Hukumu dhidi yangu: Asante Watanzania, asante Ndugu na Marafiki

Hukumu dhidi yangu: Asante Watanzania, asante Ndugu na Marafiki

Kuna mwenye hamu na CCM?! Mwanakijiji, Pascal Mayala tunatumia jukwaa moja huku mkiunga mkono watesi
Huu ni uthibitisho mwingine jinsi Tanzania na utawala wa sasa unavyozingatia na kutenda haki. Isingekuwa hivyo asingerudi hapa jukwaani na kuweka tabasamu hilo.
 
Melo tumetoka mbali pamoja na nakupa pole sana kwa msukosuko huo, ila kumbuka kuwa road bump siyo mwisho wa barabara. Hiyo sheria waliyotumia kukushitaki ni sheria mbovu sana ambayo inahitaji kupigiwa kelele ifutwe. Inapingana kabisa na katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania aya ya 18 kifungu kidogo cha kwanza na cha pili kwa watumiaji wa JF kwamba wana haki ya kutia mawazo yao na wana haki ya kupata habari.

Wewe kama msimamizi wa hii forum, haina maana kuwa unajua watu wote wanaoitumia, watu wengine hujiandikisha kwa kutumia alias za ajabu kama vile "kichuguu" kwa kutumia VPN na huna machinery ya kuverify kuwa hayo ndiyo majina na contacts zao, na wala IP zao huwa siyo zile zile bali zinabadilika kila wanapolog in hata kama ulikuwa una-trace IP address zao huwezi kujua wako wapi. Huna makosa yoyote kabisa labda wangesema kuwa unashitakiwa kwa kuhost website hiyo.
 
"Safari itaendelea, Maisha yataendelea na hakuna kurudi nyuma" - Melo.

Vyema umetambua hilo, haya mapambano yataendelea kuwepo siku zijazo ni vyema uwe tayari kukabiliana nao wakati wowote, usiogope.

All the best.
 
Shukran sana.
Team Lumumba ikiongozwa na Mwanakijiji
Mnajisikiaje??
Ndio maana kwenye harakati usimuamini mtu, baki wewe na nafsi yako!

Mwanakijiji alikesha kuandika makala nyingi enzi za Kikwete leo kalegea lege!

Inashangaza Sana!
 
Sijaelewa.

Ngoja nisome tena.
Amina, Mungu ametenda, ila tusiogope kuendeleza utashi wetu tulio pewa na Mungu maana katupa kujipambanua wenyenye, ndo maana tuko na kiumbe kiitwacho Shetani kutoka jina la (LUCIFER) Mungu mwana-demokrasia namba 1 viva viva mapambano yanaendele. WEMA UTASHINDA UBAYA. USIKU MWEMA WADAU.
 
Pole sana bwana Max, Watu imara hupata misuko suko mingi sana.
 
Back
Top Bottom