Elections 2015 Humphrey Polepole: CCM ilifanya maamuzi ya kiume, Majizi na hasa kubwa lao yakakatwa...

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Kwako Julius S. Mtatiro kwani zamani nilikuwaje?

Zamani nilisema wezi na majizi wanaoutaka Urais kupitia CCM wakatwe, na nikaendelea kusema wasingekatwa ningepiga kampeni CCM isichaguliwe, Wakati huo UKAWA-FEKI walikuwa wakichekelea chekelea. CCM ikafanya maamuzi ya kiume, Majizi na hasa kubwa lao wakakatwa. Hongera CCM.

Leo baada ya majizi kukatwa na kuelekea sehemu fulani kwa ndugu zangu, unatarajia nichekelee? Nitaendelea kusema wakatwe na kwasababu ndugu zangu wamehadaika na tamaa zao za madaraka (na fedha nono nono za kifisadi) na sio Mageuzi, na wao Nimewakataa.

Na nitaendelea kusema hii ni UKAWA-FEKI, sio ile ya Katiba, hawa ni wajanja wajanja, wanadhani ikulu wanakaa wajanja wajanja.

Nimewakataa

Sasa tofauti ya sasa na zamani na nikitizama misimamo yangu ni ipi? Mbona wewe ulisema Lowassa ana hela chafu anapelekea viongozi wenye njaa katika Makanisa? Au ni halali pesa chafu kuja kwako na kwa wenzio ndugu yangu?

Tofauti kubwa kwakweli ni kiwango cha juu cha matusi kutoka UKAWA-FEKI ndio kilichoongezeka. Ila kwa MITUSI MIKUBWA nyie NOMA.

Humphrey Polepole

Huyu mchambuzi ana hoja za msingi sana lakini kwakuwa anakwenda kinyume na matarajio ya UKAWA kipindi hichi cha uchaguzi basi anaonekana mpumbavu na lofa. Aliyokuwa anasimamia juu ya mgombea mwenye maadili CCM ndio hayo hayo anayosisitiza mpaka UKAWA.

Tuwe wakweli tuache kumshambulia Polepole, nakumbuka kabla ya Lowassa kuja UKAWA wapenzi wa CHADEMA pamoja na viongozi wao waandamizi walikuwa wakimshambulia sana Lowassa, rekodi zipo kwenye mitandao.Baada ya kukatwa huyo na kuhamia kwa wasakatonge basi wafuasi wa CHADEMA na UKAWA kwa ujumla wamejitoa akili na kusifia walichokuwa wakikipinga... Huu ni upumbavu.

Tubadilike tufanye siasa zenye mashiko tuweze kumpata kiongozi atakayeweza kutupeleka kwenye nchi ya ahadi.

Mimi kura yangu simpi kiongozi aliyeuza na kuifilisi ranchi ya Kitengule na kupeleka mradi wa maji Geita kwa sababu ana maslahi na madini kupitia kampuni dhalimu za madini, huku akiacha sehemu kubwa ya kanda ya Ziwa ikiwa haina maji.

Majibu Ya Julius Mtatiro
KWAKO NDUGU Humphrey Polepole, ENDELEA KUTUMIKIA MAJIZI MILIONI MOJA HUKO ULIKO!

Mimi napenda mijadala kama wewe na sina shaka katika hilo, tuendelee kujadiliana. Kuna watu unawaita majizi na wezi, kwamba mkubwa wao amekatwa na akaelekea kwa UKAWA-FEKI hii ya sasa na si ile ya BMK. Well and good brother.
Unachosahau ni kuwa, CCM ni kiwanda cha kuzalisha MAJIZI NA WEZI na wakiendelea kukaa hukohuko wanakuwa ni balaa na shida kubwa sana. MAJIZI na WEZI wengine wamekaa hadi IKULU na wakati wanaingia walitangaza mali zao na walipotoka madarakani walipoulizwa wana mali kiasi gani walikuja juu na kutukana, wengine walianzisha makampuni wakiwa ikulu na wengine wamejilimbikizia kila aina ya UKWASI, hawa unawajua lakini kwa sababu wewe ni CCM kindakindaki unaamini katika chama chako kuliko misingi.

Watu wengi walidhani misimamo yako katika katiba ni thabiti lakini ukweli ni kuwa kwa wanasiasa na vyama katiba ni jambo rahisi tu kutofautiana nao kuliko suala la kuendelea kushikilia madaraka ya dola. Ndiyo maana kwenye suala la katiba hata Ofisi ya Waziri Mkuu ilisema inataka serikali tatu japokuwa ilijua CCM inaamini katika serikali mbili. Jaji Warioba ambaye juzi alikuwa anamnadi Magufuli pia alihitaji serikali 3 kwa maana ya kutetea msimamo wa tume yake, hakuogopa kuwa watamshangaa. Leo limekuja suala la madaraka, wewe na wenzako hamuamini kama wapinzani wanaweza kuongoza dola, unaamini ni CCM tu ndiyo yenye uwezo wa kuongoza. Huu ni woga mkubwa sana kwa mtu ambaye hapo kabla alionekana anawaamini wapinzani kwa sababu ya kusimamia jambo kubwa kama katiba.

Unasema ati MAJIZI yalikatwa! Majizi ni yapi hayo? Na jizi KUU ni lipi hilo? Na huko kwenye kiwanda cha kuzalisha majizi yamebaki mangapi? Juzi wakati makada wa CCM wanashirikiana kuiba fedha za umma Bilioni 230 za ESCROW hilo jizi kubwa lilishiriki namna gani? Pale wizara ya ujenzi kwa rais wako Magufuli wakati mabilioni ya fedha yanaonekana kuporwa kwa mujibu wa ripoti za CAG hilo jizi kubwa lilihusikaje? Tunachotofautiana na wewe ni namna gani unautizama WIZI na UFISADI. Mimi nautizama kama KANSA ndani ya CCM na wewe unautizama kama JAMBO la MTU mmoja. Kwani hujui aliyeko madarakani leo anatuhumiwa kwa mambo lukuki tu? Mbona huyasemei? Unajua ukwasi wake ni kiasi gani? Unajua anajenda maghorofa na mahoteli mangapi? Umekaa kimya kwa sababu ni Kiranja mkuu japo najua hutafuti ukuu wa wilaya. Mfumo wa uongozaji wan chi kutoka CCM ni UOZO MTUPU na hapo ndipo tunatofautiana.

Hebu fuatilia kuona namna gani wabunge wa CCM na madiwani wamepitishwa ndani ya chama chao. Ni RUSHWA kuanzia jimbo kwa jimbo, kata kwa kata. Hii CCM unayoamini ati inaweza kusafishika haiwezi asilani, ni bora kufanya kazi nyingine kuliko kukisafisha chama ambacho juzi mlikiletea katiba bora kabisa ya kushughulikiwa MAJIZI NA MEZI MAKUBWA ikaikataa? Iliikataa ili kumlinda nani? Na aliyeongoza ukataaji yule unamjua, ni bwana mkubwa. Yeye humgusi na unajua who he is!

Ndiyo, nakubali kabisa kuitambua taswira ya huyu unayemuita JIZI KUU alipokuwa huko ndani ya CCM. Ndiyo, hadi leo na hadi kesho naamini kuwa watu wale waliokuwa wanakusanyika kwake walikuwa wananunuliwa tu, NDIYO. Na simlaumu kwa sababu huo ndiyo mfumo ambao uko huko, kununua watu. Ni kama leo hii namna ambavyo CCM itakuwa imetenga mabilioni ili kununua wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo na kata ili ishinde uchaguzi na impeleke Magufuli Ikulu. Mfumo wa huko CCM ni kununua tu. Mabalozi wa nyumba kumikumi waligawa fedha toka enzi za chama kimoja wakati Mwinyi anaingia madarakani, 1985 wakati mkapa anakuja unafahamu kuwa CCM ilikuwa kwenye wakati mgumu na kwa macho yangu nilishuhudia milungula ikigawiwa ili CCM ishinde, 2005 pia hali hiyo iliendelea kama ilivyo, ni kugawa rushwa tu. Kwa hiyo hakuna mtu aliyekuwa CCM na hatoi rushwa, labda ni Nyerere na Sokoine tu. Waliobakia wengine wote wananuka rushwa, si Lowassa, si Magufuli, Si Mkapa na si kila unayemfahamu. Wote walipata madaraka kwa njia za Rushwa, kwa hiyo huyu unayemuita JIZI MKUU lazima angetenda vile atendavyo na tuliwaona wagombea urais wenzake wakitenda hivyo kwa sababu huo ndiyo mfumo wenu.

Lakini kuwa katika JUKWAA jipya lenye taratibu jipya kunabadilisha kila kitu. Kama juzi alinunua viongozi wa dini n.k. walionunulika, leo hawezi kufanya hivyo kwa sababu huku kuna nguvu ya wananchi, huhitaji kununua. Lakini kaa chini utafakari kuwa huyu JIZI moja aliyeongoka na kuja upande huu na kupewa USUKANI mbona amewaacha MAJIZI kibao tu huko CCM ukijumuisha na yule aliyepewa USUKANI huko CCM? Sasa watanzania watakuwa na kazi ya kuchagua JIZI wa UKAWA ambaye amehamia kwenye sehemu isiyooza na inayofuata misingi, au JIZI la CCM lililobaki katika chama kilichooza, kilichojaa rushwa, wizi, ufisadi, unyonyaji n.k.

Naam, fikisha salamu zangu kwa majizi MILIONI MOJA yaliyobakia CCM na endelea kuyatumikia kwa utashi wako!
Ni mimi ndugu yako katika mijadala, Julius Sunday Mtatiro.

POST HII INAJIBU HOJA ZA POLEPOLE ZILIZOKO KWENYE LINK HII https://www.facebook.com/hpolepole?fref=ts, MJADALA UENDELEE!
 
Unapoiunga ccm mkono unamaanisha kuwa wezi majizi wametoka?
Ccm ikipita(najitia upofu) kwan ndo watabadili mcmamo wao juu ya katiba mpya??
'hatuwezi wapa nafac tena(watu walioongoza/tawala miaka zaidi ya 50) kwa ahadi zilezile, mitazamo ileile na 'chombo' kilekile'
 
Huyu mchambuzi ana hoja za msingi sana lakini kwakuwa anakwenda kinyume na matarajio ya UKAWA kipindi hichi cha uchaguzi basi anaonekana mpumbavu na lofa. Aliyokuwa anasimamia juu ya mgombea mwenye maadili CCM ndio hayo hayo anayosisitiza mpaka UKAWA.Tuwe wakweli tuache kumshambulia Polepole, nakumbuka kabla ya Lowassa kuja UKAWA wapenzi wa CHADEMA pamoja na viongozi wao waandamizi walikuwa wakimshambulia sana Lowassa, rekodi zipo kwenye mitandao.Baada ya kukatwa huyo na kuhamia kwa wasakatonge basi wafuasi wa CHADEMA na UKAWA kwa ujumla wamejitoa akili na kusifia walichokuwa wakikipinga... Huu ni upumbavu.

Tubadilike tufanye siasa zenye mashiko tuweze kumpata kiongozi atakayeweza kutupeleka kwenye nchi ya ahadi.

Mimi kura yangu simpi kiongozi aliyeuza na kuifilisi ranchi ya Kitengule na kupeleka mradi wa maji Geita kwa sababu ana maslahi na madini kupitia kampuni dhalimu za madini, huku akiacha sehemu kubwa ya kanda ya Ziwa ikiwa haina maji.
Andika vitu ulivyo na hakika navyo,Geita hakuna maji .Kama unazungumzia alivyopangua mkataba wa MTO NILE basi maji yalipelekwa mkoa wa shinyanga na bahadhi ya wilaya zake
 
Lowassa anamuona fisadi, lakini anapita huku na kule kuwapigia campaign kina Andrew Chenge, Nizar Karamagi na kuwashauri CCM waendelee kufadhiliwa na kina Rostam Aziz, Tanil Somaiya na mafisadi wengine ndani ya CCM!
 
KWAKO NDUGU Humphrey Polepole, ENDELEA KUTUMIKIA MAJIZI MILIONI MOJA HUKO ULIKO!

Mimi napenda mijadala kama wewe na sina shaka katika hilo, tuendelee kujadiliana. Kuna watu unawaita majizi na wezi, kwamba mkubwa wao amekatwa na akaelekea kwa UKAWA-FEKI hii ya sasa na si ile ya BMK. Well and good brother.
Unachosahau ni kuwa, CCM ni kiwanda cha kuzalisha MAJIZI NA WEZI na wakiendelea kukaa hukohuko wanakuwa ni balaa na shida kubwa sana. MAJIZI na WEZI wengine wamekaa hadi IKULU na wakati wanaingia walitangaza mali zao na walipotoka madarakani walipoulizwa wana mali kiasi gani walikuja juu na kutukana, wengine walianzisha makampuni wakiwa ikulu na wengine wamejilimbikizia kila aina ya UKWASI, hawa unawajua lakini kwa sababu wewe ni CCM kindakindaki unaamini katika chama chako kuliko misingi.

Watu wengi walidhani misimamo yako katika katiba ni thabiti lakini ukweli ni kuwa kwa wanasiasa na vyama katiba ni jambo rahisi tu kutofautiana nao kuliko suala la kuendelea kushikilia madaraka ya dola. Ndiyo maana kwenye suala la katiba hata Ofisi ya Waziri Mkuu ilisema inataka serikali tatu japokuwa ilijua CCM inaamini katika serikali mbili. Jaji Warioba ambaye juzi alikuwa anamnadi Magufuli pia alihitaji serikali 3 kwa maana ya kutetea msimamo wa tume yake, hakuogopa kuwa watamshangaa. Leo limekuja suala la madaraka, wewe na wenzako hamuamini kama wapinzani wanaweza kuongoza dola, unaamini ni CCM tu ndiyo yenye uwezo wa kuongoza. Huu ni woga mkubwa sana kwa mtu ambaye hapo kabla alionekana anawaamini wapinzani kwa sababu ya kusimamia jambo kubwa kama katiba.

Unasema ati MAJIZI yalikatwa! Majizi ni yapi hayo? Na jizi KUU ni lipi hilo? Na huko kwenye kiwanda cha kuzalisha majizi yamebaki mangapi? Juzi wakati makada wa CCM wanashirikiana kuiba fedha za umma Bilioni 230 za ESCROW hilo jizi kubwa lilishiriki namna gani? Pale wizara ya ujenzi kwa rais wako Magufuli wakati mabilioni ya fedha yanaonekana kuporwa kwa mujibu wa ripoti za CAG hilo jizi kubwa lilihusikaje? Tunachotofautiana na wewe ni namna gani unautizama WIZI na UFISADI. Mimi nautizama kama KANSA ndani ya CCM na wewe unautizama kama JAMBO la MTU mmoja. Kwani hujui aliyeko madarakani leo anatuhumiwa kwa mambo lukuki tu? Mbona huyasemei? Unajua ukwasi wake ni kiasi gani? Unajua anajenda maghorofa na mahoteli mangapi? Umekaa kimya kwa sababu ni Kiranja mkuu japo najua hutafuti ukuu wa wilaya. Mfumo wa uongozaji wan chi kutoka CCM ni UOZO MTUPU na hapo ndipo tunatofautiana.

Hebu fuatilia kuona namna gani wabunge wa CCM na madiwani wamepitishwa ndani ya chama chao. Ni RUSHWA kuanzia jimbo kwa jimbo, kata kwa kata. Hii CCM unayoamini ati inaweza kusafishika haiwezi asilani, ni bora kufanya kazi nyingine kuliko kukisafisha chama ambacho juzi mlikiletea katiba bora kabisa ya kushughulikiwa MAJIZI NA MEZI MAKUBWA ikaikataa? Iliikataa ili kumlinda nani? Na aliyeongoza ukataaji yule unamjua, ni bwana mkubwa. Yeye humgusi na unajua who he is!

Ndiyo, nakubali kabisa kuitambua taswira ya huyu unayemuita JIZI KUU alipokuwa huko ndani ya CCM. Ndiyo, hadi leo na hadi kesho naamini kuwa watu wale waliokuwa wanakusanyika kwake walikuwa wananunuliwa tu, NDIYO. Na simlaumu kwa sababu huo ndiyo mfumo ambao uko huko, kununua watu. Ni kama leo hii namna ambavyo CCM itakuwa imetenga mabilioni ili kununua wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo na kata ili ishinde uchaguzi na impeleke Magufuli Ikulu. Mfumo wa huko CCM ni kununua tu. Mabalozi wa nyumba kumikumi waligawa fedha toka enzi za chama kimoja wakati Mwinyi anaingia madarakani, 1985 wakati mkapa anakuja unafahamu kuwa CCM ilikuwa kwenye wakati mgumu na kwa macho yangu nilishuhudia milungula ikigawiwa ili CCM ishinde, 2005 pia hali hiyo iliendelea kama ilivyo, ni kugawa rushwa tu. Kwa hiyo hakuna mtu aliyekuwa CCM na hatoi rushwa, labda ni Nyerere na Sokoine tu. Waliobakia wengine wote wananuka rushwa, si Lowassa, si Magufuli, Si Mkapa na si kila unayemfahamu. Wote walipata madaraka kwa njia za Rushwa, kwa hiyo huyu unayemuita JIZI MKUU lazima angetenda vile atendavyo na tuliwaona wagombea urais wenzake wakitenda hivyo kwa sababu huo ndiyo mfumo wenu.

Lakini kuwa katika JUKWAA jipya lenye taratibu jipya kunabadilisha kila kitu. Kama juzi alinunua viongozi wa dini n.k. walionunulika, leo hawezi kufanya hivyo kwa sababu huku kuna nguvu ya wananchi, huhitaji kununua. Lakini kaa chini utafakari kuwa huyu JIZI moja aliyeongoka na kuja upande huu na kupewa USUKANI mbona amewaacha MAJIZI kibao tu huko CCM ukijumuisha na yule aliyepewa USUKANI huko CCM? Sasa watanzania watakuwa na kazi ya kuchagua JIZI wa UKAWA ambaye amehamia kwenye sehemu isiyooza na inayofuata misingi, au JIZI la CCM lililobaki katika chama kilichooza, kilichojaa rushwa, wizi, ufisadi, unyonyaji n.k.

Naam, fikisha salamu zangu kwa majizi MILIONI MOJA yaliyobakia CCM na endelea kuyatumikia kwa utashi wako!
Ni mimi ndugu yako katika mijadala, Julius Sunday Mtatiro.

POST HII INAJIBU HOJA ZA POLEPOLE ZILIZOKO KWENYE LINK HII https://www.facebook.com/hpolepole?fref=ts, MJADALA UENDELEE!
 
Bwana Polepole wewe kama msomi, mzalendo na muungwana, unapowaita watanzania wenzako tena pengine wenye umri sawa na wazazi wako unao wajibu pia na uwezo wa kuwafungulia mashtaka mahakamani. Thats what courageous and brave people do in modern civilised world. Haitoshi Bwana Polepole kupayuka kila siku bila kuchukua hatua muafaka. Ni mahakama peke yake yenye jukumu la kikatiba kuhukumu watanzania, vinginevyo unataka tuishi katika mazingira ya utamaduni wa porini/ushenzini!

Ni wazi sasa Polepole umejitishwa mzigo wa uchunguzi, mwendesha mashtaka na hakimu dhidi ya Lowasa. Sina hakika pia kama unao mpango na dhamira ya kuwashughulikia watuhumiwa wengine hasa kwa misingi ya Ripoti za CAG ambazo zimeweka bayana upotevu wa fedha za umma nyingi zaidi kuliko zile unazoshupalia kila uchao!

Kiu ya Watanzania ni kuleta mabadiliko ya dhati ili pamoja na mambo mengine kuziba mianya ya ufisadi na kuimarisha taasisi zenye uwezo wa kuchukua hatua kila matendo ya ufisadi yanapojitokea. Watanzania hawana tatizo na watu binafsi au fisadi mmojammoja, bali mifumo ya utawala ambayo kimsingi imedumu zaidi ya miaka 50 sasa ikiwemo - "imperial presidency". This is the essence of the Change we yearn for. Sasa madhalo Lowasa amekubali kutekeleza sera ya UKAWA ya kutupatia katiba mpya kwa misingi ya maoni ya wananchi, huyo ndiye anastahili kuwa Rais wa Tanzania baada ya uchaguzi wa 25th Oktoba, 2015.
 
Andrew Chenge, William Ngeleja, Anna Tibaijuka, Profesa Muhongo hawa wamekatwa?
Njaa tuzipeleke polepole.

soma vizuri mkuu utamwelewa, kasema kubwa lao limekatwa, hao wengine wanadhibitika, ila lileeeeeee.
 
Kubwa lao kwa mujibu wa nani? Kazi ya vikao vya maadili ni nini? Kuna mtu mbaya kama Chenge? Kuna deal gani amekosekana?

Halafu kibaraka hii ID nimeshaitambuwa hata kuke Facebook. Akili zako zimejaa funza.
 
Mi nasubiri nipate ripoti ya Dr.ndo niweze kuchangia chochote,sidhani kama polepole yuko sawa!majuzi alibanwa na mchungaji adi povu likamtoka.
 
Unapoiunga ccm mkono unamaanisha kuwa wezi majizi wametoka?
Ccm ikipita(najitia upofu) kwan ndo watabadili mcmamo wao juu ya katiba mpya??
'hatuwezi wapa nafac tena(watu walioongoza/tawala miaka zaidi ya 50) kwa ahadi zilezile, mitazamo ileile na 'chombo' kilekile'

mwana nimekukalili usipojitia upofu nakutafuta nakutoboa macho
 
Huyu mchambuzi ana hoja za msingi sana lakini kwakuwa anakwenda kinyume na matarajio ya UKAWA kipindi hichi cha uchaguzi basi anaonekana mpumbavu na lofa. Aliyokuwa anasimamia juu ya mgombea mwenye maadili CCM ndio hayo hayo anayosisitiza mpaka UKAWA.

Tuwe wakweli tuache kumshambulia Polepole, nakumbuka kabla ya Lowassa kuja UKAWA wapenzi wa CHADEMA pamoja na viongozi wao waandamizi walikuwa wakimshambulia sana Lowassa, rekodi zipo kwenye mitandao.Baada ya kukatwa huyo na kuhamia kwa wasakatonge basi wafuasi wa CHADEMA na UKAWA kwa ujumla wamejitoa akili na kusifia walichokuwa wakikipinga... Huu ni upumbavu.

Tubadilike tufanye siasa zenye mashiko tuweze kumpata kiongozi atakayeweza kutupeleka kwenye nchi ya ahadi.

Mimi kura yangu simpi kiongozi aliyeuza na kuifilisi ranchi ya Kitengule na kupeleka mradi wa maji Geita kwa sababu ana maslahi na madini kupitia kampuni dhalimu za madini, huku akiacha sehemu kubwa ya kanda ya Ziwa ikiwa haina maji.

Nimefuatilia kwa makini sana hoja za Hamfrey pole pole.Nathubutu kusema mwanzo nilidhani ni kijana mzalendo anaeipenda nchi yake tena mkweli lakini nimegundua yafuatayo kutoka kwa Polepole.

1. H Polepole ana chuki binafsi na Mgombea wa upinzani.kwa nini nasema hivyo kabla ya uteuzi wa wabunge Polepole alisema ccm inapaswa kuwakata wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi na kama hawatafanya hivyo alikuwa tayari kuisema ccm nchi nzima.Mara baada ya uteuzi kupita na wale wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi kupita Polepole amegeuka na kuacha hoja hiyo.hiyo inaonyesha ana chuki na mgombea wa Ukawa.

2. Katika nchi ufisadi uliofanyika ni mkubwa sana na waliofisadi nchi wako wengi sana na pole pole anawajuwa lakini hajawahi hata siku moja kuwataja kwa Polepole ufisadi ni Richmond pekee vipi kuhusu EPA, Kagoda, meremeta, Escrow.uuzaji wa nyumba za serikali, uuzaji wa viwanda. Tukitaka kuiokoa nchi yetu basi tuwe wa kweli bila upendeleo.Chuki anayoionyesha pole pole ni ya wazi mno.

3. CCM ni chama chetu lakini kuna mambo mengi mabaya yaliyofanyika tuyaseme ili tukiokoe chama chetu.
Mgombea wetu ametoa hotuba inayoonyesha udhaifu mkubwa katika mambo mengi yanayohitaji kurekebishwa tuyaseme kwa uwazi kama Dr Pombe anavyosema. Mgombea wetu hashambulii mtu anaongelea hoja.polepole jikite kwenye hoja za kujenga nchi si kila siku unamshambulia mtu mmoja kama vile wewe huna dhambi Acha chuki haijengi.
 
Kwa mjibu wa viongozi na wafuasi wa cdm ,kama lowasa angekuwa fisadi basi angekuwa kashafungwa.na wanakwenda mbali zaidi na kusema aliye na ushaidi kuwa lowasa ni fisadi auweke hadharani au aende mahakamani.kwa sababu hizo,hata chenge,mhongo,ngereja,tibaijuka,rostam,karamagi n.k sio mafisadi pia,kwa sababu nao hawajashitakiwa mpaka sasa.Hivyo ccm hakuna fisadi hata mmoja.
 
Back
Top Bottom