Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema serikali ya Tanzania inapaswa kuchukua hatua madhubuti ili kuondoa hali ya kuzorota kwa hali ya haki za binadamu kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Taarifa iliyotolewa Jumatano na shirika hilo, imeeleza kuwa tangu mwezi Juni mamlaka imekuwa ikiwamakata kiholela mamia ya wafuasi ya upinzani, kuzuia mitandao ya kijamii, kupiga marufuku vyombo binafsi vya habari, na imekuwa ikihusishwa na utekaji nyara na mauaji ya kiholela ya wakosoaji wanane wa serikali.
“Tangu mwezi Juni, mamlaka zimewakamata kiholela mamia ya wafuasi wa upinzani, kufungia vyombo huru vya habari na kuhusishwa na kutekwa na mauaji ya wapinzani wasiopungua wanane” - ripoti ya Human Rights Watch.
Human Rights Watch wanasema ndani ya miezi michache iliyopita kumekuwepo na matukio mengi ya uvunjifu wa haki za binaadamu nchini Tanzania hali inayotia hofu kuelekea uchaguzi huo.
Oryem Nyeko, mtafiti mkuu wa Afrika katika shirika la Human Rights Watch anasema mamlaka Tanzania zimeonyesha kuongezeka kwa kutovumilia uhuru wa kujieleza kwa kuwabana wakosoaji wao, na wapinzani wa kisiasa. Nyeko anasema serikali inapaswa kukomesha haraka wimbi la ukandamizaji au hatari ya kuongezeka kwa mazingira ya kisiasa ambayo tayari yana wasiwasi, kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika Novemba 2024.
Human Rights Watch imesema mamlaka pia inakabiliana na wale wanaoibua wasiwasi kuhusu kutekwa na kupotea kwa watu. Mwezi Agosti, chama kikuu cha upinzani CHADEMA kilitangaza kufanya maandamano jijini Dar es Salaam kupinga hatua ya serikali kuzembea katika kukemea hali hiyo ya watu kutekwa nyara, hata hivyo polisi waliyapiga marufuku maandamano hayo, wakitishia kuwashughulikia watu watakaoandamana.