Humphrey Polepole ajibu mapigo baada ya Samia Suluhu Hassan kuchukua fomu ya urais 09 agosti 2025

Polepole anazungumza kwa "code" sio ngumu kuziekewa ila kama unavyofahamu elimu yetu, wachache Sana wenye upeo wa kuelewa!

Kuna member mmoja hapa JF alisema ili kumuelewa Polepole weka uzingativu kwenye Yale ambayo "ameruka"
Machawa vichwa ngumu aidha wanaelewa ila uchawa umewajaa wanajifanya awaelewi kitu, kwa akili za Zitto na Addo hadi awajajibu hujue Polepole kawagusa kisawa sawa.
 
Kama anazungumza na waTanzania code hazina msaada.
Msambaa au Mgogo au Masai ukiweka hizo code atazielewa lini? Unless anaongea na kakikundi chake fulani anakokijua.
Tsh kwanini usiweke jina lako kamili hapa na picha zako ili ufahamike?
 
Polepole anataka reform ili ccm ipambane na chama kubwa CHADEMA siyo Mpina na Salumu
 
Kwa magu ilitoka form moja hukuongea haya...
Huyo salum Kwan hana hadhi?
Bhc ungechukua na ww hio form ya kugombea au mlete unayetaka agombee unaezani ana hadhi hio
Kwa Magufuli 2020 ni utaratibu wa kawaida ndani ya chama, hata kikwete alichukua fomu moja 2010...

Mwaka huu ni tofauti.
 
Tsh kwanini usiweke jina lako kamili hapa na picha zako ili ufahamike?
Sababu JF ni kundi la wasiofahamika wakichanganyikana na wachache sana wanaofahamika.

Wakati unajaza fomu za kujiunga na kundi la wanaoanza shule ya msingi fomu yako ilikuwa na jina moja la misasa? Hapana, na sababu ilikuwa unajiunga na kundi la wanaofahamika tofauti na JF.
 
Kanuni za jf imekuzuia kuandika majina yako halisi?
 
Siasa ndiyo politics nakumbuka kina Aristotle, Plato, Cicero na wengineo
 
Pole pole , jana usiku kiukwel it was so crazy .

Ilikuwa raha sana ali play hadi nyimbo ya wahuni akiwa live .

Jamaa yupo vzr sana

Kasema Z Anto anatumika sio mpinzani halisi.
Hahahaaaaaa Polepole katufurahisha usiku wa kuamkia Leo baada ya kuita press conference kupitia akaunti zake kwa kushtukiza, kasema kuwa;

Uchaguzi wa mwaka huu ni kama uchaguzi uliowahi kutokea Afrika miaka mingi iliyopita kama 1884-1885 pale katika mji wa Berlin nchini ujerumani kuligawa bara la Afrika kwenda kwenye makoloni Yao kama uingereza, ujerumani, ufaransa,ureno,ubelgiji nk (Scramble and Partion for Africa).

Uchaguzi mwingine ni wa mwaka 1890 yaani Heligoland Zanzibar treaty. Ni pale wajerumani na waingereza walipokubaliana kusaini mkataba wa kupeana mfereji karibu na mto Zambezi.

Hahahaaaa Polepole anasema ACT WAZALENDO ni chama Cha kazi maalumu, CHAUMMA kazi maalumu haki ya nani mwaka huu tumepatwa,tukisema msiichague CCM Sasa wananchi wachague chauma ? Au ACT Wazalendo? Vyote ni vyama vya kazi maalumu,kwani nani haijui CHAUMMA ya Ubwabwa si ni CHADEMA walioasi wamekuja CHAUMMA wote ni wahuni tu, ACT Wazalendo na viongozi wake wote ni wahuni wale wale tu kazi maalumu.

Sijawahi kuona duniani kote taifa linaingia kwenye uchaguzi mkuu wakati kiongozi mkuu wa upinzani nchini Tanzania yupo gerezani,wasifikiri Dunia haioni inaona,msikate tamaa ni dalili ya ushindi.

Wanasema Dodoma palikuwa na shamrashamra hapana Bali walikusanyana kutoka Kila upande wa nchi hii na hawakuwa na dhamira ya dhati yenye furaha kuwa huyu ndiye mgombea urais wetu- Polepole.

Mama Samia unaenda kugombea urais na Salum Mwalimu utamkosoa nini huyu ? Yaaani ushinde urais kwa kumkosoa Salum Mwalimu? Kwa kumkosoa Luhaga Mpina mwana CCM mwenzetu? Tuamini umeshinda urais wa Tanzania? Hapana.-Polepole.

Mgombea urais na makamu ni batili hawajafuata mchakato wa ndani ya chama chetu CCM,kaamuru Kikwete iwe na ikawa bila kufuata katiba ya CCM,ni uhuni kataa wahuni. Huko mbele watakorogana tu kisiasa -Polepole.
 
Mgombea hana mvuto...Wala hana wadhamini, ccm imekosa pesa za watia Nia Urais ..fomu zingechukuliwa wapate mapato tatizo la majambazi halifikilii kuongeza mapato ya halali inajiwazia kuiba mali kwa ajili ya kuongeza mapato.
 
Kanuni za jf imekuzuia kuandika majina yako halisi?

Rejea kwenye jibu kuwa JF ni kundi la watu wasiofahamika pamoja na wachache wanaofahamika.

Huwezi kwenda upareni ukamuuliza mpare kwanini unaishi upareni. Ukikutana na msukuma upareni ndo unaweza muuliza ilikuwaje akachagua kuwa upareni.

JF wasiojulikana ni wengi, ni jamii ya wasiojulikana. (Fake id). Swali lako linamfaa anayeamua kuwa na id halisi.
 
Umemaliza πŸ™ŒπŸ‘πŸ‘‹ !
Nilishasema humu huyo Jamaa hawezi kuleta solutions katika matatizo yaliyopo kwa sababu yeye ni part of the Problem’s. 😳 !

Labda amekuja kuhamisha magoli ya moto wa no reforms no elections. πŸ˜…πŸ˜‚πŸ˜€ !

Watu wameshamstukia !
Vinginevyo amwage mchele wote kwenye kuku wengi ili tujue kweli yupo siriazi πŸ˜„πŸ™ŒπŸ‘

Hii janja janja ya kula hindi bichi wacha bhana Polepole πŸ˜³πŸ™„πŸ€·πŸΏβ€β™‚οΈ !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…