Sitaki kuamini kama mdogo wangu Polepole nae kanunuliwa but kilicho dhahiri kwake ni kwamba Polepole ana chuki binafsi na Lowassa; nitafafanua.
1. Polepole amepata umaarufu kupitia tume ya katiba ile ya mzee Warioba, msimamo wake ju ya katiba pendekezwa upo dhahiri, mgombea mwenza wa ccm alikua msaidizi wa mwenyekiti wa bunge la katiba, huyu mama pamoja na chama chake walikataa kataka kuipitisha ile rasmu yao, Polepole haoni kama kuna tatizo kwake, tatizo analiona kwa Lowassa tu.
2. Nchi ina kashfa kadhaa za ufisadi, nitaja chache, IPTL, Rada, ndege ya raisi, uuwaji holela wa wanyama kama Tembo, Faru na Twiga, Richmond/Dowans/Symbion, Epa, Deep green finance, Meremeta, ujenzi wa minara pacha pale BOT bila kusahau Escrow, yooote hayo jina la Lowassa linatajwa kwenye Ricmond/Dowans peke yake. Sitaki pia kuamini kama Polepole hamjui Mr. Richmond ni nani? Dr. Mwakyembe aliisha twambia mule mule Bungeni; hapa napo macho ya Polepole yana muona Lowassa tu ya dealers wengine hayaoni.
3. CCM wameuza nchi (ccm kama chama na sio mtu) nina hakika Polepole anajua vizuri sana uuzwaji holela wa mashirika yaliokua yakifanya vizuri kibiashara kama NBC bank n.k, uuzwaji wa nyumba za serikali na hasara tunayoipata sasa hvi kama wananchi, yipo mwingine aliyeratibu zoezi hilo akampa na girl friend wake nyumba 1 na mtu huyo sasa hvi ndio mgombea wa chama chake kwenye nafasi ya uraisi (sitaki kuamini kama polepole halijui hili) but YES, still macho ya Humfrey yamepigwa upofu upande huo yana ona kwa Lowassa tu.
Namshauri mdogo wangu huyu (narudia, sitaki kuamini kama na yeye kanunuliwa) aanze kuvaa miwani ili macho yake yawe yanaona pande zote na sio upande mmoja tu.