Hukumu dhidi yangu: Asante Watanzania, asante Ndugu na Marafiki

Hukumu dhidi yangu: Asante Watanzania, asante Ndugu na Marafiki

Safari ya kupigania UELEWA ni ndefu mno.

Ni sawa na safari ngumu ya mtoto KUJIFUNZA.

Tulipo sipo pale pa JANA... kama Taifa tumetoka kupata habari magazetini, redioni mpaka kuja BLOGU, ziko zilizokuwa za UDAKU mpaka zile MAKINI.

Leo tuna FORUMS tofauti kama JAMII FORUMS (hakika ni hatua adhimu isiyoweza KUFANYIWA KEDI).

Kitu kigumu duniani ni kubadilisha UELEWA WA WATU (understanding) na kamwe TUSIWAONE MAADUI WENYE KUPITILIZA wale wote wenye UELEWA tofauti na kizazi chetu hiki chenye MABADILIKO MAKUBWA kiuchumi, kisiasa,kisayansi na kijamii.

Wako watu waitwao "wahafidhina," hawa si wa kuwatukana bali ni kuzidi kutumia NJIA BORA zenye kupeleka ujumbe MARIDHAWA ambao itafika SIKU watakuja kuuelewa tu. Kama HAWATAJIBIDIISHA kuelewa WAKIWA HAI basi watakuwa kama wale waitwao "GOYYIMS" na ndugu zetu WAYAHUDI.

Kizazi chetu na cha watoto wetu kinapitia zama zinazoonekana HATARI kubwa kwa NORMS zetu "WAAFRIKA" kitamaduni na hata kisiasa kwani UWAZI ULIOPITILIZA si miongoni mwa "elimu" ifundishwayo kuanzia UNYAGONI, JANDONI na masimulizi ya WAHENGA wetu, hapa ndipo ILIPO CHANGAMOTO kubwa kwa wale wanaoonekana FOREMEN wa kuyaleta "haya" mabadiliko MAPYA.

Kubwa ni kutambua kila zama zina mambo yake, na ni ngumu kwangu kuziishi zama alizoishi BABA WA BABU YANGU. Kubwa ni kuyachukua mazuri yao, kuyaboresha na kujua kuwa Kuna KESHO YANGU lakini pia kesho ya WAJUKUU ZANGU ambayo SITOWEZA KUIZUIA. Kubwa ni kuwakumbusha tu WASIZIACHE zile TUNU ADHIMU za UTU WA MWAFRIKA na TAMADUNI ZETU, kazi itakuwa ni kwao.

Tunaishi Katika dunia ya UTANDAWAZI ambao una changamoto zake ila hauwezi KUZUILIKA wala KUKATALIKA na jamii za walimwengu.

Hapohapo hatuna budi kutii SHERIA zilizopo...kubwa tu ni jukumu la WABUNGE WETU kutunga SHERIA zisizo za KUKOMOANA...na pia SHERIA zinazoendana na CHANGAMOTO YA DUNIA YA SASA.

Kama Taifa ni IMANI yangu kubwa TUTAFIKA kwa kila mmoja wetu kumuelewa MWENZAKE though it takes time ila DESTINATION hiyo HAITOEPUKIKA.
 
Pole na misukosuko ya kesi na hongera kwa ushindi.
 
Nikuombe tu Melo endelea kuwa na msimamo huohuo usibadilike, simama na wanyonge, simama upande wa haki, simama na wanaoonewa, pamoja na hukumu kutolewa kama mtego kwako bila shaka wanasheria wako wamekwambia nini cha kufanya.
 
Nimekupongeza mahala Mtani na Kaka. Naendelea Kukupongeza na hapa tena japo nakuomba na pia nakushauri kama itakupendeza kwa sasa hakikisha usalama wako unakuwa ni mzuri, usiamini kila Mtu hasa marafiki wapya watakaojitokeza sasa.

Historia inaonyesha Wababe wakishindwa kortini (Mahakamani) hauamua kufanya mengineyo ya hatari ili kukamilisha azma yao. Jilinde nasi tunakuombea Ulinzi kwa Mungu.
 
Huu ndio ukweli unaofichwa, kuna watu kadhaa wanatumia JF lakini wanafurahia unyama huu na wanaunga mkono
Kwanza hakuna unyama kwenye kutekeza sheria ya nchi, hapo haki imetendeka!

Pili kutumia JF hakuwezi fanya washiriki wote kuwa na mitazamo sawa abadani. Kama ilivyo kwa nchi, humu pia kuna kanuni za kufuata na mods wanazisimamia haswaa!

Tatu siyo sawa kuwasimanga watu kwa kutumia haya majukwaa halafu wakatofautiana na mmiliki. Hata Lissu, pamoja na kuponda karibu kila kitu cha serikali, bado serikali ilimhakikisha uwepo wa miundombinu na huduma (pamoja na ulinzi) kwa muda wote alipokuwa Tanzania.

Watu wawe huru, tuvumiliane tu.
 
Kuna mwenye hamu na CCM?! Mwanakijiji, Pascal Mayala tunatumia jukwaa moja huku mkiunga mkono watesi
Hahaha Magufuli kachaguliwa na nani. Hivi unawajua Watanzania wewe wakati majority wakiwa vijijini. Mwana kulitafuta mwana kuliget. Tukutane tena ukiniona 2025
 
Nawaza muheshimiwa Mungu aliyetajwa na muapishwaji ataichukuliaje hukumu hii vijana wake wanaweza kata rufaa kwamba kwanini hakimu hakumfunga Melo na JF haikufutwa kama magazeti yalivyo fanyiwa.
 
Hongera Melo, ushauri wangu omba asylum taifa linalojitambua na kuamini katika uhuru wa habari. Pia boresheni mfumo usajili uwe automatic bila email ya muhusika. Nina hofu sana ipo siku tuendako utatekwa na kubinywa utoe master key!! Maisha ya wengi yawe hatarini.
 
Pole Sana mkuu , nimefuatilia Sana kesi yako ni umagumashi na upuuzi mtupu.

Hata hukumu uliyopewa ni upuuzi na ujinga mtupu wa huyo hakimu kama utaridhia nakushauri ukate rufaa usafishe jina lako.
 
Wacha niandike kitu hapa;

Mkuu Maxence, Enzi za Mitume na Manabii katika wakati wa majaribu mengi walitokea mashujaa waliosimama kutetea na kusimamia kila ambacho walikiamini na kukihubiri. Hawa ndio mashujaa ambao leo hii wanaitwa Mitume na Manabii. Walitimiza wajibu wao kwa wakati wao na historia ikawahukumu.

Katika nyakati zao walikuwa tu ni sehemu ya jamii kama wanajamii wengine.Mawazo,fikra na misimamo yao ilikuwa ni ya tofauti inagwa haikuchukuliwa mzaha. Watu hawakuona umuhimu wa waliyosema na kusimamia mpaka wakati wao ulipopita. Uimara na utahbiti wao uliweka misingi imara na kuwaingiza katika historia kama watu mashuhuri na mashujaa wa nyakati zile ambazo zilikuwa za kiza na mateso.

Mkuu Maxence sijua unapitia magumu kiasi gani kwa nafasi yako hasa unapkuwa na mzigo wa kuwa sura pekee ya Jamii forum ambayo imejijengea heshima kama jukwaa ambalo limewapa watu wengi fursa kwa nafasi mbali mbali.Maadui zako kwa kujua ama kutokujua wanatimiza jukumu la msingi la kukuimarisha kukuwekea msingi imara wa kufanya kazi yako uliyotumwa. Kuwa sura ya jukwaa ambalo linawatu wenye sura na mitazamo tofauti sio jambo rahisi na jepesi ni jukumu kubwa sana.Kwani hata liksemwa baya basi wale walioumizwa watasema ni wewe na JF yako ndo mmetenda ubaya kwao.

Kwa kuzingatia hili naomba nikupe moyo kwamba YOU are DOING your BIT in the BIG and GOD will do THE BIGGEST.Usife moyo wala kuacha kupigana vita hii ya kulitetea taifa lako.Vita hii si kwa ajili ya kuitetea JF bali ni kutetea Misingi ya TAIFA letu.Ni misingi ya kutetea UTAIFA wetu.

Tukiruhusu kuwa na taifa la watu waoga na wanaogwaya kutoa maoni yao hasa pale yanapokinzana na maoni ya watawala tutakuwa ni TAIFA la wapumbavu.Tutakuwa taifa PUMBAVU. Kama viongozi wetu watafikiri kwamba watu wenye mawazo kinzani ni maadui basi watakuwa ni VIONGOZI WAPUMBAVU sana na ukweli huo hauwezi kubadilishwa kwa kuifungia mitandao ya kijamii kwani hata kabla ya kuwepo kwa mitandao watu walipashana habari na ujumbe ulifika.

Mimi binafsi natambua mchango wako na Mchango wa JF katika safari ya Maendeleo ya taifa.Huu ndio mtandao mkubwa kabisa wa kijamii wa lugha ya kiswahili,ndio jukwaa ambalo vipaji vya uandishi vinaibuka kwani binafsi sikufikiri naweza andika andiko refu kiasi hiki kukuhusu wewe mpaka nilipo anza andika ndani ya JF.

Naomba nikupe MOYO kwake neno.:UWE na MOYO mkuu,Usiwaogope wauuao MWILI bali mwogope yule ambaye anaweza kuuua mwili na kuitupa ROHO katika Jehanum.'

Watu madhalimu watajaribu kubeza nafasi yako kwa sababu zako binafsi ila ukweli utabaki kuwa umesimamia ulichokiamini na kwa hilo naomba nikupe KONGOLE pamoja na BARAKA NYINGI SANA ZIKE JUU YAKO NA KATIKA MAISHA YAKO NA UWEZO MKUU WA MUNGU ALIYE JUU UKAWE JUU YAKO SASA NA KATIKA NYAKATO ZAKO

Ni mimi Mtawa wa Nyakati niliye mkuu kati ya wakuu na mdogo kati ya wadogo.Niliye huru kati ya watumwa na mtumwa kati ya walio huru na niliyemjinga kati ya wajinga na mwenye hekima kati wenye hekima Niliye hai kati ya wafu na mfu kati ya waliyo hai.Niliyepo kati ya waliomo Niliyechagua kuishi bila kuisha.

Nakutakia Baraka TELE na AMANI ya KWELI Moyoni Mwako
 
Huu ndio ukweli unaofichwa, kuna watu kadhaa wanatumia JF lakini wanafurahia unyama huu na wanaunga mkono, nakaribia kuishiwa uvumilivu siku chache zijazo nitawataja waziwazi, nitakaowakwaza wanisamehe, hatuwezi kufuga majini ndani ya chupa, iko siku yatachoropoka na kuanza kula watoto.

Liwalo na Liwe.
Endelea kuwa mstahimilivu hoja hujibiwa kwa hoja.
 
Oh you beautiful thing Max. Stay blessed abundantly my brother!
 
Huu ndio ukweli unaofichwa, kuna watu kadhaa wanatumia JF lakini wanafurahia unyama huu na wanaunga mkono, nakaribia kuishiwa uvumilivu siku chache zijazo nitawataja waziwazi, nitakaowakwaza wanisamehe, hatuwezi kufuga majini ndani ya chupa, iko siku yatachoropoka na kuanza kula watoto.

Liwalo na Liwe.
Usisahau alilosema hapo juu mkuu 'Max': "Uhuru wa kujieleza."
Wewe utakuwa na haki ya kuyataja hayo majamaa; lakini yenyewe pia yanayo haki ya kujieleza.
Kwa bahati mbaya sana haki yanayoitumia inasababisha mateso, maumivu kwa wengine wasiokuwa na njia ya kuyaumiza hata menyewe!

Pangekuwepo na haki, hata haya yangestahiri kupelekwa mahakamani na kupewa vibano mbalimbali yanayovishangilia hapa jukwaani.

Lakini huenda kuna siku, HAKI ITATENDEKA.
 
Back
Top Bottom