Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Hahah sawaswa hatujisifu nadhani katika east africa zanzibar ni number one, kw maqueen, ukitaka kuwaona nenda forodhani kuanzia saa 12 jioni (forandani ya znz)
 
Mgeni akifika Zanzibar, watu wa huku ukiwatizama wanazuga kama hawana tyme nae!

Lakini lazima huwa wanamfuatilia nyuma nyuma kuona anaelekea wapi na ni mgeni wa nani!
Wakishajiridhisha mahala ulipofikia wakikuona tena!!

Utawasikia " Huyu si aishi pale kwa Ariiiiii!!" (Yaani mgeni wa Ally)

Wanawake huku Zanzibar waoga sana kusemeshwa njiani na mtu wa bara, yaani hata ukimsalimia anaitikia kwa sauti ya chini wala hasimami!

Huku Zanzibari;
  • Round about inaitwa (ikipinda) au (mviringo), kwenye daladala utasikia Shusha hapo ikipindaaah! Maana yake shusha round about
  • Huku Zanzibar sufuria linaitwa dishi,
  • Kisima cha maji kinaitwa kisima cha kuvuta
  • Huku hakuna fundi bomba Bali kuna fundi mfereji, ukitaka maji ya bomba inabidi useme unaomba maji ya mferejini
  • Pombe wanaita- moja moto moja baridi
  • Ukitafuta chupi utazunguka sana hupati hadi useme unatafuta HAFU
  • Shule huku zinaitwa skuli
  • Ukitaka kununua chepe/koleo huku hawalijui hadi useme unataka Li-PAULO
Hakika huku Zanzibar ni tabu tupu, nasubiri tarehe 30 nirudi zangu bara!
Kuna siku Mkuu wa wilaya alikua kwenye mkutano akawambia masheha waliokutwa na tuhuma ya wizi " WANANCHI EEH!, KAMA MASHEHA HAWA WANA HATIA BASI IMETOKAA HIYOOOOOO!" msuto mtupu. Zenji hautakiwi kutumia nguvu kabisa
 
Hana kichaa. Kwa sababu kuna wanawake wazuri.

Half cast za kiarabu na kihindi na kikomoro.

Unguja nzima umetembea lini weye huachi kuzugaaaa. Mmmhhhhh.

Zanzibar kuna wanawake wazuri tena sana. Labda tu kwa sbb hawavai nusu uchii
Sielewi unalotetea.
Z'bar kiukweli hakuna pisi kali.
Iwe mkokotoni, iwe jambiani, iwe matemwe hakuna pisi kali.
Pengine labda uvizie wa kuja.
 
Mnabishana ujinga. Uzuri wa mwanamke ni nini? Kila mtu atakupa jibu lake.

Umetaja Matemwe umenifurahisha, napapenda Matemwe
 
Wabongo bana ...aliesema Kiswahili kimehamia bara wa hakukosea ...sisimizi/nyenyere bado kidogo niseme Nyerere!!
 
Kule Bububu kuna sehemu inaitwa bububu kwa nyanya yaani nilikua nacheka sana nikisikia hilo jina. Kingine umesahau nyanya maji wanaita Tungule.

Mti wanaita kijiti, Shamba wanaita kondeni.

Sasa vituko full nilivipata sehemu fulani inaitwa jambiani, huko Kiswahili chao huwezi kukielewa. Niliuliza mtu anielekeze sehemu yaani alivyonielekeza hata sikumuelewa. Kuna mdada alimwambia jamaa "Kama unan'tenda nintende, Sio unanichezea kama kijibwa chaja"[emoji3][emoji3] Hapo jamaa anaambiwa kaa unanifanya nifanye sio unanichezea kama kimbwa kitoto... Jambiani, Kizimkazi na Makunduchi is a place to be. Nilipenda sana mazingira yake
Sasa ukute alieanzisha huu uzi ni mtu kutoka Mbeya kakaribishwa tu bongo tena kakaribishwa na Mzanzibari ...sasa akisema marikiti na wewe unasema sokoni zote hizo ni lugha za kigeni leo ujifanye unajua Kiswahili kuliko Mzanzibari
 
Ongeeni yooote ila msisahau kwamba Zenji ndio nchi ya kwanza kuwa na televisheni ya rangi Afrika nzima
Yaani hapa wanadanganyana tu wao wanajiona wako right wakati hio Dar wanayoringia Wazanzibari ndo waliowajanjarusha ukivuka Ubungo kwenda mbele ni kiza na vichekesho na mara huyu mtoa post hapo Dar anapojiona kafika kakaribishwa na Mpemba
 
Sasa ukute alieanzisha huu uzi ni mtu kutoka Mbeya kakaribishwa tu bongo tena kakaribishwa na Mzanzibari ...sasa akisema marikiti na wewe unasema sokoni zote hizo ni lugha za kigeni leo ujifanye unajua Kiswahili kuliko Mzanzibari
Hapo na kajitahidi kuuweka uongo mwingi akijua labda hamna wazanzibari humu. Na wasojua ukweli hawajui kama jamaa kaja kuwafurahisha tu
 
Sielewi unalotetea.
Z'bar kiukweli hakuna pisi kali.
Iwe mkokotoni, iwe jambiani, iwe matemwe hakuna pisi kali.
Pengine labda uvizie wa kuja.
Hamna pisi kali kwa sababu hawatembei nusu uchi.

Watu waliochanganya makabila ya kiarabu na kicomoro na wahindi wataacha kuwa pisikali.

Ntahamaki saivi nipost picha yangu humu.
 
Hamna pisi kali kwa sababu hawatembei nusu uchi.

Watu waliochanganya makabila ya kiarabu na kicomoro na wahindi wataacha kuwa pisikali.

Ntahamaki saivi nipost picha yangu humu.
Ntahamaki saivi nipost picha yangu humu...!!!uuwiii hapanaaa....nitunzieee
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]
 
Back
Top Bottom