The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Leo Juni 14,2021 ni siku ya Hukumu ya Mpaluka Nyagali Mdude (32) kwa jina maarufu Mdude CHADEMA.
Namuombea Mdude, Hakimu atakaye soma hukumu Mwenyezi Mungu ampe Hekima kama ya Mfalme Suleiman.
Awali Upande wa mashtaka umemuondolea kada wa chadema, mdude nyagali shtaka la uhujumu uchumi lililokuwa likimkabili na kumfungulia shtaka la jinai la kusafirisha dawa za kulevya.
Inadaiwa Mdude CHADEMA ambaye ni mkazi wa Itezi Jijini mbeya, kakamatwa na kushitakiwa kwa tuhuma za kupatikana na unga unaodhaniwakuwa ni dawa za kulevya aina ya heroine. kufuatia taarifa za kiintelijensia zilizopatikana, mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 10.05.2020 majira ya saa 17:00 jioni katika msako.
Mara baada ya kukamatwa kwa huyu mtuhumiwa, polisi walikwenda nyumbani kwake mtaa wa mwasote – itezi jijini mbeya kwa ajili ya kufanya upekuzi na katika upekuzi huo kulikutwa busta tano [05] za unga udhaniwao kuwa dawa za kulevya aina ya heroine wenye uzito wa gram 23.4 ambao ulikuwa umehifadhiwa kwenye mfuko wa kaki ambao ndani yake kulikuwa na mifuko midogo miwili ya nylon. Pia matumizi ya dawa za kulevya ni kinyume na sheria ya udhibiti, utumiaji na usafirishaji wa dawa za kulevya ya mwaka 2015 kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kwa mara.
Zaidi, soma: Mbeya: Mpaluka Nyagali Mdude akamatwa na Heroin, apandishwa kizimbani akikabiliwa na mashtaka ya Uhujumu Uchumi
- Mbeya: Mahakama imeahirisha kusoma hukumu ya Mdude Nyagali hadi Juni 28, 2021