Bwana Polepole wewe kama msomi, mzalendo na muungwana, unapowaita watanzania wenzako tena pengine wenye umri sawa na wazazi wako unao wajibu pia na uwezo wa kuwafungulia mashtaka mahakamani. Thats what courageous and brave people do in modern civilised world. Haitoshi Bwana Polepole kupayuka kila siku bila kuchukua hatua muafaka. Ni mahakama peke yake yenye jukumu la kikatiba kuhukumu watanzania, vinginevyo unataka tuishi katika mazingira ya utamaduni wa porini/ushenzini!
Ni wazi sasa Polepole umejitishwa mzigo wa uchunguzi, mwendesha mashtaka na hakimu dhidi ya Lowasa. Sina hakika pia kama unao mpango na dhamira ya kuwashughulikia watuhumiwa wengine hasa kwa misingi ya Ripoti za CAG ambazo zimeweka bayana upotevu wa fedha za umma nyingi zaidi kuliko zile unazoshupalia kila uchao!
Kiu ya Watanzania ni kuleta mabadiliko ya dhati ili pamoja na mambo mengine kuziba mianya ya ufisadi na kuimarisha taasisi zenye uwezo wa kuchukua hatua kila matendo ya ufisadi yanapojitokea. Watanzania hawana tatizo na watu binafsi au fisadi mmojammoja, bali mifumo ya utawala ambayo kimsingi imedumu zaidi ya miaka 50 sasa ikiwemo - "imperial presidency". This is the essence of the Change we yearn for. Sasa madhalo Lowasa amekubali kutekeleza sera ya UKAWA ya kutupatia katiba mpya kwa misingi ya maoni ya wananchi, huyo ndiye anastahili kuwa Rais wa Tanzania baada ya uchaguzi wa 25th Oktoba, 2015.