Uchaguzi 2020 Humphrey Polepole: Dkt. Magufuli atachukua fomu ya Urais 06 Agosti Dodoma. Mwanachama aliyepiga mazonge kwenye kura za maoni atashikishwa adabu

Uchaguzi 2020 Humphrey Polepole: Dkt. Magufuli atachukua fomu ya Urais 06 Agosti Dodoma. Mwanachama aliyepiga mazonge kwenye kura za maoni atashikishwa adabu

Mwenezi wa CCM ndugu Polepole amesema chama chake kimesikitishwa na kitendo cha Chadema kupora kaulimbiu ya TID ijulikanayo kama Ni Yeye

Polepole amesisitiza kuiburuza Chadema mahakamani ili TID apate haki yake.

Maendeleo hayana vyama!
 
Nimwombe, ajikite kwenye sera za Chama Chetu. Mambo ya kujibu mapigo au kuzungumzia vyama vingine "SIYO KAZI YAKE" ni kazi ya Msajili wa vyama na NEC.

😂😂😂 Ndo hayo hayo ameenda ongelea .
Vipi wewe ndo ulimuandalia ya kwenda kusema nini? au ndo ushakariri akili za ccm zilivyo.?
 
Ambacho kitanichekesha ni pale Chadema itacounter kwa kusema kua TID hana hatimiliki na hilo neno kisha inaletwa hatimiliki ya hilo neno ambayo itaonyesha TID ana hatimiliki tangu 2003.

Lissu; Police unasema ulisikia Bananga akisema Polisi lazima washikishwe ukuta mwaka huu, si ndio?

Polisi: Ndio alisema

Lissu:Je,kushika ukuta ni kosa? Mh. hakimu naomba Polisi atusaidie kushika ukuta uliopo hapa mahakamani tuone

Hakimu; Police hebu shika huo ukuta tuone.

Polisi anashika ukuta.

Lissu: Sasa mh. hakimu naomba police anionyeshe aliposhika huo ukuta ni sheria gani ya nchi imevunjwa.

Police: Hakuna sheria yoyote ile iliyovunjwa mh. Hakimu.

Hakimu: Hakuna sheria yoyote imevunjwa kwa police kushika huo ukuta wala kwa neno lililotumika la kuwashikisha ukuta police,Mtuhumiwa Bananga yuko huru kuanzia sasa.

Sasa nna hamu ya kumuona TID vs Lissu mahakamani.
 
Waliopora nembo ya M4C mwaka 2015 walikuwa ni chama gani?

Na je,TID ana hati miiki ya hiyo slogan?

Na,wana uhakika gani kama wameiba?

Na,slogan hiyo imetumiwa na chama kama chama au imetumiwa tu na baadhi ya wanachama kwa mapenzi yao?
 
Nimemsikiliza Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, "akijimwambafai" katika mkutano wake na waandishi wa habari, ambao kwa asilimia zaidi ya 90, aliutumia kwa kukiponda chama cha Chadema na kuwaita viongozi wake kuwa ni wahuni na chama hicho ni uvumilivu tu ndiyo "unaowalazimisha" kuwa kiwepo, bila hivyo chama hicho hakina hata uhalali wa kuwepo hapa nchini!

Aliendelea kudai kuwa viongozi wa Chadema, akina Mbowe, kuwa ni wahuni tuu!

Nimekuwa nikijiuliza, hivi chama cha Chadema, si kimesajiliwa kihalali kuwa chama cha siasa na kutambulika na msajili wa vyama vya siasa?

Iweje yeye Polepole aseme kuwa chama hicho hakina uhalali wa uwepo wake?
 
Katibu wa NEC - Itikadi na Uenezi ndugu Polepole ataongea na watanzania kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
Mkutano utafanyika ofisi ndogo ya CCM - Lumumba, Dar es Salaam. Usipange kukosa kufuatilia.




Ule mswada wa waandishi wa habari angalau wawe na elimu yenye ngazi Advanced Diploma leo ndio nimeona uhalisia wake , Waandishi wa Habari mnakwama wapi? Duh yani mpaka aibu.... ndio vitu gani mlikuwa mkiuliza , yaani mda wote wa propaganda za PRO mlishindwa kutunga maswali yenye afya?
 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, @hpolepole amesema CHADEMA imemdhulumu msanii TID kwa kutumia kauli ya "Ni Yeye" bila kumuomba wala kumshirikisha. “Ni Yeye ilikuwa ya Magufuli, wale majamaa wameichomeka kule hawajamshirikisha kwa kweli sisi Watanzania tutawachukulia hatua." https://t.co/8cG6TFs3TA

================
Kuna video imesambaa Mitandaoni ikimwonyesha Tid akilalamika Chadema kutumia msemo wake bila idhini yake.

Sasa leo CCM wametangaza kuwachukulia hatua Chadema kwa kutumia msemo wa mtu bila taarifa ya TID.

Kwa CCM lolote linawezekana tusishangae Tid akiibuka na nyaraka za umiliki wa huo msemo na ukionyesha amesajili miaka miwili nyuma.
 
Nimemsikiliza Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, "akijimwambafai" katika mkutano wake na waandishi wa habari, ambao kwa asilimia zaidi ya 90, aliutumia kwa kukiponda chama cha Chadema na kuwaita viongozi wake kuwa ni wahuni na chama hicho ni uvumilivu tu ndiyo "unaowalazimisha" kuwa kiwepo, bila hivyo chama hicho hakina hata uhalali wa kuwepo hapa nchini!..
Utaona sasa kama msajili atakionya CCM na kumkanya Polepole kwa kutumia Lugha za maudi/kejeki/kichochezi,ila subiri sasa Lissu atumie lugha kama hio kwa mwenyekiti wa Ccm uone msajili atakavyokurupuka kule aliko.
 
Back
Top Bottom