#HABARI: Wakazi wa mji wa Idlib nchini Syria wamekusanyika kusherehekea baada ya mahakama kumhukumu kifo Rais wa zamani wa nchi hiyo, Bashar al Assad.
Mahakama moja nchini Syria imemhukumu kifo kwa kutokuwepo rais wa zamani wa nchi hiyo, Bashar al-Assad, kwa makosa yanayohusiana na uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita.
Mahakama hiyo pia imemhukumu kifo ndugu yake mdogo, Maher al-Assad, kutokana na jukumu lake katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 14 nchini Syria.
Mtu mwingine aliyehukumiwa kifo ni Atef Najib, mpwa wa Bashar al-Assad, ambaye alihusishwa na kuongoza operesheni za usalama zilizochochea maandamano katika mkoa wa Daraa mwaka 2011.
Najib alikuwa mkuu wa Tawi la Usalama wa Kisiasa katika mkoa wa Daraa wakati wa utawala wa Bashar al-Assad. Anakabiliwa na tuhuma zinazohusiana na ukandamizaji wa maandamano ya wananchi.
Bashar al-Assad na ndugu yake Maher walikimbilia nchini Urusi baada ya waasi kuingia Damascus .
Picha za mitandaoni zinaonyesha watu wakishangilia katika mitaa ya Idlib, huku baadhi yao wakipanda magari na wengine wakiimba na kusherehekea uamuzi huo wa mahakama.
Haya yanajiri baada ya Mahakama ya Syria kumhukumu kifo dikteta aliyeondolewa madarakani Bashar al-Assad licha ya kutokuwa mahakamani, baada ya kumpata na hatia kwa makosa ya kivita na uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Assad alikimbilia Urusi pamoja na familia yake baada ya utawala wake kupinduliwa mwezi Desemba mwaka 2024, jambo lililohitimisha utawala wa familia yake uliodumu kwa miongo mitano.
Katika kesi hiyo hiyo, mahakama pia ilimhukumu kifo Atef Najib, binamu yake Assad na aliyekuwa mkuu wa usalama wa kisiasa katika jimbo la Deraa kusini mwa Syria.
Alionekana akiwa ndani ya kizimba mahakamani wakati jaji akisoma hukumu yake. Jimbo la Deraa linachukuliwa kwa kiasi kikubwa kuwa mahali ambapo vuguvugu la uasi dhidi ya utawala wa Assad lilianzia.
Mnamo Machi 2011, kukamatwa na madai ya kuteswa kwa kundi la vijana walioshtakiwa kwa kuandika maandishi ya kupinga serikali kwenye kuta kulichochea maandamano jijini humo, ambayo yalikabiliwa na ukandamizaji mkali kutoka kwa vikosi vya usalama.
Hatua hiyo ilichochea maandamano nchi nzima yaliyogeuka kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya mamia ya maelfu ya watu.
Serikali ya mpito ya Syria ilianza kuwashtaki maafisa waliohusishwa na utawala wa Assad ambao ulitawala nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 50, mapema mwaka huu.
#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania.