Human Rights Watch yaitaka Qatar kuachana na sheria za uongozi wa kiume

Human Rights Watch yaitaka Qatar kuachana na sheria za uongozi wa kiume

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Shirika la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch limeitaka Qatar kuiondoa sheria inayowapa wanaume mamlaka ya kuwasimania wanawake ili kuwapa wanawake uhuru wa kujifanyia maamuzi.

Maamuzi hayoni pamoja na ndoa, kusafiri na kupata huduma ya afya ya uzazi. Shirika hilo lililo na makao yake mjini New York, limesema baada ya Qatar kuchukua hatua juu ya haki za wanawake ikiwemo elimu na ulinzi wa wanawake katika jamii, nchi hiyo haijapiga hatua ikilinganishwa na majirani zake wa Ghuba, baada ya Saudi Arabia mnamo mwaka 2019 kuridhia wanawake walio na umri kuanzia miaka 21 kuweza kusafiri peke yao.

Mmoja kati ya wanawake 50 waliohojiwa na shirika la Human Rights Watch ameyaelezea na kufananisha maisha ya wanawake nchini Qatar kama ya watu walio karantini maisha yao yote. Hata hivyo serikali ya Qatar imesema taifa hilo linaendelea kusimamia sera zinazowapa wanawake uhuru wa kujiamulia mambo yao wenyewe.
 
Siyo suala la kuacha tu. Hiyo ina MIZIZI ya mila na desturi zao. Siyo kitu cha kukurupuka tu.
 
Back
Top Bottom