Melo tumetoka mbali pamoja na nakupa pole sana kwa msukosuko huo, ila kumbuka kuwa road bump siyo mwisho wa barabara. Hiyo sheria waliyotumia kukushitaki ni sheria mbovu sana ambayo inahitaji kupigiwa kelele ifutwe. Inapingana kabisa na katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania aya ya 18 kifungu kidogo cha kwanza na cha pili kwa watumiaji wa JF kwamba wana haki ya kutia mawazo yao na wana haki ya kupata habari.
Wewe kama msimamizi wa hii forum, haina maana kuwa unajua watu wote wanaoitumia, watu wengine hujiandikisha kwa kutumia alias za ajabu kama vile "kichuguu" kwa kutumia VPN na huna machinery ya kuverify kuwa hayo ndiyo majina na contacts zao, na wala IP zao huwa siyo zile zile bali zinabadilika kila wanapolog in hata kama ulikuwa una-trace IP address zao huwezi kujua wako wapi. Huna makosa yoyote kabisa labda wangesema kuwa unashitakiwa kwa kuhost website hiyo.