia nyuma nyuma kuona anaelekea wapi na ni mgeni wa nani!
Wakishajiridhisha mahala ulipofikia wakikuona tena!!

Utawasikia " Huyu si aishi pale kwa Ariiiiii!!" (Yaani mgeni wa Ally)

Wanawake huku Zanzibar waoga sana kusemeshwa njiani na mtu wa bara, yaani hata ukimsalimia anaitikia kwa sauti ya chini wala hasimami!

Huku Zanzibari;
  • Round about inaitwa (ikipinda) au (mviringo), kwenye daladala utasikia Shusha hapo ikipindaaah! Maana yake shusha round about
  • Huku Zanzibar sufuria linaitwa dishi,
  • Kisima cha maji kinaitwa kisima cha kuvuta
  • Huku hakuna fundi bomba Bali kuna fundi mfereji, ukitaka maji ya bomba inabidi useme unaomba maji ya mferejini
  • Pombe wanaita- moja moto moja baridi
  • Ukitafuta chupi utazunguka sana hupati hadi useme unatafuta HAFU
  • Shule huku zinaitwa skuli
  • Ukitaka kununua chepe/koleo huku hawalijui hadi useme unataka Li-PAULO
Hakika huku Zanzibar ni tabu tupu, nasubiri tarehe 30 nirudi zangu bara!
Hahahahaha wanazingua hao, sehemu ikiwa na mwembe basi kishakua kituo iko unaskia 'em nipeleke pale mwembeniii'
Kukiwa na kona basi utaskia 'nishushe apo konaniii'
 
Mimi ni Mswahili.. Kiswahili ni lugha niliyofundishwa na mama..'mother tongue'

Hawa wanaojiita Baraza kuu la Kiswahili si ndio hawa waliokiita KICHONGEO jina la KIFIRIO??🙂
Hahahaha ni kifirio huko kwenu, huku tunajua ni kifutio

Yeah kifutio kama rubber, KICHONGEO kinatafsiriwaje tena wakati tayari kinaeleweka
 
Achana na kuongelea Watanzania kwasababu, Watanganyika wote wana lugha zao za kiasili (mother tongue) na Kiswahili ni second selection. Tofauti na Wazanzibari. Ukubali ukatae ukweli ndio huu.
Hivi unajua English ni German 60% lakini hutosikia eti huu ujinga unasema hapa kuhusu kiswahili

Arabic ni Hebrew 50%
 
Hahahahaha wanazingua hao, sehemu ikiwa na mwembe basi kishakua kituo iko unaskia 'em nipeleke pale mwembeniii'
Kukiwa na kona basi utaskia 'nishushe apo konaniii'
Upekee wa kitu, mazingira kilipo na urahisi wa kutamkika ni rahisi sana kuwa ndio umaarufu wa eneo.
 
Arabic ni Hebrew??[emoji2445][emoji2445][emoji2445][emoji377][emoji377][emoji377]
Arabic is a Central Semitic language, closely related to Aramaic, Hebrew, Ugaritic and Phoenician.
 
Hahahaha ni kifirio huko kwenu, huku tunajua ni kifutio

Yeah kifutio kama rubber, KICHONGEO kinatafsiriwaje tena wakati tayari kinaeleweka
Kifutio =rubber

KICHONGEO = Sharpener .. Kiswahili cha kwetu

KIFIRIO kwa Kiswahili cha baraza kuu la Kiswahili = Sharpener:-O
 
Kifutio =rubber

KICHONGEO = Sharpener .. Kiswahili cha kwetu

KIFIRIO kwa Kiswahili cha baraza kuu la Kiswahili = Sharpener:-O
Neno kifutio na kichongeo yote ni maneno ya kibantu.
 
Yaani ni kwamba hata misamiati iliopo kwenye Arabic na yenyewe imetoka kwenye lugha nyingine tofauti, so point yako haina uzito
Point yangu haina uzito ila tambua miongoni mwa lugha ambayo misamiati yake inatumiwa na lugha nyingine basi ni kiarabu, kwani kimejitosheleza na hakikopi misamiati kutoka kwenye lugha nyingine, isipokuwa hizo lugha nyingine ndio zinakopa kwa Kiarabu.
 
Back
Top Bottom