Bado ubongo wa Binadamu ni juu sana zaidi ya computer kiuwezo.
Kuna kipindi niliwahi kufanya maamuzi mawili kwa wakati mmoja kwa kasi kuliko hata mwanga unavyosafiri.
Nikiwa nimemuazima Rafiki yangu pikipiki nijifunze kuendesha, alinipatia kiroho safi, lakini muda huo ananikabidhi niliichukua kimihemuko bila kujua breki ni ipi sababu alipokaribia kusimama niliona aliachia klachi pikipiki ilisimama nami nilijua hiyo hiyo ndiyo breki.
Nilienda umbali wa 4 KM nikiachia klachi na pikipiki kupunguza mwendo nikijidanganya akilini kuwa hiyo ndiyo breki yake pikipiki hadi nilipogeuza na kurudi home.
Niliporudi salama nilisifiwa na marafiki kuwa nami ni miongoni mwao madereva wazuri wanaojua kuendesha pikipiki, hatimaye kichwa kikajaa sifa nyingi kupita kiasi na nilivuta mafuta ya kutosha kwenye pikipiki kuingia ndani ya fensi umbali wa mita 15.
Baada ya kuvuta sana mafuta na kuachia pikipiki iende na iliondoka kwa kasi kubwa sana, mbele kulikuwa na fensi ya sing'enge na nguzo ya umeme, cha ajabu akili ilinipatia ufumbuzi mara 2 baada ya kuona kila nilipoachia klachi pikipiki isimame nikidhani ni breki lakini haikusimama.
Akili ya kwanza ilikuwa kulazimisha kupita na pikipiki 1 kwa 1 kwenye fensi ila akili wakati huo huo hiyo akili ilinikataza kuwa nitaweza kufa, basi nibadili maamuzi.
Akili ya pili iliniambia nikiona bado naenda mbele nilazimishe kuilaza pikipiki iserereke huenda ikaacha kuendelea na mwendo wa kasi iliyokuwa nayo ila akili hiyo hiyo ilinikatalia kuwa naweza kuvunjika miguu na kuchubuka vibaya sana, hatimaye akili ya pili ndiyo niliyofanya nayo maamuzi na kupona ingawa moshi wa pikipiki uliniunguza mkono baada ya kufanikiwa kulala na pikipiki chini huku matairi yakiwa yanazunguk, nikizidi kusifiwa na kujikuta huo moshi unaniunguza mkono wa kushoto lakini nilitoka mzima kabisa.
MASWALI:
Muda ulikuwa ni sekunde zisizozidi 2, lakini ubongo ulifanikiwa vipi kuchakata hizo akili zote 2 kwa wakati mmoja, kujadili na kufanya maamuzi sahihi kwa muda mchache tu huo wa sekunde 2?